Kwa nini-SIASA? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa nini-SIASA?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lole Gwakisa, Jun 24, 2009.

 1. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #1
  Jun 24, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Wandugu, nina swali la muhimu sana.
  Watanzania wengi sana wanapenda kujadili na kuona kuwa SIASA ndio kila kitu.
  Kinyume na hilo waTanzania wengi ni wavivu ukilinganisha na majirani zetu wa Kenya na Uganda.Ukianzia ngazi za juu , utendaji wa kazi bado ni mdogo aidha kwa utendaji na utatuzi wa matatizo ya kijamii(actual problem solving).
  Leo bado kuna majopo, makongamano, warsha na semina za kila aina, muda tosha wa kutatua matatizo ya kijamii. Hivi sasa uwanja wa mambo haya ni Mnazi Mmoja badala ya Bagamoyo.
  Je ni KWA NINI watu hupendelea zaidi SIASA kuliko kufanya kazi za kujiingizia kipato?
   
 2. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #2
  Jun 24, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Mkuu siasa ndo kila kitu kwa Tanzania, analo lisema mwana siasa ndo final, utaalamu hauna nafasi katika maamuzi nchini kwetu, ulaji wote upo kwa wana siasa, nani asiye taka hilo? ndo maana kilicho kikubwa kwetu ni siasa!

  Kama siasa inaamua mwizi fulani asiguswe hata na sheria zetu wenyewe hadi PM anaapa bora asurubiwe lakini wizi huo usisemwe, what else do you want?
   
 3. O

  Ogah JF-Expert Member

  #3
  Jun 24, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  1. mustakabali wa maisha yetu ya kila siku.....its very unfortunate though.......umeshikiliwa na wanasiasa..........

  2.Ni kweli watendaji wengi serikalini ni wavivu kwa sababu accountability ni ZERO na jinsi system ilivyo....inalea wazembe......they always get away with blunders thay make or institute........tunatakiwa tuwe na performance based contracts kwa wafanyakazi wote serikalini........

  ..........na sisi wana JF tusiache kuwaasa na kuwakumbusha ndugu zetu kuwa tufanye kazi na tuache blah blah.........."no free lunch"
   
 4. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #4
  Jun 24, 2009
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Sio ukweli kwamba watu wanapenda Siasa kuliko kazi za kuwaingizia kipato.
  Sio ukweli kwamba watanzania ni wavivu kuliko wakenya na waganda.
  Kujadili siasa ni hobby ya watanzania wengi na hakuna ubaya kwenye hili. Waingereza wanapenda kujadili vilabu vya mpira. kuna wanaopenda kuajdili macelebrity etc.
  Imetokea tunavutiwa zaidi na mijadala hii kwenye free time yetu, haimaanishi kuwa hatufanyi kazi.
   
 5. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #5
  Jun 24, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Sawa sawa Mkuu, lakini inaelekea tunatumia muda mwingi sana ambao hauna mwisho na mijadala mingi inaishia hewani, aidha utekelezaji wa matokeo ya mijadala hii ya kisiasa unakuwa haupo.Na hapo ndio naona kuna upotezaji wa muda muhimu sana ,muda ambao ungetumika kwa maendeleo.
   
 6. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #6
  Jun 24, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Siasa ndio maisha yetu Tz na wanasiasa ndio wameipeleka na kuifikisha nchi hapa ilipo. Kujadili siasa ni kujadili mstakabali wetu. Tukinyamaza tumekwisha.
  Si kweli kwamba watu hawafanyi kazi. Bwana we watu katika nchi hii wanafanya kazi ujapata kuona lakini wanaibiwa kwa kasi ambayo hujapata kuona tangu kuumbwa kwa Tanganyika.
   
 7. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #7
  Jun 24, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Hauoni kwa kuweka bandiko kwenye jukwa la siasa na kujadili siasa wewe ni mmoja wa hao watu unaowasema kwenye thread yako? Umekua interested na wewe umeamua kujadili kwa hiyo labda ukiji tazama mwenyewe utapata jibu. Maybe tunafuata mkumbo, maybe kwa kuwa kila mtu ana interest na siasa kwa hiyo na sisi tunaamua kuingia ili tujionee wenyewe kwa nini kama ulivyo fanya wewe mkuu.
   
 8. L

  Limbukeni Senior Member

  #8
  Jun 24, 2009
  Joined: Feb 27, 2009
  Messages: 117
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ndio maana tanzania for change dot gov inasema mahesabu badala ya siasa mfano mradi wetu mama wa maths for all ni kufundisha hisabati kwa level zoto ili tuwe na walimu wengi wa maths nakupata kazi kila pembe ya dunia
   
 9. J

  Jafar JF-Expert Member

  #9
  Jun 24, 2009
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 1,138
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Siasa is what pays the most in Bongo. From a mere radio presenter, through sect clergies, footballers, choir singers, doctors (name it) to a professional practising professor, all of them are struggling to be politicians. We have taken this country so far that everybody believes that the only quick way to win is to be a successful politician. Unless, this utopia is changed this will continue to be a Tanzanian norm.

  We need about turn, we need to pay people according to their deliveries and I believe this is the only way to get people to value professionalism. I cant be sitting in a desk say as a medical doctor, while my siblings cant go to good school, hard to meet my daily needs, land-lord is always on my nose, no better retirement benefits etc. What do you expect?

  This has a long history back to those old JKN (RIN) days of "fikra sahihi za mwenyekiti" or "chama kushika hatamu (kamba ya kuongozea farasi)". JKN (RIP) had mistakenly declared that this country is for "peasants and workers". So poor boys and girls were all struglling through many years of schooling just to become an employee. The opposite of that you remain in villages to farm. This is the Tanzania we see today. Foreigners were enchored in business (Indians etc) and we were left to sing CCM acronyms and dance before Uhuru torch.

  Mungu Ibariki Tanzania.
   
 10. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #10
  Jun 24, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Siasa inasomewa wapi wakuu, au inabidi uwe fundi wa mipasho,fitna ,wizi na udanganyifu?
   
 11. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #11
  Jun 24, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  LOLE,
  Tafadhali KANUSHA sentesi hii waTanzania wengi ni wavivu.
  Unatumia takwimu zipi?
   
 12. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #12
  Jun 24, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,336
  Likes Received: 1,801
  Trophy Points: 280
  Siasa tatizo lake inagusa kila kitu.Hakuna mahospitali,mabank, barabara nzuri etc kama siasa ni za rushwa au ufisadi tunaouona.Ili maendeleo yawepo basi siasa ni lazima iwe imekaa vizuri. Nafikiri kwa muda wa sasa ni kushirikiana wote kuelimishana na kukumbushana umuhimu wa kufanya siasa safi ili basi mambo mengine nayo yaweze kuchukua mkondo wake.
   
 13. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #13
  Jun 24, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Lole,

  Blah blah! haziwezi kupimwa tofauti na utendaji. Ndio maana wasanii wote hupenda kujikita kwenye siasa za makongamano semina na vitu vingine. Kwanza wanalipwa kwa kupoteza muda huko na pia hakuna performance measurement kwenye hizo semina. Bora uende na utapata posho. Labda huko kwenye semina na kongamano kuwe na mitihani na matokeo yake yatangazwe hadharani.

  Utendaji wetu Watanzania ni mbovu sana. Ukitaka kujua ubovu wa utendaji wa Watanzania, wewe uwe mfanyabiashara ambaye unatafuta haki zako kwenye hizo ofisi za serikali na makampuni binafsi. Yaani kuna watu mimi badala ya kuchukia ninaangua kicheko. Ubabaishaji mkubwa sana!
   
 14. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #14
  Jun 24, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Kwani uwongo? Ni ukweli mtupu! Of course labda uvivu huo una sababu ambazo zinaweza kueleweka lakini kwasasa Watanzania wengi ni wavivu sana!

  Blah blah! chungu nzima huku nchi inaliwa na wajanja, sisi ni kupiga sogo tu, kusoma magazeti ya mapapa na manyangumi ambao hawana hata mpango na maendeleo ya mtu wa kawaida.

  Nakubaliana na Lole, Watanzania walio wengi tu wavivu mno!
   
 15. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #15
  Jun 24, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mtanzania, Lole,
  Mnapata wapi ujasiri wa kusema kuwa watanzania wengi ni wavivu?
  Mbona hamtoi takwimu?
  Je ninyi ni kati ya hao wavivu au la?
   
 16. m

  mokant Member

  #16
  Jun 24, 2009
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  jamani hebu angalieni kwamba hata elimu yetu nayo inaendeshwa kisiasa zaidi , eti kuanzia darasa la kwanza hadi la saba mwanafunzi husomeshwa kwa kiswahili alafu sekondari kwa kiingereza. Hii inachangia watu wa nchii hii kutopata elimu inayofaa na hivyo wengi wao huona siasa ndio kimbilio kwani kwa hakika siasa humpatia mtu nguvu ya kuamrisha bila ya kujali elimu aliyonayo.
   
 17. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #17
  Jun 24, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Exaudi ndugu yangu,hebu nikupe mchanganuo mdogo wa mfanyakazi wa kawaida ambaye nimem-monitor ukilinganisha na mfanyakazi mwingine niliyem-monitor hapa hapa nchini na kugundua ni kwa nini hatuendelei.
  Mtanzania :Mgeni
  Saa za kazi:saa 2- saa 10=8hrs : saa1-saa 12=10hrs(lunch 1hr)
  (Tz actual work hrs=5hrs)
  Siku za kazi kwa wiki: 5days: 7days

  Siku za kazi kwa mwezi: 22days :26days

  Miezi ya kazi: 11 months :11months

  Actual productive work hours per year: Mtanzania= 1,210 work hrs
  Mgeni = 2,860 work hours

  Huu ni utafiti uliofanyika na umeonekana kuwa ni kweli kabisa.
  Hivyo basi mkuu Exaudi, kama tuna resource moja kubwa sana ya MUDA,matumizi ya muda huo kwa waTanzania ni matatizo.Katika muda huo huo wenzetu wanafanya kazi kwa bidii sana(twice!).
  Hivyo basi kwanini wasiendelee?
   
 18. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #18
  Jun 24, 2009
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135

  Haitakuwa na maana kuweka sehemu nyingine zaidi ya jukwaa la siasa ambako ndiko kila mmoja yuko.
  Mtu akitaka kutangaza na JF, tuseme anatangaza biashara yake ya nyanya na kuuza mapapai - atakuwa hajafanya la maana asipoweka hilo tangazo jukwaa la siasa.
   
 19. Kilasara

  Kilasara JF-Expert Member

  #19
  Jun 24, 2009
  Joined: Dec 21, 2008
  Messages: 578
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Uongozi wa Tz bado haujatambua kwamba wananchi ni lazima wawezeshwe kufanya kazi kwa kujituma kuzalisha na sio kufanya biashara.

  Mabilioni ya Kikwete yaliishia kununua bidhaa nyingi za nje (na kidogo za ndani), nyingi zikiwa mitumba; badala ya kuingizwa ktk kilimo na viwanda vidogo vidogo kuzalisha mazao ya chakula na bidhaa nyingine za matumizi halisi. Matokeo ni chakula kuendelea kuwa adimu na njaa kukithiri.

  Hata kauli mbiu ya KILIMO KWANZA iliyosisitizwa na Rais wetu na Mhe. Mkulo juma lililopita, itakuwa ni maneno matupu kwa vile Bajeti yenyewe imetenga asilimia chini ya 7 kwa sekta ya Kilimo.

  Cha ajabu zaidi ni kwamba, fedha hizi za kilimo nyingi zitakwenda ktk mikoa sita yenye rotuba na mvua ili kuzalisha chakula. Na "chakula" hapa inamaanisha mahindi.

  Mikoa yenye ukame, ambapo wananchi wanahitaji msaada zaidi ili waweze ku-survive haipewi msukumo stahili. Wanahitaji msaada wa Serikali kupata irrigation facilities na elimu kuweza kukuza mazao kama mtama na serena vinavyostahimili ukame. Elimu kuwezesha WaTz kutumia vyakula zaidi ya mahindi ni muhimu. Hata kunaweza kuwa na vipindi maalum vya kufundisha mapishi bora ili vyakula hivi vituokoe kutoka baa la njaa.

  Viazi, mihogo, ndizi , mtama na serena viwe vinaongezea mchele, ngano na shairi ktk mazao ya chakula ktk hii nchi yenye maeneo makubwa yanayongoja kulimwa.

  Tunahitaji siasa zenye kutilia mkazo kujikomboa kutoka kwenye umaskini, badala ya siasa za kufunifunika ufisadi na ubadhirifu wa mali ya umma,
   
  Last edited: Jun 24, 2009
Loading...