Kwa nini sasa hivi ndoa nyingi hazidumu sana

kabila01

JF-Expert Member
Apr 21, 2009
4,235
4,949
Habari wana JF
Hapa mtaani nimeshuhudia ndoa kama 4 hivi zimevunjika na hazijadumu zaidi ya miaka miwili, pia nina rafiki zangu ambao nimesoma nao chuo kikuu nao ndoa zao zimevunjika wakati muda si mrefu walikua wakitusumbua kwa michango ya send off na harusi.
Bado najiuliza tatizo ni nini tofauti na wazee wetu wao wamefanikiwa kutulia kwenye ndoa zao mpaka katika umri wao huu wa uzee
 
Si watu wanaoana fashion tu, hawajali kama wako inlove wala nini , kila mtu anaangalia maslahi yake
 
Siku moja babu yangu aliniambia usimdanganye mwanamke unayetaka kumuoa.weka ukweli wote mezani alafu aamue mnaoana au la
 
tatizo wanaume mnafungua sana hizo zipu zenu hamjali kama mmeoa wala nini, na kinachowapa kiburi ni kuamini kuwa kwa kuwa umeoa basi hata ufanyaje mkeo hawezi kukuacha,bt its unfortunately wanawake wa hivyo hawapo tena kwenye jamii yetu, wanawake wa sasa ni dot com zaidi, hawawezi maisha walioshi mama zetu,wewe kama unajiona bado unahitaji kufungua sana hiyo zipu yako usikimbilie kuoa maana na wewe utaingia kwenye hiyo list ya marafiki zako
 
ni ngumu sana kuwa kama baba zetu au mama zetu walivyodumu kwenye ndoa
ustaarabu na elimu na democrasia vinasababisha ndoa kuvunjika haraka
wanawake wamekuwa wabishi na hawataki kujishusha kama mama zetu
na sisi wanaume bado tunajiona ni waafrica na tunataka wake zetu wajishushe kitu ambacho hakiwezekani
 
Bado najiuliza tatizo ni nini tofauti na wazee wetu wao wamefanikiwa kutulia kwenye ndoa zao mpaka katika umri wao huu wa uzee

ubepari na utandawazi sababu kubwa

hivi sasa vijana ni wabinafsi sana,hamna uvumilivu,maadili(desturi) pembeni,imani za kidini za mashaka
 
tatizo la siku hizi ni kwamba watu wengi wanapenda kuiga kuishi maisha wanayoona watu wanaishi kwenye tamthilia wazoziona kwenye luninga.......hamna kabisa upendo wa dhati pamoja kuheshimiana katika ndoa.
 
wa2 wanapend cna kula bata na kupombeka.starehe zimezid then chambi hakuna,ndo mwanzo wa usaliti.c unajua starehe gharama.
 
tatizo wanaume mnafungua sana hizo zipu zenu hamjali kama mmeoa wala nini, na kinachowapa kiburi ni kuamini kuwa kwa kuwa umeoa basi hata ufanyaje mkeo hawezi kukuacha,bt its unfortunately wanawake wa hivyo hawapo tena kwenye jamii yetu, wanawake wa sasa ni dot com zaidi, hawawezi maisha walioshi mama zetu,wewe kama unajiona bado unahitaji kufungua sana hiyo zipu yako usikimbilie kuoa maana na wewe utaingia kwenye hiyo list ya marafiki zako

in blue napingana na wewe...
in red uko sahihi, watoto wa kike mnafikiri ndoa ni matarumbeta ndio maana huwa mnalazimisha sana hiyo kitu wakati katika hali halisi huwa hamko tayari kukabiliana na changamoto ya maisha ya ndoa!!nyie mda wote macho juu juu tu!
kumbuka mwanamke ndiye anayejenga/kubomoa nyumba kwa mikono yake mwenyewe, natumai umenipata Nailyne....
 
huu msemo wa mwanamke anajenga au kubomoa nyumba yake mwenyewe kwa kweli siupendi sijui kwa nini.ndoa ni kushirikiana wote wawili,na mwanamume pia anaweza kuijenga au kuibomoa nyumba yake.wangapi huwaacha wake zao,wakaenda kwengine kukawa moto,wakaona bora mke wake wa zamani
 
Mimi nionavyo ndoa nyingi hazidumu siku hizi kwa sababu za maamuzi ya Beijing, Mafahari wawili hawakai zizi moja , Mabmbo mengi siku hizi watu huiga bila kufikiria kwa undani matokeo ya baadae , haraka haraka na kuiga mambo ya utandawazi ndicho kilicho tufikisha hapo. bado vijijini sehemu nyingi wanafuata mila haya tunayo yaongea ndoa zinadumu tuige huko.
 
wengi wanaamua kuingia kwenye ndoa kutoka na misukumo iiyokuwa ya maana kama
  1. mimba
  2. msukumo wa wazazi
  3. kuiga kisa marafikize au nduguze kaoa au kuolewa
matokeo yake akiingia anakuwa
  1. hajui nini maana ya ndoa
  2. hakujiandaa au kuandaliwa kuishi na mwenza
  3. haelewi abcd ya ndoa
  4. anaishi maisha ya kuigiza au kujilaumu kwa kuwa yawezekana hakukuta kama alivyotarajia
 
Back
Top Bottom