Kwa nini Serikali Ya CCM Haichukui Hatua Dhidi ya Majangili Wa Kisomali

Muke Ya Muzungu

JF-Expert Member
Jun 17, 2009
3,444
264
Rasilimali zetu zinazosimamiwa na serikali ya CCM hasa wanyama wetu, mara nyingi wanamalizwa na maharamia wa Kisomalia. Tembo wengi Serengeti wameuwawa na maharamia wa kisomali. Faru nao wamewindwa na kuuwawa na hao hao maharamia wa kisomamali wanaoingia mbugani kupitia mkoa wa Arusha na Mara. Je ni kwa nini serikali ya CCM imefumbia macho hawa majangili wakati wanamaliza rasilimali zetu na kuleta hofu kubwa kwa wakazi maeneo ya mbugani ? hii serkali ina mikakati gani kutokomesha hawa watu kuingia kwenye Mbuga zetu na silaa nzito za kivita?
 
Kwa sababu ndani ya ccm wako viongozi ambo ni majangili na wana mtandao mkubwa wa kuiba rasilimali zetu na kuuza nje ya nchi.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Naskia majangili wamefanya party huko manyara baada ya kinana kulamba utendaji mkuu wa wizi
 
Haaa Hapo hakuna hatua kubwa wala ndogo inayoweza kuchukuliwa ndani ya Chukua Chako Mapema, nani asiyependa gari zuri na nyumba nzuri, Totooz na Serengeti Boys ndani ya CCM, Si umesikia juzi tu wamepweka kushughulikia Ishu ya manoti ya Uswis, Eti wanataka majina toka kwa wananchi, Je polisi, Usalama wa Taifa, na Interpal wanafanyakazi gani? na Jamaa aliyetoa taarifa si anajua alichokua anasema Pale Bungeni , ila wasi wasi wangu asije akawa ashapewa chake nae
 
Rasilimali zetu zinazosimamiwa na serikali ya CCM hasa wanyama wetu, mara nyingi wanamalizwa na maharamia wa Kisomalia. Tembo wengi Serengeti wameuwawa na maharamia wa kisomali. Faru nao wamewindwa na kuuwawa na hao hao maharamia wa kisomamali wanaoingia mbugani kupitia mkoa wa Arusha na Mara. Je ni kwa nini serikali ya CCM imefumbia macho hawa majangili wakati wanamaliza rasilimali zetu na kuleta hofu kubwa kwa wakazi maeneo ya mbugani ? hii serkali ina mikakati gani kutokomesha hawa watu kuingia kwenye Mbuga zetu na silaa nzito za kivita?
Huwezi kutofautisha CCM na Majangili
 
Back
Top Bottom