Kwa nini Tanganyika hawadai Nchi yao walio ipigania uhuru? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa nini Tanganyika hawadai Nchi yao walio ipigania uhuru?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by abdulahsaf, Feb 4, 2011.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Feb 4, 2011
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0  Na. B.OLE,
  Nashindwa kuelewa sababu halisi inayowafanya majirani zetu wa Tanganyika kutodai nchi yao na kukaa kimya huku wakiwaona Wazanzibar kama vile watoto wa kambu. Mara nyingi vilio vinavyosikika kwa kwikwi ni kutoka Visiwani jambo ambalo linanifanya nione kama vile kuna utata fulani katika suala zima la Muungano wa Nchi hizi mbili. Hata hivyo napata kigugumizi na ukiwa hasa pale ninapoangalia historia na kuona kwamba Zanzibar lilikuwa ni Taifa huru, lenye himaya na mamlaka yake tokea enzi na jadi.
  Lakini kama yote hayo hayatoshi, kubwa zaidi ni kwamba katika Bara la Afrika sioni Nchi ambazo zimeungana au zenye Muungano wa aina hii tulionao hapa Tanzania, inawezekana ikawa labda Wazanzibar na Watanganyika wamepiga hatua kubwa katika hili lakini pia inawezekana kama pengine ni kuzidiwa nguvu na maarifa kwa Nchi moja kati ya hizi zinazoambiwa kama zimeungana na muungano wao ni wa damu, ambao unazidi kuimarika siku hadi siku .
  Wasi wasi unakuja kwamba mbona hakuna uwiano sawa katika shughuli zote za serikali, lakini pia kwa nini upande mmoja tu ndio uwe unalalamika na mwengine umekaa kimya kama vile vilio vya ndugu zao hawavisikii ? Bila shaka kwa mawazo yangu mapotofu hapa ipo namna fulani, ambayo kama haitofichuliwa basi itaipelekea udugu uliopo kuwa mgumu hapo baadae. Kinachojitokeza katika sakata hili ni kwamba Tanganyika wameonja keki na minofu ya ndafu kwa maana hiyo kurudia tena viporo vya ugali wa jana na mlenda, hili kwao itakuwa ni vugumu na haliwezekani na iwe itakavyokuwa lakini kamwe hawatasikiliza vilio vya Wazanzibar.
  Majirani zetu ni kwamba wanachukua nafasi hii adhimu ya ulibwende, udhaifu na ubwanyenye walio nao Wazanzibar kutekeleza yale waliokusudia huku wakijua fika kwamba kelele za mlango hazimfanyi mwenye Nyumba yake kulala usingizi mnono. Ni kweli kwamba Wazanzibar wamechoshwa na Muungano huu uliopo lakini jee tujiulize kuna hatua gani ambazo Wazanzibar wamechukua ili kuonesha Dunia kama kweli hii hali tulionao imetuchosha na hatuko tayari kuendelea nayo ? Madhila wanayopata Wazanzibar yatamalizika lini na yatasikilizwa na nani katika ulimwengu huu tulionao ambao wahusika wanajitapa ya kuwa ni ulimwengu wa kidemokrasia!
  Zanzibar tokea enzi za Wakoloni imekuwa iko mashakani lakini Wazanzibar wanashindwa kujiuliza suali dogo tu la msingi, kwa nini iwe ni sisi tu Wazanzibar tunaoishi katika hali hii ? Mbona wengine kama sisi ambao wako katika Bara hili hili la Afrika, Visiwa kama vyetu, na mazingira yanayo shabihiana na kwetu hawamo katika kadhia kama yetu ?. Hapa naona ipo namna fulani, na ikiwa kweli Wazanzibar tunavilio vya kweli na sio vya mamba, basi hatuna budi kutafuta njia nyengine mbadala ili kuiondosha hali hii, tukumbuke kwamba balaa siku zote haiwezi kuondoka mpaka ije balaa nyengine. Mapinduzi yaliofanyika Zanzibar yalikuwa ni janga kubwa kwa Wazanzibar, tulitegemea yakwamba kwa yale yaliotokea huko nyumba tutapa shufaa kwa njia moja ama nyengine lakini matokeo yake yamekuwa ni kuzidi kwa nakama na beluwa. Jee tunahitaji Mapinduzi mengine badala ya yale yanayoitwa matukufu ? Hivi kwa nini Watanganyika wahisi kwamba Zanzibar ni mali yao na huku Wazanzibar wenyewe washikilie kwamba tumeungana tu, mbona hizi kauli zinapingana Wazalendo pana siri gani hapa.
   

  Attached Files:

 2. L

  LAT JF-Expert Member

  #2
  Feb 4, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  mimi sielewi unazungumzia kitu gani l....... tafuta diclopar na maumivu yako yataisha ..... JF itakuongezea maumivu
   
 3. T

  Tata JF-Expert Member

  #3
  Feb 4, 2011
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,732
  Likes Received: 651
  Trophy Points: 280
  Sioni uhusiano kati ya kichwa cha habari na makala yako. Kichwa cha habari kinauliza kwa nini watanganyika hawadai nchi yao wakati habari inahoji kwa nini wazanzibari wanaendelea kuwa kwenye muungano wakati, kwa maoni yako, hawautaki. Sasa suala hapa ni nini hasa?
   
 4. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #4
  Feb 5, 2011
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Tanganyika ipo sema imekuwa kubwa zaidi kwani Zanzibar imekuwa nchi moja na Tanganyika na inaitwa Tanzania. Tatizo ni nini? Kama haupendi muungano basi watoeni wabunge wenu bara!
   
Loading...