Kwa nini tume inachelewa kutangaza matokeo Igunga? Vurugu zimeanza

NEC ndo wanataka hivyo, hakuna sababu yeyote ya kuendelea na mfumo mbovu kama wa NEC wakati kila siku watu wanaimba TECHNOHAMA. Hawataki kutumia vipesa kidogo kwa ajili kujenga miundo mbinu yao ya habari. Hata kama CCM wameshinda, watasababisha vurugu visivyokuwa na ulazima.

miundombinu bora haitaruhusu wizi wa kura, ndio maana hawataki.
 
mkileta fujo tunapiga risasi tu. Dr. Kikwete alishasema hataki uhuni Igunga.
 
NEC ndo wanataka hivyo, hakuna sababu yeyote ya kuendelea na mfumo mbovu kama wa NEC wakati kila siku watu wanaimba TECHNOHAMA. Hawataki kutumia vipesa kidogo kwa ajili kujenga miundo mbinu yao ya habari. Hata kama CCM wameshinda, watasababisha vurugu visivyokuwa na ulazima.

Unajua TZ uzushi mwingi.

Hawa NEC wanasema ati wanatumia technologia ya computer...sawa lakini wenyewe wanamaanisha matumizi ya excel sheet kujumlisha....
hivi kwa dunia ya leo excel sheet bado ni technologia NEC wanajisifia.

Wewe kama hawana network na vituo vyote wanategemea karatasi zifikishwe ndio waingize kwenye spread sheet huu ni Ukale....
Viongozi wetu wanapenda sana kuongea uongo hasa pale wanapojua wananchi walio wengi hawaijui hata hiyo computer
 
Unajua TZ uzushi mwingi.
Hawa NEC wanasema ati wanatumia technologia ya computer...sawa lakini wenyewe wanamaanisha matumizi ya excel sheet kujumlisha....
hivi kwa dunia ya leo excel sheet bado ni technologia NEC wanajisifia.
Wewe kama hawana network na vituo vyote wanategemea karatasi zifikishwe ndio waingize kwenye spread sheet huu ni Ukale....
Viongozi wetu wanapenda sana kuongea uongo hasa pale wanapojua wananchi walio wengi hawaijui hata hiyo computer


Mkuu ukifikiria sana unaweza kujiumiza bure!! Ni kuwa na subira tu. Ila wanauzi sana, watu wenyewe computer wanaijua basi, wanatafuta herudi kwa tochi kwenye hiyo keyboard. Wamejazana wajomba na maanko. Vurugu zikitokea nani alaumiwe. Mkuu Omr, sawa wapige risasi lakini sidhani kama ndo unapenda itokee hivyo lazima kuna sehemu ya akili yako itakuwa inasema kwa sauti ya chiniiiiiiiii "hapana ccm wamezidi hata kama ni shabiki lao"
 
Wandugu, what's happening? Kuchelewesha kutangaza matokeo ya uchaguzi mdogo Igunga ni mbinu isiyo nzuri kabisa...
 
Mtalijua jiji na matokeo yenu... Taarifa zlizopo CDM inaongoza.. 2me ya uchaguz ina haha... Kuchakachua matokeo..
 
It looks CCM wameshinda! Fine, wameshinda lakini wameshindwa vibaya sana, kutoka uchaguzi wa mwaka jana inaonekana wameporomoka kwa zaidi ya kura 9,000, viashiria vinazidi kuonyesha kuwa CCM haikubariki!

Ni ushindi mwembamba sana kwa chama tawala na kwa nafasi hii napenda kuwapongeza sana CHADEMA kwa mafanikio makubwa waliyoyapata na wanayoendelea kuyapata nchini.

CHADEMA tambueni kuwa tayari CCM wanauhakika kuwa mmekaribia kabisa kutwaa Dola na wanajaribu kila njia kuwadhoofisha. Now a way-forward, Fungua matawi ngazi zote za vijiji, kata, hadi wilayani, simika mizizi, hii nchi ni ya CHADEMA kwa sasa.

Tunafurahia ushindi huu kwa CHADEMA kwa kuwa imejidhihirisha kuwa chama kina uwezo mkubwa wa kujieleza, kueleweka na sera safi. Ninasema tena Hongereni CHADEMA hamjachaguliwa ila mmeshinda! Ninyi ni washindi.
 
Wadau wanasema NEC - igunga wanajaza matokeo kwenye computer, sasa si unajua tena kama watu wa Dar wanazitafuta herudi kwenye keyboard itakuwaje huko kwetu Ukenyenge na Igunga ambako shule nzima ya sekondari inawalimu 3 (F1 - F4), shule ya msingi nako hivyo hivyo. INternet ndo wameijua baada ya RA kujiuzuru nyadhifa zote ndani ya chama.
 
Wale wenye access, watch Channel Ten Now!

Mwandishi wa Channel Ten Tabora, Juma Kapipi ameripoti live kuwa mapanga yameanza kutembea Igunga!.

Kwa mujibu wa Kapipi, vurugu hizo zimeanza pale wafuasi wa Chadema, walipojitokeza mitaani asubuhi hii kujipanga kuivamia ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi wakidai haki yao ya ushindi.

Katika rabsha hiyo, kundi hilo la wafuasi wa Chadema, waliizingira hoteli waliofikia viongozi wa CCM na kuleta fujo kubwa ikiwepo kutupa mawe na kuvunja vioo gari moja ya Landcruiser Prado. Ndipo kundi la watu wanaodhaniwa kuwa ni wafuasi wa CCM, liliibuka kutoka ndani huku wameshika mapanga, na kuwasambaratisha wafuasi hao wa Chadema, ambapo kuona mapanga, kila mmoja alishika njia yake kujiokoa maisha yao!.

Baadhi ya wafuasi wa Chadema waliofurushwa, waliliripoti tukio hili polisi, na mara polisi na FFU walifika na kuizingira hoteli hiyo, ikiwemo kuingia hotelini humo kuyasaka mapanga hayo, cha ajabu, hakuna hata panga moja lililopatikana!.

Kapipi amesema, maduka yamefungwa, FFU wametanda likiwemo lile gari la maji ya upupu, ila amani imedibitiwa.

Mtangazaji David Ramadhani, aliwatafuta viongozi wa CCM, Chadema na Jeshi la Polisi kuzungumzia hali hiyo.

Mpaka sasa Ch.10 iko hewani Charles Hilila akihojiana na Studio.

Naomba Kuwakilisha.

Pasco.
 
Leo ni siku ya pili tangu uchaguzi ufanyike hapo jana kwenye jimbo la igunga, tume imeshindwa kwani sababu zote zinazotolewa ni uzembe wa tume ya uchaguzi kutojipanga vizuri.

Sasa kama jimbo moja tu kutangaza matokeo inakuwa issue itakuwaje kwa uchaguzi mkuu? tume jipangeni bwana, igeni nchi nyingine zinafanya nini au zinatumia jitihada gani au maandalizi gani wanayafanya kutangaza matokeo mapema.

Tambueni kwamba tume ya uchaguzi inapochelewa kutangaza matokeo mapema wananchi wanakosa imani na tume. sometime vurugu zinazotokea kwa kuchelewa kutangaza matokeo zinasababishwa na ninyi wenyewe
.
Mkuu umenena vema,vurugu zote za uchaguzi husababishwa na tume,kumbuka arusha,ubungo,kawe kote huko vurugu zilisababishwa na tume,na ukiona ucheleweshwaji ujue kuna jambo
 
Mkuu yanasubiriwa matokeo rasmi tu kutangazwa lakini hadi sasa tayari CCM, ndiye mshindi maana ameongoza kata nyingi zaidi.
 
Duh Mungu tuepushie na hili balaa,vp anasema matokeo yatatangazwa saa ngapi?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom