Kwa nini serikali isijenge kiwanda cha ku process madini hapa tanzania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa nini serikali isijenge kiwanda cha ku process madini hapa tanzania?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kubingwa, Jan 11, 2012.

 1. K

  Kubingwa JF-Expert Member

  #1
  Jan 11, 2012
  Joined: Apr 23, 2010
  Messages: 502
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Jamani wadau wa jf,hili la mchanga wenye madini kupelekwa nje litakoma lini? Au ndo moja ya makubaliano katika mikataba na kwa nini hii mikataba inaendelea kuwa siri? Inauma jamani,kama serikali haina pesa si watafute makampuni ya nje na ndani au hao wanaochimba hayo madini wabanwe wa process hapa hapa.Viongozi wanalalamikia tatizo la ajira bila kuchukua initiatives,kulalamika hakusaidii viongozi wangu!
  Wadau hili mnalionaje?
   
 2. The Stig

  The Stig JF-Expert Member

  #2
  Jan 11, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 881
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 80
  Kila aina ya Ore (mchanga) una namna yake ya kuuchuja utoe madini. Aina ya mchanga hupelekea aina ya kiwanda cha kusafosha. Mchanga wa Geita, kwa mfano, unasafishwa kwa kiwanda cha Carbon in Leach (CIL) tanks, ambazo ni chemical zaidi, kabla ya electrolysis na mwishoni uyeyushaji.

  Mcahnga wa Kahama una copper nyingi. Ili kuitoa dhahabu bila kupoteza copper nyingi, inahitaji kiwanda cha aina nyingine chenye electrolysis zaidi. Kukijenga kiwanda kama hicho TZ haileti economic sense kwa sababu;

  1. Copper inayopatikana hai-justify kujenga kiwanda cha namna hiyo
  2. Umeme unaohitajika ni mwingi sana
  3. Hauwezi ukasema upeleke kwenye migodi ya copper ya Zambia ili utoe copper, kwa sababu migodi ya Zambia haikujengwa kwa ajili ya kuchuja dhahabu.

  Kutokana na hiyo, Barrick hupeleka mchanga wenye copper Japan, ambako kuna kiwanda kinachoweza kufanya hii kitu. Vwanda kama hicho vipo vichache sana ulimwenguni na ni migodi mingi tu inayovitumia.

  Wazo lako la kutaka serikali ijenge kiwanda ni potofu kutokea mwanzo. Serikali haiwezi ikafanya biashara - siyo TZ tu, bali duniani. Hasa hii biashara ya migodi, haiwezi kabisa - sahau na uache kuwadanganya wananchi
   
 3. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #3
  Jan 11, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  tulijenga kiwanda cha makaa ya mawe rais akakiiba,sasa tukijenga cha kusafisha madini si watatuua?
   
 4. The Stig

  The Stig JF-Expert Member

  #4
  Jan 11, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 881
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 80
  Mifano mingine ya jinsi type ya mchanga unavyopelekea aina ya kiwanda;

  1. Ghana kuna kiwanda kinachotumia aina ya funza ndani ya matanki makubwa kutoa dhahabu kwenye mchanga. Huu mtambo upo Obuasi Gold Mine (mgodi mkubwa kuliko yote nje ya SA) na unaita Biox Plant.

  2. Huko Guinea, kuna mgodi unaitwa Siguiri. Mtambo wao ni wa kuweka mchanga kama matuta makubwa na kuyamwagia acid - Unaitwa Leaching.

  4. Ukienda Chunya utakutana na wachimbaji wadogo wadogo. Huu uchimbaji mdogo mdogo kwa kweli uko kinyume kabisa na wafanyakazi humo hufanya kazi katika mazingira hatarishi na ya kitumwa kabisa. Uhalifu na Ushirikina unatawala kila nyanja ya maisha. Hawa waheshimiwa mtambo wao ni mgongo wa binaadamu na mercury (zekali) kwa wingi. Merrcury ina sifa ya kupunguza maisha ya mtu kwa kiasi kikubwa sana.

  Vile vile kuna njia nyingine nyingi. Unatakiwa uelewe hili ili uache ku-generalize kuwa kila kitu unachoona ni ufisadi.
   
 5. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #5
  Jan 11, 2012
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,422
  Likes Received: 393
  Trophy Points: 180
  Tawire!

  The Stig, nawe ni mmoja wa watz wachache wanaojua hiyo fact.

  Years back I was a metallurgist in the gold mines, you have reminded me that.
   
 6. Kinyungu

  Kinyungu JF-Expert Member

  #6
  Jan 11, 2012
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 4,380
  Likes Received: 3,340
  Trophy Points: 280
  Kule kile walisema wanaanzisha enzi za mkapa kule vingunguti sijui kiliishia wapi
   
Loading...