Kwa nini tulibeza viboko vya DC kwa walimu wakati mambo hayaendi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa nini tulibeza viboko vya DC kwa walimu wakati mambo hayaendi?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by sulphadoxine, Oct 28, 2011.

 1. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #1
  Oct 28, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  MWAKA 2009, aliyekuwa Mkuu wa Wilaya Bukoba (DC), Albert Mnali, ‘aliweka rekodi ya taifa’ kwa kuwachapa viboko walimu waliochelewa kufika shuleni kwao, shule za msingi za Kanazi, Katerero na Kasenene huku akiwa amekasirishwa na shule zao kufanya vibaya katika mitihani ya darasa la saba.


  Kiongozi huyo alilaumiwa sana na wanajamii, hususan walioshindwa kutambua falsafa au maana ya viboko vya Mkuu huyo wa wilaya. Wengi kati ya waliotoa maoni yao juu ya kitendo kile walikiita cha udhalilishaji, kisichofuata haki za binadamu eti kisa ni walimu kuchapwa mbele ya wanafunzi wao.

  Bila ajizi, Rais aliamua kumtoa huko mkuu huyo wa wilaya na kumweka mbali na jamii ya watu wenye hasira ili yasije kumsibu yanayowakuta vibaka mitaani na kumsababishia madhara ama hata kumpotezea maisha kiongozi.

  Miaka miwili baadae (mwaka huu) katika mkoa wa Tabora wilayani Igunga wakati wa fukuto la kampeni za uchaguzi mdogo mkoani humo, wafuasi wa chama kimoja cha siasa wakiwa na wabunge wa chama hicho walimkuta kiongozi mwingine wa wilaya akiwa anafanya mkutano na viongozi wa kijiji kimojawapo wilayani humo, wakamfanyia vitendo vya vurugu mithili ya vile alivyoepushwa navyo Mnali. Huyu hakuwa mwingine bali mwanamama Fatma Kimario.

  Hebu tuangalie tafsiri juu ya viboko vya Albert Mnali dhidi ya walimu ambao aliamini wameshindwa kutimiza wajibu wao pamoja na nia hasa ya kuweka uwiano wa kiutendaji unaozingatia falsafa ya viboko.

  Baada ya baadhi ya watu kusikia habari za viboko vya Mnali dhidi ya walimu wale, walijua kwamba gwaride la kufundisha litachezwa vizuri kwa walimu husika kufundisha ipasavyo na kuwahi kazini kwa wakati.

  Lakini kilichosikika katika jamii baadae kilikuwa kinyume na matarajio ya wengi ingawa baadhi ya walimu walishituka na kuanza kuacha kutegea kazi ikiwa ni pamoja na kuwahi kazini kwa hofu ya kukutwa na viboko kama vya Mnali wakiwa nje ya kazi ama hawajafika.

  Wengi walitarajia kuona viongozi wakuu wa serikali wakiishia kuwapa pole tu wale walimu, pole ya kiungwana pamoja na kuwahimiza kuwahi kazini na kuacha kutegea ama kufanya uzembe wanapokuwa wanatekeleza majukumu yao. Na hakuna ubishi kwamba kushindwa kufaulu kwa shule hizo kulisababishwa na walimu kuchelewa kazini pamoja na kutofundisha ipasavyo, hivyo kwa mnali aliona hakuna sababu kuwakata mishahara ama kuwabembeleza, bali adhabu kama ambayo wao pia huitoa kwa wananfunzi wanaoshindwa kutekeleza majukumu yao wanayowapa.

  Lakini ikumbukwe pia wakati wa ujenzi wa Reli ya Kati na kazi zingine za maendeleo ya jamii zilizokuwa zikifanywa chini ya usimamizi wa serikali ya Mjerumani, viboko vilitumika ili kufanya ‘mambo yaende’. Nadhani sote tunaijua falsafa iliyo katika methali ya Punda haendi bila kiboko.

  Pamoja na ukweli huo, watu wengi, hususan wanaharakati walikimbilia kujificha kwenye utetezi wa haki za binadamu katika kuwatetea walimu wale na kusahau haki hizo hizo zinazowatetea wanafunzi. Wanafunzi wale walikuwa na haki ya kufundishwa ipasavyo. Katika kuamini kuwa walimu wetu wamedhalilishwa wengi wao walikata tamaa ya kufundisha katika shule hizo tena kwa kisingizio kwamba wanaona aibu na kujisikia wanyonge wanapokutana na wanafunzi wao, hasa walioshuhudia wakichapwa.

  Mjerumani alitumia bakora katika utawala wake ili kukabiliana na wabishi wasiotaka kufanya kazi, wategeaji wa kazi wasiokosa sababu wanapokuwa na udhuru hata kama walilala tu. Mjerumani alijua kuwa wakati mwingine Watanganyika ni watu wa udhuru ni waoga wa kazi na ndio maana alitumia kiboko na mambo yakaenda. Sasa hivi wanaofaidi matunda ya viboko vya Mjerumani kwa matumizi ya Reli ya Kati si Wajerumani bali Watanzania hata kama awali Wajerumani waliifaidi pia reli hiyo.

  Kwa mtazamo wangu, mambo mengi hayaendi nchi hii kwa sababu ya uzembe na utegaji wa Watanzania katika kazi. Walimu wengi hawafundishi, wauguzi mahospitalini, makarani katika ofisi za umma na kadhalika.

  Mimi ninadhani kama sheria za kazi na makaripio ya viongozi yanapokuwa yameshindwa kufanya kazi, pengine suluhisho sasa linakuwa ni viboko. Viboko, hata Mwalimu Nyerere aliposema alikuwa havipendi japo walivipitisha ili kuwaadhibu wala rushwa, vinaweza kuwa dawa ya uwajibikaji, si kwa walimu pekee bali hata kwa watumishi wa wizara na sekta nyingine za serikali na taasisi zinazotoa huduma kwa jamii katika nyanja tofauti na vitengo mbalimbali.  Mnali kwa wengi alionekana mtu katili, asiyezingatia maadili ya kazi lakini kwangu ni shujaa kwa sababu alikuwa na nia njema. Mimi ninaamini alipaswa kupewa uongozi wa juu zaidi katika Wizara ya Elimu (ama hata nyingine) kwa sababu tayari alikuwa keshaweka mazingira ya nidhamu na uwajibikaji makini kwa walimu. Mnali kwa kweli alitakiwa kuzinyoosha kada mbalimbali za utumishi wa umma kama vile wauguzi, waganga na madaktari wanaolala hasa nyakati za usiku zinapotokea dharula za kuwajibika.

  Ni juhudi kama za Mnali (hata kama si kwa njia ya kutembeza fimbo) zinazotakiwa pia katika kukabiliana na tatizo la ufaulu mdogo wa wanafunzi, hususan kidato cha nne na darasa la saba.
   
 2. dedam

  dedam JF-Expert Member

  #2
  Oct 28, 2011
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 846
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Huyo dc angekuta wewe upo na wanao, mkeo na mamamkwe wako akakuamuru ulale kifudifudi akulambe viboko ungetii amri yake
   
 3. Obuntu

  Obuntu JF-Expert Member

  #3
  Oct 28, 2011
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 512
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Haya bana:

  INNOVATION IS LIFE
   
 4. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #4
  Oct 28, 2011
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Mkuu hujaongea kitu kimoja, nacho ni sababu zipi zinazowafanya watanzania wasifanye kazi kwa bidii? Je ni kwa sababu hakuna viboko? Je ni kwa sababu hatuna role - model ya viongozi wenye kutoa mifano? Je ni kwa sababu watu wanajua viongozi wao wanatenda sivyo hivyo watu wengi wanavunjuwa moyo wa kufanya kazi kutokana na matendo ya viongozi wao? Je ni utamaduni wa mtanzania kutofanya kazi kabisa? Je ni kwa sababu tunaoneana aibu kila wakati?

  Naimani suala la viongozi kutosimamia wajibu wao, ndo linalotufanya watanzania wengi tuwe na nguvu kidogo ya kufanya kazi!! Pili hao hao viongozi wanapotafuna fedha au wanapokutwa na mikashfa kibao, inatufanya tuamini vingine kabisa na maadili ya kazi zetu.
   
 5. SILENT ACtOR

  SILENT ACtOR JF-Expert Member

  #5
  Oct 28, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 618
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  Sababu za matokeo mabaya siyo walimu tu. Pata muda usome tafiti au hata magazeti yameongelea sana hili. Wewe unaongelea upande mmoja tu wa walimu sawa na mfugaji anayetaka ng'ombe wake ampe maziwa wakati hampi chakula cha kutosha. Otherwise unaonesha tu jinsi ulivyozoea kuchapwa viboko na wazazi wako bila kupata nafasi ya kujitetea. Haisaidii sana, tuliangalie suala hili kwa mtazamo mpana zaidi.
   
Loading...