Kwa nini thamani ya shilingi ya Tanzania inaendelea kushuka?

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,072
1,250
WIKI iliyopita mchumi alifafanua vigezo vinavyotafsiri ukuaji wa uchumi, ukuaji wa pato la taifa la Tanzania kwa kipindi cha miaka mitano (2004 – 2008) na ukuaji wa pato la mtu mmoja mmoja.
Pia alielezea madhara ya upimaji wa uchumi kwa njia inayofuatwa na uwiano wa ukuaji wa uchumi na ukuaji wa uchumi kwa mtu mmoja mmoja.

Leo anaeleza sababu za thamani ya sarafu yetu kuendelea kushuka.

Thamani ya shilingi ya Tanzania inaendelea kushuka kila mwaka huku kukiwa na mabadiliko ya muda mfupi yanayoonesha kupanda kwa thamani, ingawa mwelekeo wa jumla umebaki katika kushuka ikilinganishwa na dola ya Marekani.

Mchanganuo huu unaonekana hapa chini kuanzia mwaka 2005 mpaka leo.

Wakati Rais Jakaya Kikwete alipotawazwa kwa mara ya kwanza kuwa rais, thamani ya dola moja ya Marekani ilikuwa sawa na sh 1,042.33 za Tanzania.

Mwaka uliofuatia (2006) shilingi ilizidi kushuka na kuwa 1,162 kwa dola moja ya Marekani; mwaka 2007 dola moja ya Marekani ilinunuliwa kwa sh 1,260.

Hata hivyo mwaka 2008 thamani ya shilingi ilipanda kidogo kwani zilitumika sh 1,150.5 kununulia dola moja ya Marekani lakini mwaka uliofuatia, 2009 ilishuka mpaka 1,310 ili kununua dola moja ya Marekani na mwaka 2010 ilifikia sh 1,335 kwa dola moja.

Yafaa kukumbukwa kuwa mwaka 1993 thamani ya shilingi ya Tanzania kwa dola moja ya Marekani ilikuwa 437/-; mwaka 1994 ikawa 476/-; mwaka 1995 ikapanda mpaka 524/- na mwaka uliofuatia, 1996, ikapanda mpaka sh 544.5 kwa dola moja.

Mwaka 1997 thamani ya shilingi ikazidi kushuka kwani dola moja ya Marekani ilinunuliwa kwa shilingi 593; mwaka 1998 shilingi ikashuka zaidi na kuwa 618.6 kwa dola; mwaka 1999 shilingi ikazidi kuporomoka na kuwa 699.55 na mwaka 2000 ikazidi kudorora kwani ilikuwa sh 791.5 kwa dola moja.

Hali ya kushuka thamani ya sarafu ya Tanzania ilizidi kuwa mbaya kunako mwaka 2001 kwani dola moja ya Marekani ilinunuliwa kwa sh 800 na mwaka 2002 ilishuka mpaka sh 912 dhidi ya dola moja ya Marekani.

Mwaka 2003 shilingi ilizidi kushuka thamani kwani dola moja ya Marekani ilinunuliwa kwa sh 973 na mwaka 2004 ikatoka kwenye mamia na kuingia kwenye maelfu. Dola moja iliuzwa kwa sh 1,052.17 na inaendelea kushuka.

Kadoka mtiririko huo ni vipi mkulima wa jembe la mkono, machinga anayetembeza mitumba mchana kutwa, kibarua na mtu asiyekuwa na ajira atashawishika kukubali kuwa uchumi unakua?

Kushuka kwa thamani ya sarafu, kiuchumi inamaanisha uzalishaji mdogo, hasa ule unaotoa fursa ya kuuza bidhaa nje kwa minajili ya kupata fedha za kigeni.

Kukosekana kwa uzalishaji wa kutosha unaoliingizia taifa fedha za kigeni zinazotosheleza mahitaji ya kiuchumi, husababisha thamani ya shilingi yetu kushuka.

Kitaaluma, ni kwamba sarafu yetu haihitajiki tu kwa ajili ya kuwa nayo, bali watu huihitaji sarafu ya nchi husika kwa sababu wanahitaji kununua bidhaa zinazouzwa na nchi hiyo.

Madhali sasa nchi haina kiasi kikubwa cha bidhaa zinazouzwa nje ya mipaka yake, basi ni vigumu sarafu yake kuhitajika katika masoko ya fedha na hii husababisha kushuka kwa thamani ya sarafu.

Hii ina maana pia kwamba kama nchi haiuzi sana bidhaa zake nje, basi huenda soko la ndani ni kubwa sana kiasi cha kutokuwa na ziada ya kuuza nje na kwa hiyo nchi huagiza bidhaa nyingi za nje ili kukidhi mahitaji ya ndani.

Uagizaji mkubwa wa bidhaa za nje husababisha nchi kuhitaji zaidi sarafu ya nchi ya kigeni ili kuagiza bidhaa. Hali hii husababisha msukomo mwingi wa sarafu ya nchi kwenye soko la fedha ambayo husababisha kushuka thamani ya sarafu yetu.

Ulinganishaji wa uagizaji na uuzaji wa bidhaa nje ya nchi

Mwaka hadi mwaka kumekuwa na ongezeko la uagizaji wa bidhaa za nje huku kukiwa na ongezeko dogo sana la bidhaa tunazouza nchi za nje.

Kadhalika, kila mwaka mpanuko kati ya sekta ya kuuza nje na sekta ya kununua nje huzidi kuwa mkubwa hasa kwa kusababishwa na ongezeko kubwa la mahitaji ya bidhaa kutoka nje ya nchi.

Hali huchangia kushuka kwa thamani ya shilingi ya Tanzania dhidi ya dola ya Marekani.

Kwa mujibu wa mchumi, ukilinganisha ukuaji wa sekta ya kuuza nje kama sehemu ya pato la taifa, imedhihirika kuwa sekta hii kiuwiano imeendelea kubaki palepale bila kukua huku sekta ya kununua nje ikiendelea kuchukua sehemu kubwa ya pato la taifa.

Hali hii si hatarishi kwa uchumi wa taifa tu, bali imeendelea kuzorotesha thamani ya sarafu ya Tanzania.

Ili kuwa na sarafu imara, lazima uwepo uzalishaji mkubwa wa ndani utakaosababisha ukuaji wa haraka wa sekta ya kuuza nje.

Si hivyo tu bali inabidi kuzalisha bidhaa nyingi zitakazouzwa kwa thamani zaidi na si kuuza bidhaa ghafi.

Aidha, changamoto iliyopo ni kuzalisha bidhaa za viwanda vyenye ubora utakaohimili ushindani wa soko huria.

Mfumuko wa Bei

Mfumuko wa bei nchini Tanzania kwa kipindi cha miaka mitano 2005-2010; umeendelea kuwa katika viwango visivyoridhisha ingawa si vibaya sana ikilinganishwa na nchi nyingi za Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Hali haikuridhisha sana msimu wa mwaka 2008/9 ambapo mfumuko ulikuwa kwa zaidi ya asilimia kumi ikichangiwa mno na mtikisiko wa uchumi duniani (global economic meltdown) na kupanda sana kwa bei za bidhaa za mafuta duniani.

Athari hii haikuishia kwenye mfumuko wa bei tu, bali bali iliathiri kwa kiasi kikubwa thamani ya sarafu ya Tanzania ikizingatiwa kuwa nchi yetu inaagiza zaidi bidhaa kuliko inavyouza n-nje ya nchi.

Vita dhidi ya umasikini inakuwa ngumu sana unapokuwapo mfumuko wa bei na hukwamisha juhudi zote za kuinua pato la mwananchi wa hali ya chini.

Safari ya kuinua pato la Mtanzania lina changamoto nyingi na husababishwa na suala la sera, usimamizi wa rasilimali na hasa utashi wa kisiasa unaweza kuleta mabadiliko stahili na endelevu.
 

markach

Senior Member
Oct 18, 2010
121
195
Ili pesa iwe na Thamani, Ni lazima tuimarishe viwanda vyetu ili viweze kuzalisha bidhaa bora ambazo tunaweza kuuza nje ya nchi khali kadhalikka tuimarishe secta ya kilimo pia
 

roby m

Member
Nov 21, 2010
28
20
Nchi yoyote yenye mendeleo ya uchumi siku zote huwa inakua na uwiano mzuri baina ya sekta ya viwanda na Kilimo!!!! Lakini hii ni tofauti sana kwa nchi yetu ya Tanzania, kwani Kilimo imekua ni sekta isiyo na uhusiano wowote na ukuaji wa viwanda kwani mazao huzalishwa bila kuwa na sehemu ya kupeleka!! katika hilo thamani ya sarafu yetu itaendelea kushuka kila siku.

"PLIZ VIONGOZI TUSIINGIZE SIASA KWENYE UCHUMI "
 

Mallaba

JF-Expert Member
Jan 30, 2008
2,555
1,170
nakubaliana na wewe,bila viwanda ni kazi bure pesa yetu itashuka kila siku
Ili pesa iwe na Thamani, Ni lazima tuimarishe viwanda vyetu ili viweze kuzalisha bidhaa bora ambazo tunaweza kuuza nje ya nchi khali kadhalikka tuimarishe secta ya kilimo pia
 

Bongolander

JF-Expert Member
Jul 10, 2007
5,068
2,000
uchumi wetu ovyo, pure and simple. Watanzania wengi hawajui hilo lakini wengi waliopo hapa JF mnajua.
 

Keykey

JF-Expert Member
Dec 1, 2006
3,252
2,000
Ili pesa iwe na Thamani, Ni lazima tuimarishe viwanda vyetu ili viweze kuzalisha bidhaa bora ambazo tunaweza kuuza nje ya nchi khali kadhalikka tuimarishe secta ya kilimo pia

Trade balance inakula kwetu; maana yake tunaagiza zaidi kutoka nje kuliko tunavyouza nje. Hebu fikiria, ni vitu gani tunavyouza nje ili tupase pesa ya kigeni ambayo tunatumia kuagizia mf. petroli?

Katika hali kama hii, pesa ya nje inahitajika zaidi kuliko ya ndani na kwa kanuni ya supply & demand, itabidi utoe pesa nyingi ya ndani ili upate hizo dola.

Kama viwanda vyetu vingekuwa vinazalisha, hii hali ingesaidia sana uchumi wetukwani gharama za uzalishaji zengekuwa chini na kule sokoni bidhaa zetu zingeuza zaidi.
 

Newvision

JF-Expert Member
Nov 9, 2010
446
0
Asante wachumi kwa kutuelemisha lakini mwaongea wakati Wenyewe wenye maelekezo wamekaa magogoni etc hawana shida na haya eti hawayaoni.
 

Njowepo

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
9,536
2,000
Sasa kama kila mnacholima mnakipeleka nje tena mbaya zaidi kikiwa raw alafu wenzenu wakikiprocess mwaenda nunua kwa USD.
URAFIKI huwa wana import nyuzi toka CHINA wakati pamba iko tele kule Mwanza.
In such a situation what do u expect
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom