Kwa nini TCU guide book ya mwaka huu hawajaonesha kozi zenye vipaumbele vya mkopo?

Nipe Andiko

Senior Member
Jan 20, 2017
150
250
Zamani TCU guide book ilikuwa inabainisha kozi ambazo ukizichagua kuna uwezekano wa kupewa mkopo, lakini cha ajabu mwaka huu 2017/2018, Tcu wametoa guide book, ambayo haionyeshi Kozi ambazo ni PRIORITY na ambazo ni NON PRIORITY, na hakuna hata possible loan amount!

Na wengine bila mkopo kusoma chuo kikuu ni vigumu, sasa tutajuaje kozi zenye mkopo ili tuzichague na zisizo na mkopo ili tuziepuke au kama tutazichagua, basi tujipange kabisa mapema, sio vizuri kukaa kimya bila kutuambia kozi za vipaumbele na zisizo na vipaumbele vya mkopo, mwisho wa siku watu tunachagua kozi mbalimbali alafu baadae mnatunyima mkopo kwa kisingizio eti kozi tulizochagua hazikuwa PRIORITY, afadhali muwe mnatoa taarifa mapema, kabla hatujaanza kuapply!

Ni hayo tu wadau!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom