Kwa nini rahisi nje na si ndani?

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,955
22,136
Kwa nini rahisi nje na si ndani?



Je, unajitahidi kuhakikisha mume au mke wako awe anakusikiliza?
Je, unahisi hakusikilizi na hana response kwa kila kile unataka kuongea naye?
Je, ukitaka kuwasiliana naye unajikuta hana muda na wewe au ndoa imekuwa kimya kizito kinachotisha na umefika mahali unajiuliza hivi kwa nini tunaishi watu wawili tofauti kiasi hiki.

Je, unajua kwamba sasa tunaishi kwenye ulimwengu unaoshangaza sana, just one click unaweza kuwasiliana na mtu yeyote duniani bila kujali yupo bara gani, nchi gani, mkoa gani au wilaya gani huduma nyingi ni bure na pia unaweza kuwa na options kama hutaki ku-click unaweza kupiga simu, unaweza ku-beep, unaweza kutumia FEDEX au DHL kuhakikisha unawasiliana na mtu yeyote mahali popote.

Kitu kinachoshangaza zaidi ni kwamba katika ulimwengu wa sasa suala la mawasiliano kati ya mke na mume yanazidi kuwa magumu kuliko mke au mume kuwasiliana na ulimwengu wa nje.

Hata hivyo tunafahamu kwamba ulimwengu wa sasa haupo kwenye industrial age bali information and technology age ambapo information huweza kusambaa kila pande bila tatizo hata hivyo lazima tufahamu kwamba mawasiliano kwa ajili ya information ni tofauti na mawasiliano ambayo ni PERSONAL
Kuwasiliana na partner wako ni mawasiliano ambayo ni personal yaani two souls together wakati mawasiliano na wengine nje ya mke wako au mume wako ni kwa information.

Mawasiliano ni indicator ya failure au success ya ndoa hivyo ni vizuri kujiuliza je unawasiliana vipi na mke wako au mume wako ukilinganisha na wengine zaidi yake.

Kuna wanandoa wawili bila kujua walikuwa wanamtindo wa kutumiana email kwanza kwa kawaida baadae wakaja kufikia hatua ya kuwa closer zaidi na kuamua kufanya mpango wakutane ili waweze kufahamiana zaidi, wakakubaliana wakutane kituo cha train usiku na kweli wakakutana na kwa kuwa kila mmoja alikuwa very excited hawakuwa makini sana kuchunguzana sana sura hata hivyo baada ya maongezi wote wakajikuta wanaelekea mtaa mmoja katika hilo jiji na baadae block moja apartment moja, nyumba mmoja, mtoto wao mmoja na zaidi kumbe ni mke na mume bila kujua.

Kumbe aliyekuwa haongei naye nyumbani ndiye yule aliyekuwa anaongea naye kwa love and romantic wote wakifika kazini.
Jambo la msingi huwezi kuwasiliana na mke au mume kwa email kama ndiyo njia pekee ya kujenga mawasiliano, unahitaji kusikia sauti yake na pia kumuona anapoongea hata kwa machozi uweze kumfuta au mpangusa, unahitaji kusikia kile anaongea kwa sauti nna kile haongei pia unahitaji kumsikiliza kila anaongea kwa moyo kitu ambacho email au technolojia zingine haziwezi isipokuwa kuwa live na mke au mume kwa furaha, upendo na kicheko.

Jiulize kwa nini wakati wa uchumba au mwanzo wa ndoa ukiwa na mume wako au mke wako ile akichezesha jicho tu ulikuwa unaweza kufahamu anataka kuongea kitu gani na sasa mkiwa wawili ni kimya hadi aje mgeni na akiondoka anawaacha mabubu.

Kumbuka mmeamua kuishi pamoja kwa hiari yenu hakuna aliyewalazimisha hivyo anza kuwasiliana kama pale mwanzo ili ndoa yenu iwe ya kuridhisha .
NB:
Wise men talk because they have something to say; fools, because they have to say something

4MORE
MBILINYI.BLOGSPOT.COM
 
Back
Top Bottom