Kwa nini tume inachelewa kutangaza matokeo Igunga? Vurugu zimeanza

dedam

JF-Expert Member
Jan 5, 2011
845
165
Matokeo hayajatangazwa mpaka sasa labda mpaka mchana ila ushindani ni mkali ccm na cdm source bbc swahili saa 12

==============
UPDATE
==============

Wale wenye access, watch Channel Ten Now!

Mwandishi wa Channel Ten Tabora, Juma Kapipi ameripoti live kuwa mapanga yameanza kutembea Igunga!.

Kwa mujibu wa Kapipi, vurugu hizo zimeanza pale wafuasi wa Chadema, walipojitokeza mitaani asubuhi hii kujipanga kuivamia ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi wakidai haki yao ya ushindi.

Katika rabsha hiyo, kundi hilo la wafuasi wa Chadema, waliizingira hoteli waliofikia viongozi wa CCM na kuleta fujo kubwa ikiwepo kutupa mawe na kuvunja vioo gari moja ya Landcruiser Prado. Ndipo kundi la watu wanaodhaniwa kuwa ni wafuasi wa CCM, liliibuka kutoka ndani huku wameshika mapanga, na kuwasambaratisha wafuasi hao wa Chadema, ambapo kuona mapanga, kila mmoja alishika njia yake kujiokoa maisha yao!.

Baadhi ya wafuasi wa Chadema waliofurushwa, waliliripoti tukio hili polisi, na mara polisi na FFU walifika na kuizingira hoteli hiyo, ikiwemo kuingia hotelini humo kuyasaka mapanga hayo, cha ajabu, hakuna hata panga moja lililopatikana!.

Kapipi amesema, maduka yamefungwa, FFU wametanda likiwemo lile gari la maji ya upupu, ila amani imedibitiwa.

Mtangazaji David Ramadhani, aliwatafuta viongozi wa CCM, Chadema na Jeshi la Polisi kuzungumzia hali hiyo.

Mpaka sasa Ch.10 iko hewani Charles Hilila akihojiana na Studio.

Naomba Kuwakilisha.

Pasco.
 
Matokeo hayajatangazwa mpaka sasa labda mpaka mchana ila ushindani ni mkali ccm na cdm source bbc swahili saa 12
Ndugu yangu si ZITTO walaDK SLAA waliothubutu kutoa matokeo hapa JF, DK KIGWANGALA na NAPE ndio wanao tamba humu JF alfajiri hadi asubuhi hii bado ujasoma alama za nyakati?
 
magamba kabla hata kura hazijapigwa walisema wameshinda na usishangae nape akawa na figure zake na wengine figure tofauti
 
Haipendezi kuwa Mzandiki Nape ambaye alifukuzwa kutoshiriki Uchaguzi huko anajipendekeza kuwa CCM wamishinda lakini tume haijamaliza Ni wizi mtupuuu!!!!!
 
kwan dr slaa yupo wapi kutangaza naye yake?,ebwana kama noma na iwe noma hawa magamba wamezid ushenzi. Mi napatwa na hasira jaman CCM wanavyo2fanyia watz
 
wanaendelea kuchakachua,pia najiuliza viongozi wote wa serikali walipokuwa igunga wanalipwa na nani?
 
Hata mafisadi wakishinda bado chamoto wamekiona! tunajua ni uchakachuaji tu umefanyika. mwaka 2015 wapinzani wasikubali kuingia kwenye uchaguzi bila tume huru.CDM msikate tamaa endeleeni kupambana hadi mafisadi watokomee!
 
CDM inaongoza Nape huna chako pale Magamba wamekugeuka saiv huna kitu wewe kaa unaruka ruka pembeni tu...na moyoni mwako unajua wale sio wenzio...
 
Kwa kweli hapa vyama vitakuwa vimejifunza kuwa watu wanataka mabadiliko.
Kumbe yale matokeo aliyotoa Nape ni feki??
 
Leo ni siku ya pili tangu uchaguzi ufanyike hapo jana kwenye jimbo la igunga, tume imeshindwa kwani sababu zote zinazotolewa ni uzembe wa tume ya uchaguzi kutojipanga vizuri.

Sasa kama jimbo moja tu kutangaza matokeo inakuwa issue itakuwaje kwa uchaguzi mkuu? tume jipangeni bwana, igeni nchi nyingine zinafanya nini au zinatumia jitihada gani au maandalizi gani wanayafanya kutangaza matokeo mapema.

Tambueni kwamba tume ya uchaguzi inapochelewa kutangaza matokeo mapema wananchi wanakosa imani na tume. sometime vurugu zinazotokea kwa kuchelewa kutangaza matokeo zinasababishwa na ninyi wenyewe
.
 
CDM inaongoza Nape huna chako pale Magamba wamekugeuka saiv huna kitu wewe kaa unaruka ruka pembeni tu...na moyoni mwako unajua wale sio wenzio...
ktk ofisi za cdm namwona waitara akitangaza kuwa hadi saa 12 asubuh cdm ilikuwa inaongoza. Watu wanakusanyika kwenda halmashauri, rabsha inatokea hapa piki lodge wafas wa ccm wenye mapanga wamevamia maandamano ya cdm, cdm nao wamejibu kwa mawe ni vurugu tupu, naona polisi wameingilia na wa2 wamesambaa.
 
cuf wameuza kura zao kwa wapenzi wao ili chadema isishinde. kifo cha cuf bara ni dhahiri!
 
Wanachama na wapenzi wa cdm wamekizunguka kituo cha kutangaza matokeo wakiwa ni wengi kwa mamia na kuna askari wengi sana na magari ya washawasha. Wanaimba wimbo wa Mungu bariki cdm. Madai yao ni matokeo yatangazwe kwani muda tayari umepita na uchakachuaji unafanyika.Je matokeo tunayotangaziwa na Nape, Mtanzania, kwamba ccm wameshinda yametoka wapi?

Source Radio 5
 
Matokeo ya nape na cyprian musiba ni feki musiba alitoa matokeo kabla hata vituo havijafungwa na saa tano usiku akarudi akisema chadema wanaongoza sio mchuano mkali tena,matokeo bado!
 
NEC ndo wanataka hivyo, hakuna sababu yeyote ya kuendelea na mfumo mbovu kama wa NEC wakati kila siku watu wanaimba TECHNOHAMA. Hawataki kutumia vipesa kidogo kwa ajili kujenga miundo mbinu yao ya habari. Hata kama CCM wameshinda, watasababisha vurugu visivyokuwa na ulazima.
 
Back
Top Bottom