Kwa nini subira ni lazima katika mafanikio na mahusiano...? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa nini subira ni lazima katika mafanikio na mahusiano...?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Sep 25, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Sep 25, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Hata katika kuelekea kujenga uhusiano imara kunahitaji subira.....


  Ralph Waldo Emerson, mkongwe wa ufahamu, aliwahi kusema. Fuata mwenendo wa maumbile, siri yake ni subira. Subira hiyo yaweza kukufikisha kwenye maisha bora kama unajua jinsi ya kufanya kazi na Nguvu ya Subira na maumbile kwa pamoja.

  Kwa nini subira ni ya lazima kwa mafanikio?

  Muulize mfanyabiashara yoyote aliyefanikiwa ama yeyote aliyefanikiwa bila ujanjaujanja, atakwambia kwamba, hakufikia uamuzi mara moja. Huchukua muda mrefu wa utafiti, kufuatilia na kufikiria, wakisubiri hadi muda muafaka kufanya uamuzi. Maumbile hufanya kazi kupitia mchakato maalum na yana uwezo mkubwa wa kusubiri.

  Kwa mfano: Unataka kupanda mbegu, imwagilie maji, iache kwa muda, na utakapofikia muda muafaka, wakati kila kitu kiko sawa, mbegu hiyo itaanza kuota na baadaye mmea. Hii ni kwa mmea wowote utakaoupanda. Hii hutokea tu wakati hali inapokuwa sawa, lakini kulikuwa na kazi iliyokuwa ikiendelea kufanywa kabla ya matokeo yote haya kuchukua nafasi yake. Mbegu inatakiwa kupandwa, inatakiwa kutunzwa, inatakiwa kuachwa ili ianze kutoa mizizi michanga ardhini, na baadaye muda utakapofika mmea unaanza kujitokeza juu ya ardhi katika hali hasa iliyotarajiwa. Bila kuweko kazi ya mwanzo ya kupanda na kumwagia maji mbegu, mmea usingetokeza juu ya ardhi, na hungeweza kuwa na bustani yako ya matunda ama maua ambayo huenda hivi sasa unakula matunda yake.

  Kama unataka kufikia malengo yako, iko haja ya kuwa na subira ya aina hiyo. Hii haina maana kwamba ukae kitako na kusubiri kila kitu kiende kwa wakati wake. Badala yake unatakiwa kufanya kazi kwanza, kuweka msingi, kupanda mbegu, na kuhakikisha ardhi unayolima ni ya kufaa. Tayarisha na usubiri kwa kila hali kuwa sawa kabla ya kutoa maamuzi sahihi yatakayokusukuma kwenye mafanikio makubwa. Kwa bahati mbaya, watu wengi hawako tayari kufuata mchakato huu na badala yake wanataka kwa siku moja kupata kila kitu katika maisha yao. Siyo wazuri kufuata taratibu zinazokubalika za vitu kubadilika, na hivyo hujikuta wakitaka vitu vibadilike mara moja na hivyo kuishia wakichanganyikiwa na kukata tamaa kutokana na mabadiliko haya ya ghafla kushindikana.

  Moja kwa moja hiyo huwa haifanyi kazi. Wakati unapofanya kazi kinyume cha maumbile, unasukumwa nyuma zaidi. Ikiwa unataka kufanikiwa, unatakiwa kuwa na subira kwa kiasi fulani. Fikiria kile unachotaka ufanikisha, fikiria kuhusu mabadiliko unayoyataka, anza mchakato wa kuleta mabadiliko haya kwa kujua kile unachotaka na kwa nini. Pandikiza mbegu zako za mafanikio kwenye bustani ya akilini mwako. Kuwa na subira ukisubiri alama za nyakati za kukuruhusu kuendelea. Hakikisha mawazo yako ya kawaida na yale ya kina yanafanya kazi kwa pamoja ili kukusaidia kufikia malengo yako. Wakati unapokosa subira, wakati unaposhindwa kuamini na kukubali kwamba mambo yatakuwa, huwa unapunguzwa kasi yako, kukwamishwa na hatimaye kuishia kwenye njia isiyo sahihi na baadaye unashangaa:
  ‘Nimefika vipi hapa?'

  Kwa mfano, uko kwenye foleni ukisubiri kulipia kitu fulani, foleni ni ndefu, lakini kuna mtunza fedha mwingine ambaye naye ana foleni ndefu kama hiyo. Kama utachoka na kukasirika, haitakusaidia. Ikiwa utaamua kuhamia mstari mwingine, hiyo huenda ikakuchukua muda mrefu zaidi, kama utaacha na kuondoka, hutopata kile unachohitaji. Unaweza kuamua kuondoka ukipanga kurudi foleni itakapopungua, lakini baadaye ama ukashindwa kurudi ama unaporudi ukakuta foleni ni ndefu maradufu ya ile ya kwanza na hivyo kuamua kuachana kabisa na zoezi hilo ulilotaka kulifanya, na hivyo kukosa kile ulichotaka.

  Unapokosa subira unakasirika haraka, ukidhani mambo ni rahisi upande wa pili, lakini ukaondoka bila kupata kile unachotaka. Kama ungekuwa na subira, ungeweza kufanya malipo yako na kuendelea na kile ulichotaka. Usifikirie mambo ni mazuri upande wa pili, shughulika na kile ulichonacho na kile unachojua na hivyo kuwa na subira na utatoa maamuzi sahihi
  . Ukikimbilia Marekani kwa kudhani huko mafanikio yanakuja mara moja, utashangazwa. Utakaa huko kwa miaka kumi na ukirudi hapa nchini, utakuta uliyemwacha akiwa anafanya kile ulichoona hakilipi, akiwa mbali sana.

  Ni vigumu mtu kuanza na kufanikiwa kupata fedha nyingi katika kipindi kifupi kama cha miezi mitatu, kwa sababu lazima zitakuwepo taratibu zinazohitaji kufanyika kama ilivyo kwa wakati wa kupanda mbegu. Ikiwa utakuwa na subira na kungojea mchakato ufikie wakati wake, ni wazi utapata mamilioni ya fedha si kwa miezi mitatu tu, bali katika kipindi kirefu cha maisha yako, mpaka pale utakapokiuka mchakato wake. Unaweza kujaribu kufanya mambo ya haraka kwa kujaribu mradi na hivyo kuwekeza kwenye miradi ya hatari na pengine kuishia kuingia kwenye uchezaji wa kamari na bahati nasibu, lakini ni wazi utapoteza fedha nyingi zaidi. Hata unapoyatazama maisha ya binadamu, utakuta yanafanya kazi kwa kufuata utaratibu wa maumbile, utaratibu wa kusubiri.

  Tunaanza tukiwa watoto wadogo, tunakuwa, na kuwa watu wazima na umri unazidi kupanda hadi kuzeeka, kama ilivyo kwa utaratibu wa maumbile. Mtu hawezi kuzaliwa leo na kufikia umri wa utu uzima ili aweze kuwahi nafasi fulani ya kazi ambayo hivi sasa iko wazi. Mafanikio katika maisha huwa hayatokei kwa usiku mmoja. Kuanzisha biashara na kuifanya ifanikiwe kunahitaji subira. Kukosa subira katika biashara ni kualika janga. Uhusiano nao huchukua muda kuujenga na kuuboresha, kukosa subira katika uhusiano ni njia fupi ya kuhitimisha uhusiano huo. Kutafuta kazi sahihi kunahitaji subira na juhudi, kukosa subira katika kutafuta kazi ni njia rahisi ya kuikosa kazi hiyo. Mambo yanaweza kutokea ghafla, lakini mafanikio yanahitaji subira. Kwa mfano, waweza ukakutana na mwenza wako hata leo, lakini mafanikio ya uhusiano wenu huo yatahitaji subira ili yaweze kukua na kufanikiwa.

  Unaweza ukawa na wazo la biashara hata leo, lakini kwa biashara hiyo kuweza kukua hadi kufikia mafanikio kutategemea jinsi utakavyokuwa na subira si kwa kazi tu, bali pia kwa wafanyakazi wenzako na viongozi wako. Ili kuanza kujenga msingi wa mafanikio yako leo, anza kupanda mbegu hivi sasa ili uweze kupata mafanikio yako hapo baadaye.
   
 2. MKATA KIU

  MKATA KIU JF-Expert Member

  #2
  Sep 25, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,167
  Likes Received: 966
  Trophy Points: 280
  Kaka huu uzi si mchezo, kweli subira ni muhimu sana kwenye maisha mbegu inatakiwa kupandwa muda sahihi,, huwa napenda sana kuangalia sports tofauti, kwenye basketball kule america college players wanasema una declare your name for NBA draft wakati sahihi wakat umeifikisha your college kwenye final four, upo kwenye first team all america una awards za kutosha as player of the year zitazokusapoti kwenye draft,, ili uwe na uhakika wa kuwa drafted early na kupata guarantee contract.. Age is doesn't matter than planting your seed at the right time.... Sipendi kupelekeshwa sana kwa mafanikio ya watu wakati muda wangu bado, na hata kuhama hama kazi sana kutegemea mambo mzuri wakati muda sahihi bado mwisho wa siku unahamia kuwa subordinate kwingine wanakokupelekesha kuliko ulipotoka ni ujinga
   
 3. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #3
  Sep 25, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Mtambuzi, uzi wa leo mtamu, lakini kipi kikomo cha subira....
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. Paloma

  Paloma JF-Expert Member

  #4
  Sep 25, 2012
  Joined: Jan 22, 2008
  Messages: 5,341
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  ..........anyway!
  uzi mzuri Mtambuzi
  subira huvuta heri!
  nasubiri..........!!!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #5
  Sep 25, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  @MadameX ..... Nguvu ya subira ina uwezo wa ajabu na inaweza kukuletea mafanikio ambayo hata wewe hutoweza kuamini. Ni nguvu hii utakayoweza kuitumia ili kupata kazi unayoitaka, kukutana na watu sahihi na hata kufanya kazi kwa kutumia nguvu hii ili kuwekeza katika sehemu sahihi. Ikiwa utapanda mbegu na kukesha ukiisubiri iote, utakuwa kichaa, ikiwa utapanda mbegu na kuisahau ukidhani unaisubiria, itakufa na ikiwa utaipanda na kuiwekea jiwe juu yake, haitajitokeza nje ya ardhi. Lakini ikiwa utapanda mbegu na kufanya kazi ya kuimwagilia maji na kuitunza, itaota na kumea vizuri.

  Hivi ndivyo nguvu ya subira inavyofanya kazi. Fanya kazi zako vizuri kabisa, kuwa na subira na uelewa kwamba vitu vitakuja wakati utakapokuwa muafaka. Kama unatafuta kazi mpya, fanya kila uwezalo kupata kazi hiyo. Lakini uwe na subira ukijua wakati utafika, nawe utaipata. Kuna tofauti kati ya subira na kungoja. Kungoja si kusubiri. Kungoja ni kupoteza wakati. Kusubiri hakuna maana kuwa ni lazima ungojee.

  Unaposubiri unafanya kile kinachohitajika ili kuboresha maisha yako huku ukielewa kwamba mabadiliko yatatokea wakati muafaka. Unajitayarisha huku akiamini kwamba mabadiliko yatakuja. Lakini unapongoja, unakaa ukiwa na matumaini ya kuboreka kwa hali yako, bila kufaya jitihada za kutosha.

  Usikae chini na kungoja, ni wajinga tu wanaoweza kufanya hivyo.


   
 6. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #6
  Sep 25, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Hii nimeipenda Mtambuzi... Katika moja ya mitihani ya Mapenzi ni Subira... Subira ni dawa kubwa sana katika Mapenzi na kwa kiasi fulani inaweza hata kuku define mtu (tokana na subira yako ndani ya mapenzi).

  Hata hivo unapoambiwa subira haina maana tu kuwa lazima usubiri sana katika kila jambo lihusulo penzi lako... Subira huwa more in the lines ya kuelewa kila jambo fulani katika penzi lenu linahitaji subira ya kipimo kipi? Ukifaulu hapo then kwa kiasi kikubwa inajenga na kukuza hilo penzi lenu.

  Wataalam wa subira katika mahusiano na amabo wanashika hatamu ni sie akina mama... Sometimes hadi tunai misuse na hio subira kuharibu badala ya kujenga. Hii nazungumzia sababu ni wazi kuna baadhi ya mambo katika mahusiano kama mwanamke hujajua ni kiasi gani usubiri na nini ufanye basi hakitafanyika wala kuganikiwa. Mungu ni wa ajabu saana... Alifaulu kuumba mwili wa mwanamke na mwanaume tofauti kama alivofaulu kutengeneza mtazamo tofauti wa mwanamke na mwanaume katika Mapenzi....
   
 7. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #7
  Sep 25, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Ahsante Da AshaDii kwa maoni yako mazuri.

  Niliwahi kuandika humu wakati fulani kwamba, wanaume huchukua muda sana kufikia maamuzi pale linapokuja swala la kuchagua mwenza. Jambo hili huwatatiza sana wanawake kiasi kwmaba hufika mahali wakaoana kama wanapotezewa muda au wanalaghaiwa. kama mwanamke atatumia nguvu ya subira, anaweza kufaulu katika mtihani huo na kuvuka salama na kuishi katika ndoa aliyoikusudia. Kwa wanawake kumpata mwenza mwenye muafaka ni sawa na kucheza kamari, kwani wanaume sahihi mara nyingi hawaji na sura ya kuvutia, ni wanawake wachache wenye utambuzi wanaoweza kuling'amua hilo na kuvuta subira.

  Je utajuaje kwamba huyu ndiye?

  Ni rahisi sana, Ungana nami katika mfululizo wa makala zangu humu JF nitakuja na uzi utakaozungumzia jambo hilo.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #8
  Sep 25, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,945
  Likes Received: 1,818
  Trophy Points: 280
  Mtambuzi mzima lakin kaka? bado naendelea kusugua goti Mungu atajibu kwa wakati wake.

  Nirudi kwenye mada kwanza nimeipenda sana na ukweli imeongelea jambo la msingi sana katika mahusiano.

  Unajua hakuna kitu rahisi dunian, na wala hakunaga maisha ya kuanza na kukolea kama chumvi. huwaga napenda kusema kwa ninaowashauri mahusiano sio chumvi useme ukieka itakoza mara moja. mahusiano grows gradually na wakati yanakuwa hukutana na changamoto nyngi sana njian. hapo ndipo unapotaiwa kuwa na imani na uskate tamaaa.

  mara nyingi sana washindi wa tuzo hizi huwa akina mama ambao kwao uvumilivu, subira na imani hutumika kama nguzo ya kuimarisha mahusiano tofauti na wenzetu akina baba ambao kwao, heshima, ukuu na uwajibikaji hutumika kama nguzo kwenye mahusiano.

  daima wanawake wenye subira, uvumilivu na imani huweza kufanya familia zao kudumu milele ukilinganisha na wale ambao wana lack hizi skills. kama uliusoma uzi wa BADILI TABIA wa jana juu ya nini kinachowarudisha wanaume ukaona comment za Kongosho basi utanielewa vizuri sana katika hili.

  kwa nyongeza tu sometimes love follows the normal growth curve pattern. ambayo iko in exponential form ila tu inapo acclimatize basi tunategemea inaweza kuanza kudeteriorate na kurudi chini. kwa mwanamke mwenye hizi sifa hatakubali ipururuke atajitahd irudi kwenye peak tena kwa busara na hekima yake. na hii ni common life phenomena.
   
 9. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #9
  Sep 25, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Watu wawili wanaweza kuanza kufanya kazi kwenye kampuni moja, wote wakiwa wameanzia katika kiwango kimoja cha cheo kazini na wote wakiwa na matumaini ya kupata mafanikio makubwa hapo baadaye.

  Mmoja siku zote anakuwa na subira, akiwa ni aina ya watu wavumilivu. Mwingine anaonekana kuwa na haraka, kila wakati akitaka kupata vitu kwa haraka, akionesha wazi kutokuwa na subira na kila wakati akitaka apate zaidi kwa haraka. Baada ya mwaka mmoja tu, huyu wa pili akawa tayari anataka kupanda cheo na hivyo akaanza kutaka mshahara mkubwa na kupandishwa cheo huku akitishia kuacha kazi.

  Miezi michache baadaye akaacha kazi na kumshawishi mwenzake achukue hatua kama hiyo, lakini mwenzake akaamua kubaki. Kuanzia hapo akawa anahama kutoka ofisi moja hadi nyingine, akitafuta mshahara mkubwa zaidi na kama kuna mahali alipodumu kwa muda mrefu, basi si zaidi ya miaka miwili. Hatimaye mtu huyu anakuta jina lake likiwa limeharibika, kwani anakuwa amepitia sehemu nyingi mno kiasi cha kuwatia wasiwasi hata wale wanaotaka kumwajiri.

  Hakuna mwajiri anayetaka kumwajiri mtu asiye na subira, mtu anayejua akimwajiri ataweza kuondoka wakati wowote, tena ghafla na kumsababisha atafute mtu mwingine bila kutarajia. Wakati huyu mmoja akihamahama, yule aliyebaki na kampuni ya mwanzo atajikuta akiwa amepanda na kuwa katika ngazi ya juu, kwani hata mwajiri wake atakuwa anamwamini.
   
 10. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #10
  Sep 25, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,945
  Likes Received: 1,818
  Trophy Points: 280
  unajua Mtambuzi subira haihitajiki wakati wa kuanza mahusiano peke yake bali hata ndani ya mahusiano. mfano uko ndani unaona uliyotarajia kutoka kwa mwenzio hayapo kabisa, upendo hamna yeye na friends zaid kuliko wewe, anajali kazi pesa na pombe kuliko familia unafikir hapo mtu afanye nini? lazima awe na subira, imani na uvumilivu ili kufikia amani aliyoikusudia. asipofanya hivyo safari yake kweye haya mahausianao huishia hapo hapo.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #11
  Sep 25, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Mtambuzi kama nilivosema hapo juu kuashiria ‘men are from mars and women from venus'… What I know (labda nisahihishe wewe kakangu); katika mahusiano ya kawaida wanaume walio wengi akilala kwa mara ya kwanza na huyo mpenzi wake mpya ndio hu determine kama kutakuwa na mahusiano ama Lah! Hali kwa sie wanawake inakuwa tayari ishapitishwa kuwa sasa upo katika mahusiano toka pale ukubaliane nae kuwa mpo katika mahusiano.

  Tukija upande wa kuoa, wanaume kitu ambacho anaangalia kwa huyo mwanamke wa kumuoa ni tofauti kabisa na kwa mtu ambae anataka kutoka nae… Na mara nyingi ukiwa na uchumba na mwanaume ambae ana vigezo vya kuoa (single/financially sustainable/ appropriate age na the like); mpo tu katika uchumba zaidi ya mwaka, wa pili wa katika, wa tatu… Basi hapo possibility ya mwanamke kuolewa na huyo ni ndogo (usishangae unaletewa card ya mchango wa harusi yake). Ndio hapo unapotambuwa kua Subira inatakiwa ipimwe kuwa to what extent inatakiwa kwenda.

  Haya mambo magumu, will be looking forward to your article…
   
 12. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #12
  Sep 25, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,223
  Trophy Points: 280
  asante Mtambuzi nilikuwa nahitaji hili neno....
  kuna jambo nalivutia subiri....acha ni endelee kuvuta subira... sio rahisi ila nakaza roho...
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. Z

  Zero One Two JF-Expert Member

  #13
  Sep 25, 2012
  Joined: Sep 16, 2007
  Messages: 9,390
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  Mtambuzi! unaonekana mkalii sana kwenye haya mambo.
   
 14. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #14
  Sep 25, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Hapo kwenye bold nimecheka sana.....LOL

  Ni kweli dada yangu, kwanza najisikia faraja kuzungumza nawe kupitia uzi huu. Nakubaliana na wewe kwa silimia nyingi tu,
  Hebu soma hii quote yangu, halafu nitasherehesha kile nilichokisema kwa lugha nyingine:
  Nimesema kwa mwanamke kumpata mwanaume mwenye muafaka au niseme mwanaume sahihi ni sawa na kucheza kamari, nilikuwa namaanisha kwamba sio kila mwanaume ni wa kufanyiwa subira, kuna mahali unaweza kufika ukaona dhahiri kwamba hapa subira ni kuendelea kujipotezea muda, wapo wanaume ambao kwa hakika na hata moyo wako unakusukuma uwe na subira, ni kwamba unaona kabisa anayo dhamira ya thabiti ya kukata shauri, lakini kuna mambo madogo madogo yanamtatiza na kama mtashirikiana kwa pamoja mnaweza kufikia muafaka.

  Utajuaje kuwa huyu ndiye sahihi...

  Kuna namna nyingi za kumuangalia mwanaume kwa jicho la tatu na ukajua kwamba huyu ndiye na ndio maana nilisema kwamba ni wanawake wachache wenye utambuzi wanaoweza kumjua mwanaume kama yeye ndiye au siye.

  Nikisema nidadavue namna ya kujua kama mwanaume uliye naye ni sahihi au la, nitakuwa naanzisha uzi mwingine, wakati uzi huu unajitosheleza... Naomba uvute subira siku zijazo nitadadavua hapa MMU ili wote tuweze kujadili kwa pamoja...
   
 15. k

  katawa JF-Expert Member

  #15
  Sep 25, 2012
  Joined: Jan 29, 2010
  Messages: 203
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 60
  kipimo bora cha subira ni kufikia malengo uliyojiwekea kwa njia halali.
   
 16. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #16
  Sep 26, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Nakusalimu mkuu, habari za siku nyingi.........
   
 17. Beb

  Beb Member

  #17
  Sep 26, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  asante kwa thred nzur ila subira is not my strength,kama gred ningejipa C si mbaya ila si nzuri pia..kutokana na hili somo basi itabid niongeze subira.
   
Loading...