Kwa nini Tanzania tunatakiwa kuwa na visa kuingia baadhi ya nchi za SADC?

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,143
18,774
Kuna wakati siwaelewi kabisa wanasiasa. Kwa hivi wanasiasa wanaongelea kwamba na kupiga porojo nyingi sana juu ya SADC regional integration, lakini unakuta mambo ya msingi kabisa kama uhuru wa kutembeleana bado hawajakamilisha. Sasa unawezaje kuwa na akili ya kuongelea kumwingiza mwanao mashindano ya mbio wakati bado anatambaa hata kutembea hajaanza?

Ni kwa nini hadi leo Tanzania tunatakiwa kuwa na visa kwenda baadhi ya nchi za SADC? Hakuna policy ya SADC inayosema nchi wanachama wa SADC hazitakuwa na visa katika wananchi wake kutemebeleana? Na kwa nini nchi kama Zambia na Swaziland wanatoa siku 30 tu badala ya 90 kama nchi nyingine za SADC? Ningependa kupata majimbu toka Mambo ya Nje au yeyote anayefahamu juu ya hili.

Hadi sasa, suala la visa kwa Watanzania kwa nchi za SADC liko kama ifuatavyo;
upload_2017-7-3_11-50-14.png
 
Kuna wakati siwaelewi kabisa wanasiasa.,,,
Suala la Visa ni makubaliano baina ya nchi mbili. Swali la muhimu kujiuza ni je nchi hizo ambazo zinahitaji Visa, wao kuingia kwetu wanahitaji. Kuwa SADC hakumaanishi kuna free VISA kila mahali ni utaratibu baadhi ya nchi zimejiwekea na zingine zina reciprocate nao kwa kutoa free VISA. Na nchi nyingi za SADC zimeamua kumeana free VISA zenyewe kwa zenyewe. Na pia kwenye baadhi ya nchi, ada za elimu kwa wanafunzi local zina apply pia kwa wanafunzi wanaotoka nchi za SADC. Kwa hiyo ukisema kuna faida gani ya SADC, basi huna tu taarifa. Zipo nyingi tu. Moja ni kwa upande wa elimu tunapewa discounts katiba baadhi ya nchi za SADC
 
Nakuelewa Mkuu, ila kwa suala la visa nchi za SADC, nadhani tulishatoka kuwa visa ni makubaliano ya nchi mbili. Limekuwa ni suala la integration. Kuna zaidi ya visa - hata mfumo wa leseni za magari tuliamua kufanya ufanane. Nadhani hata registration number za magari walishasema sifanane. Na pia hata suala la kuingia na gari nchi ya SADC likarahisishwa. Swali langu ni kwamba kwa nini hizo nchi kwenye red bado tunasua sua wakati policy ya SADC kiujumla ni kuondokana na vitu hivi?
 
Sijajua sababu. Labda wanajaribu kuwa protective.
 
Hii ni mojawapo ya thread fikirishi...heko mleta maada! tukianzia na issue ya kuwa na visa or kutokuwa nayo kwa nchi za ukanda wa SADC inatokana na utashi wa kisiasa wa nchi mwanachama, pamoja na mahusiano dhidi ya nchi na nchi. ndo maana umeona nchi kama Msumbiji haikuhitaji kuwa na viza, endapo ukiwa M-Tanzania...hii inatokana na historia ya hizi nchi mbili! kwa upande mwingine, kila nchi inataka ione watu wake na mipaka yake ikiwa salama...kwa maana nyingine ku-implement mkataba wa SADC kwa asilimia 100% kunahatarisha usalama katika nyanja zote...(watu na rasilimali zake).

Pamoja na yote, kuna faida nyingi za kuwa mwanachama wa SADC ikiwa ni pamoja na biashara, uwekezaji na fursa za kupata Elimu. kwa mfano, ibara ya 4 ya SADC PROTOCOL ON EDUCATION AND TRAINING inasisitiza ushirikiano katika fursa na elimu. kwa upande mwingine SADC protocol on trade nayo inasisitiza uhuru kwa kufanya biashara bila vikwazo ikiwa ni pamoja na kutembeleana kwa lengo la kujifunza na kutafuta fursa. hali-kadhalika, kuna mkataba wa ulinzi ambao unaitwa protocol on security, defence and political cooperation...kwa Lengo la kudumisha amani na usalama kwa nchi mshirika na mwanachama...
ikumbukwe kuwa mikataba yote hiyo inabidi iwe incorporated kwenye sheria za ndani kwa kila nchi mwanachama ili kuleta tija. kinachotokea, wana-sign protocol hizo na kisha wanategeana nani aanze kutekeleza kilichomo...
take note: kwa upande wa Elimu, utekelezaji wa mikataba(protocols) umefanikiwa kwa kiasi kikubwa...though watanzania huwa hatuko aggresive kutafuta elimu nje ya tz! though changamoto inabaki kwenye upande wa kisiasa etc......
 
Back
Top Bottom