Kwa nini ripoti ya Mukama isiwe batili kama haimtaji Kikwete kuwa ndiye tatizo! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa nini ripoti ya Mukama isiwe batili kama haimtaji Kikwete kuwa ndiye tatizo!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kingcobra, May 1, 2011.

 1. Kingcobra

  Kingcobra JF-Expert Member

  #1
  May 1, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,008
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  Ashakumu siyo matusi waswahili walisema ''kujamba ajambe mkubwa kosa linaelekezwa kwa mtoto''. Huu msemo ndiyo uliotumiwa na kamati ya Mukama na wenzie waliotwishwa mzigo na Mwenyekiti wa Chama Kukichunguza chama anachokiongoza yeye mwenyewe. Ni jambo la kustaajabisha kwamba ripoti yote yenye kurasa zaidi ya mia haimtaji kwa namna yoyote ile kikwete kuwa ndiye kinara wa vurugu ndani ya chama. Chini ya uongozi wa kikwete chama na serikali vimepoteza integrity mbele ya jamii. Hata hao wanaoitwa magamba ndani ya chama walikaribishwa na kuenziwa na kikwete mwenyewe. Mimi nadhani akina mukama hawajaandika tu kwenye rpoti lakini mioyoni mwao wanatambua kwamba gamba kubwa na gumu ambalo ilikuwa ni muhimu livuliwe pia ni kikwete. Wameacha kuandika hivyo kwa sababu ndiye aliyewatuma na wasingekubali kuacha kumtumikia kafiri wakakosa mkate wao.
   
Loading...