dedam
JF-Expert Member
- Jan 5, 2011
- 845
- 165
Matokeo hayajatangazwa mpaka sasa labda mpaka mchana ila ushindani ni mkali ccm na cdm source bbc swahili saa 12
==============
UPDATE
==============
==============
UPDATE
==============
Wale wenye access, watch Channel Ten Now!
Mwandishi wa Channel Ten Tabora, Juma Kapipi ameripoti live kuwa mapanga yameanza kutembea Igunga!.
Kwa mujibu wa Kapipi, vurugu hizo zimeanza pale wafuasi wa Chadema, walipojitokeza mitaani asubuhi hii kujipanga kuivamia ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi wakidai haki yao ya ushindi.
Katika rabsha hiyo, kundi hilo la wafuasi wa Chadema, waliizingira hoteli waliofikia viongozi wa CCM na kuleta fujo kubwa ikiwepo kutupa mawe na kuvunja vioo gari moja ya Landcruiser Prado. Ndipo kundi la watu wanaodhaniwa kuwa ni wafuasi wa CCM, liliibuka kutoka ndani huku wameshika mapanga, na kuwasambaratisha wafuasi hao wa Chadema, ambapo kuona mapanga, kila mmoja alishika njia yake kujiokoa maisha yao!.
Baadhi ya wafuasi wa Chadema waliofurushwa, waliliripoti tukio hili polisi, na mara polisi na FFU walifika na kuizingira hoteli hiyo, ikiwemo kuingia hotelini humo kuyasaka mapanga hayo, cha ajabu, hakuna hata panga moja lililopatikana!.
Kapipi amesema, maduka yamefungwa, FFU wametanda likiwemo lile gari la maji ya upupu, ila amani imedibitiwa.
Mtangazaji David Ramadhani, aliwatafuta viongozi wa CCM, Chadema na Jeshi la Polisi kuzungumzia hali hiyo.
Mpaka sasa Ch.10 iko hewani Charles Hilila akihojiana na Studio.
Naomba Kuwakilisha.
Pasco.