Kwa nini serikali ya Tanzania haiwapendi wananchi wake? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa nini serikali ya Tanzania haiwapendi wananchi wake?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sarikoki, Jul 27, 2012.

 1. s

  sarikoki JF-Expert Member

  #1
  Jul 27, 2012
  Joined: Sep 30, 2011
  Messages: 1,196
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Ni swali ninalojiuliza kila siku lakini sipati jibu,kila siku ya Mungu inayopita watawala wetu wanalala wakiwaza mbinu mpya ya kuzidi kumdidimiza huyu mlalahoi.

  Utaniuliza nina ushahidi gani....kama kawaida yetu na mimi nitakuuliza ni lini umesoma magazeti au umesikiliza taarifa ya habari ambayo haina habari ya kummaliza MTanzania? ni lini umesoma sheria mpya inayompa matumaini MTanzania? Ni lini umesikia MTanzania akiifuraia badget ya serikali? ni lini mwekezaji amemnyanyasa MTanzania akachukuliwa hatua?

  Watu wananyang'anywa mali zao... wananyang'anywa ardhi zao.... wanafungwa kwa kubambikizwa kesi....wanapigwa risasi kwa kudai haki zao za msingi...wanateswa kwa kuhoji mambo ya msingi..... na kubwa zaidi ni hili linaloendelea sasa hivi hata mafao yao wanataka kuporwa kisiasa.

  Nimesoma kuhusu viwanja vya gezaulole nimegundua sasa wanataka kuwa na ngome yao... nafikiri ni ngome ambayo itavitenganisha na kuvilinda vizazi vyao na mlalahoi.

  Najiuliza hii amani itaweza kuendelea kweli kwa namna hii?. Kwa nini wanaishi kama vile hamna kufa? Kwa nini wanaifanya Tanzania kua mali yao?

  Mungu atusaidie na tuendelee kumuomba Mungu atubariki na atuondoe kwenye hili wingu jeusi.
  Mungu ibariki Tanzania Mungu ibariki Africa.
   
 2. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #2
  Jul 27, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  UJAMBAZI,ULIMBIKIZAJI MALI na ndio maana tunawaponda kila leo iyendayo kwa MUNGU!

  (UBINAFSI)
   
 3. k

  kimeloki JF-Expert Member

  #3
  Jul 27, 2012
  Joined: Jul 9, 2012
  Messages: 1,931
  Likes Received: 954
  Trophy Points: 280
  kazi ya walaji ni kula, but days are numbered.
   
Loading...