Kwa nini TCRC wasiruhusu redio kutumia lugha asilia! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa nini TCRC wasiruhusu redio kutumia lugha asilia!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by theophilius, Aug 27, 2011.

 1. theophilius

  theophilius Senior Member

  #1
  Aug 27, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 151
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Nimekuwa karagwe kwa wiki kadhaa sasa, nimeshuhudia mengi. mojawapo ni maendeleo ya kasi ambapo hivi sasa kuna redio mbili za FM, Karagwe Fm na FADECO FM. kwa hakika zinafanya kazi nzuri maana hapo kabla wakazi wa wilaya hii inayo pakana na nchi mbili za Rwanda na uganda ilikuwa vigumu kwao kupata redio za tanzania ikiwemo Redio ya taifa.licha ya matatizo ya kukosa waandishi wa kutosha mahili wa taaluma ya uhandishi na utangazaji,

  cha ajabu hata hivyo ni kwa wageni wanaoishi wilaya hii ambao si wenyeji yaani wanyambo, kwani kuna wakati watangazaji na sources wao wanaongea ki'nyambo kwa dakika kama 30 hivi, bila hata kutafsiri kinachozungumzwa, pengine kwa sababu wanaohojiwa hawawezi kujieleza vizuri kwa kiswahili au lugha nyingine isipokuwa kinyanbo, na hivyo watangazaji kuamua kutwanga kinyambo ili kuwachimba zaidi sources wao na mambo ni burudani kabisa, kwani nadhani kama si wote basi wengi wa watangazanji nao ni wanyambo (kabila wenyeji wa karagwe).

  hata hivyo kama kumbukumbu yangu inafanya kazi vizuri, kuna sheria inazuia kutumika kwa lugha asili (siyo kilugha) kama kinyambo, licha ya kuwa baadhi ya lugha kama hizi zinatoweka ama kwa kumezwa na lugha zingine au lugha kubwa zilizozizunguka. na kwa mujibu wa kumbukumbu hiyo, ilisikika miaka kadhaa iliyopita redio moja nusura inyimwe usajiri kwa kuwa ilionesha nia ya kutangaza/kukuza lugha ya asili, huko Maswa

  hata hivyo kama nilivyodokeza awali kwa tanzania hii ambayo wasiojua kusoma na kuandika inaongezeka, kwa wanaotoka vijijini wanajua maana yake, kwamba kutojua kusoma na kuandika ni sawa na kutojua kiswahili vizuri maana kishwahili vijijini hufundishwa mashuleni hadi watoto hupewa adhabu, kwa nini tusiangalie upya sheria hii?

  ndiyo maana nikajiuliza kwa nini tusifike mahali ikaruhusiwa rasmi, ili hata bibi na babu walioko huko, rwanyango, chamchuzi na ihembe ambao hawawezi kujieleza vizuri au kusikiliza na kutambua vizuri lugha zingine ikiwemo kiswahili, wapate haki yao ya msingi na kikatiba ya kupasha na kupata habari! tunamuhitaji mtu kama mchungaji mtikila afungue kesi mahakama kuu ndiyo sheria kama hii ifutwe au vipi!

  naomba tujiulize pamoja na tujadili
   
 2. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #2
  Aug 27, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  NYERERE alishafuta ukabila na tukaunganishwa taifa moja lugha moja.jiulize huo mkoa wanakaa tu wanyambo<+ je wageni nao waelewee nini sasa? arusha ipo radio moja ya kimasai lkn wanatangaza kwa kiswahili vipindi vyake vingi ni vya kimasai. sikuungi mkono radio au tv zitangaze kilugha yasije yakatokea ya kenya.
   
 3. Bornvilla

  Bornvilla JF-Expert Member

  #3
  Aug 27, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 925
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Kenya kuna Mirembe fm inatangaza Kiluya,nyingine sizikumbuki majina lakini zinatangaza Kijaluo na nyingine Kikikuyu. Mambo haya yameendelea kuleta hisia za ukabila mkubwa Kenya. Naomba TCRA wasije ruhusu utamaduni huu wa kutumia lugha za asili katika redio na tv,kwani sisi sote ni mashahidi kwa kile kilichotokea Kenya,Burundi na Rwanda na hata Congo. Jamani Watanzania wote kabila yetu ni moja nayo ni Waswahili pamoja na kuwa na asili zetu. Ukabila husababisha wengine kujiona wao ni watukufu na hii ni hatari sana.
   
 4. j

  juni Member

  #4
  Aug 27, 2011
  Joined: Apr 5, 2011
  Messages: 87
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  sasa tcra wako wapi? kama wengine wanapigwa mkwara mbona hiz za kinyambo na kmasai hazizuiwi! au ni mabonde kwinama kiasi kwamba mitambo yao haizinasi?
   
Loading...