Kwa nini serikali yetu ina nongwa kiasi hiki? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa nini serikali yetu ina nongwa kiasi hiki?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, Sep 17, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Sep 17, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Wana-JF:

  Katika haya nitakayowaeleza nimeshindwa kupata neno sahihi mbadala wa ‘nongwa' lakini pengine labda ningetumia ‘kiburi' au ‘jeuri' ya kuonyesha hali ambayo kusema kweli sijui chimbuko lake. Ni hivi:

  Ukilinganisha na jirani yetu Kenya, kwa muda mrefu Tanzania imekuwa inaonyesha tabia ya ukiburi katika masuala mbali mbali na hasa ya siasa na demokrasia. Unaweza kusema viongozi wa serikali ya CCM hawataki ku-adopt a liberal policy kama vile Kenya. Ntatoa mifano ifuatayo:

  1. Baada tu ya upepo ya demokrasia kubadilika duniani mwishoni mwa miaka ya 1980, Kenya ilikuwa ya kwanza kupata vyama vingi na kuwa na uchaguzi mwaka 1992. Hapa tulichelewa hadi 1995. Kwa nini?


  2. Hata kabla ya kuja kwa Katiba yao hii mpya ambayo hakika ni masterpiece kwa standard ya katiba nyingi za Barani humu, ilikuwa rahisi sana kuanzisha chama cha siasa na kukiandikisha katika kipindi cha wiki moja tu. Hapa Tanzania ni kazi kubwa, labda kama chama tawala kinataka chama hicho kuandikishwa kwa haraka kukidhi mahitaji yake,

  3. Kuungana kwa vyama (yaani ku-form alliances). Wenzetu Kenya hiki ni kitu rahisi tu – vyama vinaungana – katika chaguzi – huku vikibakia na identities zao. Hapa kuungana – hata kama ni katika alliance kwa ajili ya uchaguzi – ni kwamba lazima chama kimoja kijifute.

  4. Ushindi katika kura ya urais. Kenya ni lazima mshindi apate asilimia 50+ ili atangazwe kuwa mshindi, la sivyo kuna run-off kati ka wagombea wawili wa juu. Hapa kwetu ni simple majority yaani tunaweza kuona mwaka huu JK akichaguliwa kwa asilimia 45 tu ya kura zote na akina Slaa, Lipumba, na wengine wakigawana zile asilimia 55.min


  Ajabu ya hii ni kwamba katika uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi Kenya wa 1992 hawakuwa na ulazima mshindi kupata asilimia 50+ ya kura zote, lakini walipoona kasoro kubwa ya kidemokrasia (Moi alishinda kwa asilimia 35 tu ya kura zote) walibadilisha na kuweka ulazima wa kupata asilimia 50+. Kilichotokea hapa ni kinyume chake – yaani uchaguzi wa mwaka 1995 kulikuwa na ulazima asilimia 50+ lakini baadaye walibadilisha hii na kuiondoa.

  Hii ni mifani michache katika nyanja ya uendelezaji wa demokrasia. Kuna mengine kama vile kwa mfano, baada ya EAC ya zamani kuvunjika, Kenya iliwalipa raia wake waliokuwa katika jumuia hiyo mafao yao mara moja baada tu ya mgawanyo wa mali. Hapa nongwa ilitawala, Watanzania hawakulipwa hadi 2005, kiduchu na baadsa ya kupelekana mahakamani. Kwa nini viongozi wetu wanakuwa na tabia ya unyimi unyimi tu kwa raia zake?

  Kiburi hiki, na ubanaji huu wa demokrasia katika nchi yetu iaashiria nini? Jibu nadhani inaashireia kitu kimoja tu – kwamba pindi ikifika wakati ambapo vitu hivyo ni lazima vije, basi vitakuja kwa mtikisiko mkubwa nchi hii haijapata kuona. Viongozi wa CCM (kama wapo wenye kuona zaidi ya urefu wa pua zao) waliangalie hili, walirekebishe ili kuepusha janga.


   
Loading...