Kwa nini shikamoo siku hizi imegeuka uhasama kwa wenye kustahiri kupewa?

TzComedy

JF-Expert Member
Jul 15, 2017
890
700
Juzi nusura nivunjwe Jicho langu la kulia baada ya kurushiwa ngumi moja takatifu, kilichonishangaza sio kurushwa kwa ngumi hiyo ispokuwa mtu mwenyewe alienirushia hiyo ngumi takatifu.

Kwakweli yule mtu kama ni chuvi, hakika nawaambia kaila na sio kaila tu, bali kaila vilivyo.

Chanzo ni huu utamaduni wetu wa shikamoo kwa yule unaeona kakuzidi umri, ni kawaida yangu na ndio nilivolelewa na kufundishwa na wazazi na hata walezi pia kuwa kwa mujibu wa utamaduni wetu sisi watz, mtu aliekutangulia kuliona Jua kumpa Shikamoo si jambo la mjadara bali ni la mtekerezo, kwahiyo tangia hapo najiona mwenye fahari kubwa kukupa haki yako ya Shikamoo wewe ulienizidi kwa umri.

Hasa inakuwaje mimi mtoto mwema natekeleza wajibu wangu kwako kwa kukupa Shikamoo yako alafu unataka kunipa kilema cha maisha?!, mboni kwenye Daradara nikikupisha kwenye siti kwa kuamini wewe ni Mkubwa kwangu kwa hiyo unastahili kukaa kuliko mimi kwa utamaduni wetu, hauwi Mbogo?.

Waenga shikamoo ni haki yenu, mboni hamuitendei haki Shikamoo kwa nini??.
 
Kweli wamama na wababa wa mjini hawapendi shikamoo utasikia asante,salama,nimekuzalia mamako? Tena ole useme shkamoo baba/mama utakiona! Na wengn hawajb wanakukata jicho tu so kawaida we chukulia poa japo vingn vibabu kbs
 
ila salamu ya shikamoo imekaa ki umwinyi mwinyi sana , mimi mwenyewe tangu nipate akili za kiutu uzima sitoi shikamoo
 
Sababu inatumika kuhujumu maslahi yetu..! Nikisalimiwa na mdada namuuliza unataka kuninyima nini??
 
Mimi hata akiwa kibibi huwa shikamoo mapaka adai mwenyewe, yaani unakuta mama au mdada mtu mzima hataki shikamoo, za saa hizi ndio mpango nzima
 
Juzi nusura nivunjwe Jicho langu la kulia baada ya kurushiwa ngumi moja takatifu, kilichonishangaza sio kurushwa kwa ngumi hiyo ispokuwa mtu mwenyewe alienirushia hiyo ngumi takatifu.

Kwakweli yule mtu kama ni chuvi, hakika nawaambia kaila na sio kaila tu, bali kaila vilivyo.

Chanzo ni huu utamaduni wetu wa shikamoo kwa yule unaeona kakuzidi umri, ni kawaida yangu na ndio nilivolelewa na kufundishwa na wazazi na hata walezi pia kuwa kwa mujibu wa utamaduni wetu sisi watz, mtu aliekutangulia kuliona Jua kumpa Shikamoo si jambo la mjadara bali ni la mtekerezo, kwahiyo tangia hapo najiona mwenye fahari kubwa kukupa haki yako ya Shikamoo wewe ulienizidi kwa umri.

Hasa inakuwaje mimi mtoto mwema natekeleza wajibu wangu kwako kwa kukupa Shikamoo yako alafu unataka kunipa kilema cha maisha?!, mboni kwenye Daradara nikikupisha kwenye siti kwa kuamini wewe ni Mkubwa kwangu kwa hiyo unastahili kukaa kuliko mimi kwa utamaduni wetu, hauwi Mbogo?.

Waenga shikamoo ni haki yenu, mboni hamuitendei haki Shikamoo kwa nini??.
Nakwambia suala hili lumekuwa changamoto kubwa sana leo hii.

Ukiwa unatoka kituo kikubwa cha gerezani pale dsm unakuja maeneo ya machinga complex, mkono Wa kushoto kabla hujavuja hii road ya kwenda karume, kunae Mzee mmoja huwa anachoma mahindi hususan mida ya jioni.

Nilipita pale nikisubiria gari zenye seat kuelekea Machimbo. Nikawa pale kwa muda. Nilimuona nikamsalimia jioni ile. "Shikamoo Mzee". Hapo nilijipalia mkaa mwenyewe aisee. Kwanza nilishtukia nimerushiwa kipande cha mhindi kikatua shavu langu la kushoto. Sijakaa vzuri naona anaanda mazaga mengine kunishambulia.

Abiria wenzangu wakaanza pambana nae wakati huo mi sjaelewa kinachoendelea. Hali ilivotulia ndo nikaanza kumsikia akifoka(huku jamaa wamemshilia), pumbafu sana. Wazee umewaacha *******(matusi makali) halafu unakuja kunambia Mimi shikamoo?

Namwambia kuanzia sasa, nikiwa DSM siangalii sura ya mtu. Nimeachana na utamaduni huo kabisa.

Duh!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom