Elections 2010 Kwa nini Picha za Mgombea Urais wa CHADEMA Dr.Slaa na wabunge hazionekani?

Mpendanchi-2

JF-Expert Member
Apr 4, 2009
304
37
Katika pita pita yangu sijaona matangazo wala picha za Mgombea urais wa CHADEMA na Wabunge wa Chadema kwenye Bango lolote!!! Si mijini wala vijijini.

Chadema imekuwaje kwani, maana watu wa mjini at least wanafahamu maana ya mgombea urais Dr. Slaa na CHADEMA , je huko vijijini kwenye watu wengi itakuwaje!! Kama tatizo ni pesa itisheni harambee tuchangie ili picha na majina ya wagombea ubunge yatangazwe kwa nguvu kama CCM anavyofanya.
 
wazo zuri..
ccm waliwaburuta waendesha baiskeli na pikipiki na kuwaburuta wananchi kwenye malori lakini watz walijaa wenyewe kwenye mkutano wa chadema bila kupewa lifti au kupewa pilau..........watz wamejua ukweli na ukweli siku zote ndio utakaotuweka huru........
 
hhuenda anazo chache,maana kuna maeneo machache nimeona hizo picha za wagombea wa CHADEMA.kama eneo ninaloishi zilibandikwa ila kwa sasa wameondoa zote naona hii ni kampeni ya vijana ccm kuondoa hizi picha za DR.
 
Katika pita pita yangu sijaona matangazo wala picha za Mgombea urais wa CHADEMA na Wabunge wa Chadema kwenye Bango lolote!!! Si mijini wala vijijini.

Chadema imekuwaje kwani, maana watu wa mjini at least wanafahamu maana ya mgombea urais Dr. Slaa na CHADEMA , je huko vijijini kwenye watu wengi itakuwaje!! Kama tatizo ni pesa itisheni harambee tuchangie ili picha na majina ya wagombea ubunge yatangazwe kwa nguvu kama CCM anavyofanya.

Wazo zuri, nadhani haya mabango kuna sehemu nyingine ni muhimu sana...
 
Kweli hata mimi hilo limenishangaza! Kama ni swala la pesa, ni bora tuchangishane mapema. Andika " CHADEMA" halafu tuma 15710 upate kuchangia ewe mzalendo. Mimi nilidhani labda ni tactics, yaani wanangoja wachoke picha za mafisadi ili waweke za wazalendo. Kama hawataweka kabisa itakuwa mbaya kikampeni.
 
Si kwamba picha hazipo zipo ila kutokana na wingi wa picha za CCM zinakuwa kama hazipo, hii ni kutokana na CCM kutumia bil.2 kwa picha tu ikisaidiwa na pesa za serikali.
SLAA.jpg
 
Si kwamba picha hazipo zipo ila kutokana na wingi wa picha za CCM zinakuwa kama hazipo, hii ni kutokana na CCM kutumia bil.2 kwa picha tu ikisaidiwa na pesa za serikali.
SLAA.jpg

Sijui maeneo mengine lakini kwa Dar es salaam nimezunguka sana, sijakutana na picha kabisa, labda niamini kwamba zikiwekwa kuna vijana ma Agent wa mafisadi wanazibandua!!!
 
Pamoja na kuchanwa au kuondolewa nafikiri Chadema hawana picha nyingi, zitawekwa last wiki watu watakapokuwa wamechoka kuona rangi ya kijani tuu wakiona rangi tofauti moja hata ndani ya picha 100 za kijani lazima watataka wajue ni nani, ni sawa na doa moja jekundu kwenye shati jeupe huonekana zaidi.
 
Katika pita pita yangu sijaona matangazo wala picha za Mgombea urais wa CHADEMA na Wabunge wa Chadema kwenye Bango lolote!!! Si mijini wala vijijini.

Chadema imekuwaje kwani, maana watu wa mjini at least wanafahamu maana ya mgombea urais Dr. Slaa na CHADEMA , je huko vijijini kwenye watu wengi itakuwaje!! Kama tatizo ni pesa itisheni harambee tuchangie ili picha na majina ya wagombea ubunge yatangazwe kwa nguvu kama CCM anavyofanya.
Usibabaishwe na wingi wa mabango!! Bango moja la Chadema lina nguvu kuliko mabango 400 ya ccm.
 
si kwamba picha hazipo zipo ila kutokana na wingi wa picha za ccm zinakuwa kama hazipo, hii ni kutokana na ccm kutumia bil.2 kwa picha tu ikisaidiwa na pesa za serikali.
slaa.jpg

tena kumbuka kuwa hawakulipia kodi
 
CCM imetumia pesa za serikali kufanyia kampeni, imeyumbisha utendaji wa serikali nzima ,
na hapa Mwanza mfano wameweka mabango kibao, watu wakiona hizo picha huishia kufyonza, na kumtusi mgombea wao wa urais, kweli nawaambia, kama hamuamini jaribuni kuchunguza sura za watu wanapokaribia mabango ya Kikwete, watu wanamchukia sana, ndo maana Mbeya walimzomea.
 
Chema chajiuza kibaya chajitembeza. Hii inaweza ikawa dalili ya jinsi vipaumbele vya nchi vitakavyokuwa pindi watu watakapoingia madarakani. Je effectiveness ya kutumia mabilioni kujitangaza,tena dar kwa mabango lukuki iko wapi? kuna wamama wanaovaa viatu vya laki mbili na kupaka lipstick ya sh 50,000 tshs huku watoto wana kwashakoo!
 
Katika pita pita yangu sijaona matangazo wala picha za Mgombea urais wa CHADEMA na Wabunge wa Chadema kwenye Bango lolote!!! Si mijini wala vijijini.

Chadema imekuwaje kwani, maana watu wa mjini at least wanafahamu maana ya mgombea urais Dr. Slaa na CHADEMA , je huko vijijini kwenye watu wengi itakuwaje!! Kama tatizo ni pesa itisheni harambee tuchangie ili picha na majina ya wagombea ubunge yatangazwe kwa nguvu kama CCM anavyofanya.

Kila nikiona Bango lenye maandishi: Chagua Chama Cha Mafisadi
Chagua Fisadi

NAPATA KINYAA.

Kwa ufupi ni kwamba hayo mabango hayana mvuto, hata wao wanajua.
 
siku hizi dhambi inayonikabili ni kutukana kila bango la ccm ninaloliona, im sorry lakini ni ukweli.
 
Kizuri chajiuza kibaya chajitembeza.mungu ibariki tanzania ijiondoe katika minyororo ya utumwa wa mafisadi,wala rushwa wezi ccm
katika pita pita yangu sijaona matangazo wala picha za mgombea urais wa chadema na wabunge wa chadema kwenye bango lolote!!! Si mijini wala vijijini.

chadema imekuwaje kwani, maana watu wa mjini at least wanafahamu maana ya mgombea urais dr. Slaa na chadema , je huko vijijini kwenye watu wengi itakuwaje!! Kama tatizo ni pesa itisheni harambee tuchangie ili picha na majina ya wagombea ubunge yatangazwe kwa nguvu kama ccm anavyofanya.
 
Mungu yupo nyuma na mbele ya watanzania wapenda mabadiliko hata bila mabango dr.atashinda tu mungu aliamuru usiibe ccm wameiba pesa za wananchi kwa kutengenezea picha hakika ni dhambi hukumu yao inanukia
 
Nafikiri suala la kubanduliwa kwa mabango ya CHADEMA yaweza kuwa kweli, maana siku chache zilizopita nilikutana na vijana fulani waliovalia Ki-CCM wanaongea wenyewe kuwa wanaenda kuondoa mabango ya CHADEMA na kuweka za kwao na hamna mtu atakayewauliza hata mmoja.
Na mimi nilishindwa kuwaongelesha kwani hata hivyo walikuwa wawili na wameshiba kiasi! ilibidi ninyamaze tu,wakaendelea na sfari yao.
 
Back
Top Bottom