Kwa nini Serikali Isijenge Ofisi zake Nje ya Mji Badala ya Kupanua Barabara? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa nini Serikali Isijenge Ofisi zake Nje ya Mji Badala ya Kupanua Barabara?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by M.L., Sep 24, 2012.

 1. M

  M.L. Senior Member

  #1
  Sep 24, 2012
  Joined: Feb 11, 2012
  Messages: 184
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa sasa serikali imekazana kupanua barabara na reli katika jiji la DSM ili kupunguza foleni jijini. Ujenzi wa barabara unagharimu fedha kama ambavyo ujenzi wa ofisi mpya nje ya jiji ungegharimu. Na tatizo la barabara kutotosha ni endelevu. miaka ijayo barabara zitapanuliwa na kujengwa tena. Magari yanaongezeka na wakazi wa mijini wanaongezeka kila uchao.

  Gharama za ujenzi na ubomoaji nyumba unagharimu fedha nyingi. Na bado wanataka kuhamia Dodoma.

  Je! Isingekuwa vema zaidi kujenga majengo " Complex" nje ya kila manispaa ambayo yangetumika kuwa ofisi za serikali na idara zake? Hii ingeokoa fedha na usumbufu kwa watu wanaobomolewa nyumba kila kukicha kwa kigezo cha upanuzi wa barabara.
   
Loading...