Kwanini Rais Samia Hakuongea na Watanzania Wanaoishi Marekani?

HansMaja

Senior Member
Nov 9, 2010
102
114
Tulitarajia kwamba Rais Samia takutana na Watanzania wanaoishi Marekani kwenye ukumbi, lakini hili halikufanyika. Kuna sababu zozote zilizotajwa kwa Rais kutokutana na Diaspora na kujibu baadhi ya maswali tuliyo nayo?
 
Hana cha kuongea. Na si ajabu angepata watu wachache sana na kwenye issue ya uDC ambayo wao wanataka kutoa special status angeishia kuzomewa tu kwani DIASPORA kwa asilimia kubwa hawataki kusikia huo upuuzi hasa ukitilia maanani Nchi nyingi za Africa zinaruhusu uDC zikiwemo Kenya, Uganda na Rwanda.
 
Tulitarajia kwamba Rais Samia takutana na Watanzania wanaoishi Marekani kwenye ukumbi, lakini hili halikufanyika. Kuna sababu zozote zilizotajwa kwa Rais kutokutana na Diaspora na kujibu baadhi ya maswali tuliyo nayo?
Huenda ni Yale mabango waliyoanza kumwonesha Hotelini alihisi yangemuandama kwenye hilo kutaniko na Wa-tz..
 
Alinusa mchezo, chawa wake walimtonya kuhusu Diaspora kuja na mabango ya kupinga sera zake za kuibatiza Tz kama nchi ya kigaidi.
 
Ataongea nini na diaspora.

Wale wanajielewa, mabeberu yamewacivilize hawana ushamba tulionao vijana wa kwa mtogole.

Jamani mnaosema rais ametuheshimisha, mjisemee nyie binafsi kwamba "rais ameniheshimisha"
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom