Kwa nini tume inachelewa kutangaza matokeo Igunga? Vurugu zimeanza

Duuuuuuuuuuuuuuu! Tume ya uchaguzi wanatupeleka wapi jimbo moja tu matokeo hayajatoka mpaka saizi na vituo vilifungwa jana saa kumi jioni!
 
Tangu lini wanyamwezi wakajua kucharangana mapanga?

Hii habari ina walakini, labda vibaka watakuwa wamekurupushwa wakitaka kuiba, sio sababu ya uchaguzi.
 
Mkuu ukifikiria sana unaweza kujiumiza bure!! Ni kuwa na subira tu. Ila wanauzi sana, watu wenyewe computer wanaijua basi, wanatafuta herudi kwa tochi kwenye hiyo keyboard. Wamejazana wajomba na maanko. Vurugu zikitokea nani alaumiwe. Mkuu Omr, sawa wapige risasi lakini sidhani kama ndo unapenda itokee hivyo lazima kuna sehemu ya akili yako itakuwa inasema kwa sauti ya chiniiiiiiiii "hapana ccm wamezidi hata kama ni shabiki lao"
mimi sio shabiki wa CCM, mimi ni CCM yenyewe.
 
ni kweli.

Wa Jikoni amenitonya pia.

CCM ndiyo wana mapanga, waliocharangwa ni wafuasi wa chadema waliokuwa wanapita karibu na gesti (walipokuwa CCM na mapanga yao), na CCM wakaaza kuwazomea Chadema, hali iliyopelekea Chadema kuwavaa wapinzani wao.

Mapanga yametembea.

Gari imevunjwa vioo.

Taarifa kwa mujibu wa Wa Jikoni.
 
Wanachama na wapenzi wa cdm wamekizunguka kituo cha kutangaza matokeo wakiwa ni wengi kwa mamia na kuna askari wengi sana na magari ya washawasha. Wanaimba wimbo wa Mungu bariki cdm. Madai yao ni matokeo yatangazwe kwani muda tayari umepita na uchakachuaji unafanyika.Je matokeo tunayotangaziwa na Nape, Mtanzania, kwamba ccm wameshinda yametoka wapi?

Source Radio 5


ccm yaanza kutembeza mapanga source c ten
 
itabidi tuendelee kukubali kulazimishwa hivyo hivyo tu siku zote, aidha kwa maamuzi ya wananchi au kwa maamuzi ya wenye nguvu wa nchi hii.
 
kumbuka msimamizi wa uchaguzi ni mkurugenzi wa wilaya ambapo hapo kuna mlolongo wa vyeo visivyopungua 30 kuja kumfikia rais ambaye naye anaweza kuwa anataka matokeo yawe in their favor!
Kwa maana hiyo msimamizi anaweza kuwa na matokeo tayari lakini wazee walio juu yake, 'waajiri wake', wanajaribu kupoteza ushahidi wa kupelekwa kwa Ocampo - The Hague
Duuuuuuuuuuuuuuu! Tume ya uchaguzi wanatupeleka wapi jimbo moja tu matokeo hayajatoka mpaka saizi na vituo vilifungwa jana saa kumi jioni!
 
Mh, kutachimbika Igunga ila jamani daima amani iwe mbele! Na daima TANGANYIKA kwanza!
 
Back
Top Bottom