Kwa nini Simuamini Rais

Hume

JF-Expert Member
Sep 25, 2007
340
108
Mara nyingi nimekuwa nasikiliza kauli za mh. Kikwete ila huwa nashindwa kuelewa kama anamaanisha anachokisema!

kwa mfano: Wakati anazindua Bunge alisema hatasubiri ushahidi wa mahakama katika kuwawajibisha watendaji wake wataotuhumiwa kwa rushwa, alisema atawastaafisha kwa maslahi ya umma au hata kuwafukuza. Wakituhumiwa leo anasema tusijifanye wapelelezi, mahakimu na wakamataji, anafanya yaleyale aliyosema hatayafanya!

2. Alitoa maagizo kuwa wanafunzi wa shahada ya udaktari na ualimu walipiwe ada 100% vyuoni lkn hakuna kilichofanyika, na sijasikia akitoa maagizo kwa subordinate wake wamweleze ni kwa nini maagizo yake hayajazingatiwa.

Kuna mengi ambayo amekuwa akiagiza bila kutekelezwa na watendaje wake, suala ninalojiuliza mara kwa mara ni what kind of president is he!
 
Hume,

huyu Kikwete ni ..... watanzania walidanganywa na vyombo vya habari vya Rostam vilivyosifia uzuri wa sura yake... hata mtabiri yule wa Dar akatetea ubovu wake wa kutabiri kuwa rais angekuwa mwanamke kwa kusema kuwa Kikwete anamvuto wa kike..

Sasa hili ni fundisho kwa watanzania next time wachague raisi wa nchi na wala sio mtu mwenye mvuto wa kike (I have no idea what the heck is this).....
 
MWK na Hume, panapo ukweli uwongo hujitenga. Huyu jamaa alitoa ahadi chungu nzima zikiwemo za maisha bora, kupambana na rushwa na ufisadi na kuipitia upya mikataba ya uchimbaji wa madini. Yote hayo ameshindwa kuyafanya na badala ya kuwa mtetezi wa Watanzania wapenda haki amekuwa ni mtetezi wa mafisadi na wala rushwa, kama mtakumbuka kauli zake za "Mwacheni mzee wetu astaafu kwa amani." "Kama wana ushahidi waupeleke polisi au mahakamani." na pia kuhusiana na umwagaji wa damu.

Kiongozi mwadilifu huakikisha kwamba hakuna mtu yeyote aliye juu ya sheria. Kama amefanya madudu basi sheria iachwe ifanye vitu vyake. Na kiongozi yeyote aliyekosa credibility ya wale anawaongoza kama Karamagi na wengineo wanastahili kuondolewa madarakani mara moja, badala ya kushinikiza ushahidi upelekwe polisi na mahakamani.

Sasa Mzee Ruksa na Butiku wamemuumbua. Akitoka huko majuu hana jinsi inabidi akae chini kufanya mabadiliko makubwa ya mawaziri na wakati huo huo aonyeshe nia ya kweli ya kupambana na ufisadi na rushwa bila kumuogopa yeyote na pia kuipitia upya mikataba ya madini ili iwe na maslahi ya kweli kwa Watanzania. Vinginevyo atakuwa ni Rais wa awamu moja , maana CCM ni lazima imtoe kafara hapo 2010.
 
Bubu ninakubaliana na wewe kwa ahadi hewa za huyu Rais wa Awamu ya Nne ... ahadi ya kupambana na rushwa na kutosubiri ushahidi pia iliwahi kutolewa na BWM, kwa kiasi kikubwa miaka 5 ya mwanzo aliweza kuwatoa kafara baadhi ya mawaziri wake. Miaka 5 ya lala salama aliziba masikio na ndipo tulipoanza kusikia misamiati mipya ya wivu wa kisiasa! Nina uhakika kwamba miaka 5 ya lala salama baadhi ya mawaziri wa BWM walikuwa tayari wanajua madudu yake na ndiyo maana ilikuwa ni kipindi cha watu kujifanyia wayapendayo na hata kama ni rushwa basi ilikuwa ya wazi zaidi na kila mtu alikula kwa kasi kubwa maana mkuu wa kaya alishaonyesha mfano wa namna ya kula bila kunawa!

Swali linalosumbua wengi ni moja ... je JK ana uwezo wa kufanya hayo mabadiliko? Waathirika wa hayo mabadiliko watakuwa ni wale ambao waliingia kwenye Baraza la Mawaziri kwa njia ya mlango wa nyuma, lakini kama ni mmoja wa wana mtandao basi swala liko wazi kabisa kwamba hawezi kuwagusa. Kauli zake za hivi karibuni akiwa nchini zimeonyesha wazi kwamba hayuko interested na swala la kufuatilia hizo tuhuma na ndipo tunapoambiwa kwamba watu wanaoibua skendo hizo wana uchu wa madaraka na kwamba wanataka damu imwagike. Nani kasema kuna mtu anataka kumwaga damu? Hoja ya wapinzani ni kuwashughulikia mafisadi, lakini yeye haoni kama kuna mafisadi. The very same person leo hii akiulizwa swala la Buzwagi na Bwana Gordon Brown unaweza kushangaa kusikia majibu ya JK kwamba linashughulikiwa na wote wataogundulika kuhusika watashughulikiwa! Kauli kama hiyo hawezi kuitoa akiwa Tanzania kwa kuwa anajua kwamba anachokisema ni uongo mtupu na unafiki wa hali ya juu kabisa. Ndiyo maana akina Karamagi wameonyesha wako kwenye process ya kudai bilioni 10 kwa barua ya 24/9, leo ni 17/10 (almost mwezi mzima tangu notice hiyo itolewe) wala hatujasikia kama kuna jalada limefunguliwa na Karamagi alitoa siku 2 za kuombwa msamaha vinginevyo atawaburuza wahusika mahakamani. Sijaona Karamagi, wala Mgonja wala Rutta ambaye kaenda huko mahakamani! Sasa sijui hiyo ndiyo new fashion ya kujisafisha majina kwa kutishia kwenda mahakamani halafu unaingia mitini kiaina? Wanajua wazi kwamba hawawezi kuguswa maana kwenye hilo kundi la mafisadi wanajuana kama wana mtandao na madhambi ya kila mmoja yako wazi na hivyo JK akianza kuwashughulikia kwa kuwatoa kafara, basi inawezekana wakamgeuka na yeye akazamishwa kwenye dimbwi la madhambi ya ufisadi, maana tunayoyajua kuhusu JK ni machache sana na inawezekana ni fisadi mzuri sana ila hafanyi yeye moja kwa moja kwa kuwa alikuwa na motive ya kugombea urais. Wengine kama akina EL walijikatia tamaa tangu 1995 walipoambiwa waeleze utajiri wao wameupata wapi na kwa kipindi kifupi sana!
 
Kufanya mabadiliko kutakuwa na ugumu mkubwa. Baada ya mgawanyiko mkubwa uliotokea ndani ya CCM katika kinyang'anyiro cha 2005, baada ya kuingia madarakani hakutilia maanani kuuvunja mtandao na kurudisha umoja ndani ya CCM. Sasa mgawanyiko huo utampa mtihani mkubwa katika kuteua baraza jipya la mawaziri maana mawaziri wengi ni wana mtandao, hivyo ili kubadilisha baraza hilo inabidi awaweke wale ambao sio wana mtandao.

Ama kweli wahenga walisema mdharau mwiba mguu huota tende. Alishauriwa mara nyingi tu kuuvunja 'mtandao' lakini hakuona umuhimu wa kufanya hivyo. Sasa mtandao huo huo utamwaathiri yeye mwenyewe katika kufanya maamuzi yake ya baraza jipya la mawaziri ambalo linasubiriwa kwa hamu na Watanzania.
 
Muungwana hashauriki,ni mtu wa kupenda kusifiwa tu sasa unategemea maendeleo yatakuwapo?
 
Swali linalosumbua wengi ni moja ... je JK ana uwezo wa kufanya hayo mabadiliko?

Keil na wana JF wengine, naungana nanyi kuwa hakuna kiongozi yoyote wa sisiemu ya sasa anayeweza kumwajibisha mwenzake! Hawana utashi wa kisiasa, wote ni wachafu, wote watenda madhambi, sasa nani amwajibishe nani? Mabadiliko ni magumu sana, hawezi kuwatoa wanamtandao kwa sababu ndio waliomuweka pale alipo. Akishawatoa atawapeleka wapi? Fadhila zao atazilipaje? Ni ngumu!
Lakini mimi bado nasubiri "Maamuzi Magumu" aliahidi Kikwete wakati anaingia madarakani. Huenda hili la kuwawajibisha watu wake likawa mojawapo. Tukumbuke kauli za Sumaye kuhusu muungwana.
 
Sasa mnamkumbuka na kumuimbia nyimbo Bungeni..
 
Back
Top Bottom