Kwa nini tax consultants wateuliwe/kupewa leseni na TRA ili kuwatetea tax payer?

Silicon Valley

JF-Expert Member
Mar 6, 2012
1,092
1,116
KWA NINI TAX CONSULTANTS WATEULIWE/KUPEWA LESENI NA TRA ILI KUWATETEA TAX PAYER ?
Wakuu natumaini muko salama, naomba ushauri wenu kuhusu utaratibu huu ulivyokaa ,

Kumekuwepo na utaratibu ili Tax Consultant aweze kufanya kazi yake ya kuwashauri , kuwatetea, kuwaandalia mahesabu ya kodi wateja wake wafanya biashara au walipa kodi wote, ni lazima awaombe TRA ili ateuliwe rasmi au kuidhinishwa kama tax consultant kwa kupewa kibali/leseni ya kazi hiyo na pia kupewa masharti na taratibu zao,,,,

Kwangu mm naona utaratibu huu hautendi haki kabisa walipa kodi, kwani ni sawa kama unashitakiana na mpinzani wako mahakamani (wewe na mpizani wako = tax payer na TRA) then unamchukua advocate ili akutetee wewe halafu anaambiwa lazima apewe leseni/ ateuliwe na huyo mpinzani wako TRA,,, KWELI PANA HAKI HAPO ? ? NI LAZIMA TAX PAYER ATAUMIZWA TUU,,,, KWA MAANA HIYO CONSULTANT ATAKUWA NA MABWANA WAWILI, WA KULIPA UJIRA NA WA KUMPA LESENI ambaye ndie atakaye msikiliza zaidi…

Ushauri wangu hao tax consultants walipaswa kupewa leseni au kuteuliwa na bodi tafauti kabisa TRA kama vile NBAA, n.k
 
Mtazamo tu, lakin TRA wanachokifanya ni kutoa kibali kwa mtu mwenye sifa ili awasaidie walipa kodi. TRA haipo kukukomoa, ipo kukusanya kodi kwa mujibu wa sheria. Tax Consultant kazi yake si kukutetea wewe usilipe kodi, kazi yake ni kukushauri ulipe kodi sahihi kwa mujibu wa sheria.
 
Back
Top Bottom