Kwa Nini Performance ya Wizara Itegemee Zaidi Waziri Aliyepo na Siyo Watendaji??

Gosbertgoodluck

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
2,856
401
Wakuu,
Nimeamua kuchokoza hii mada ili kupata mawazo ya wachambuzi wa mambo. Hivi karibu, rais jk aliteua baraza jipya la mawaziri lenye sura mpya na za zamani zilizozoeleka. Katika mawaziri ambao uteuzi wake ulipokelewa kwa shangwe na vifijo alikuwa John Pombe Magufuri aliyereshwa kwenye Wizara ya Ujenzi. Cheche zake tayari zimeshamchoma Chief wa Tanroad. Tayari ameondolewa. Wakandarasi wenye ofisi kwenye mabegi yao ya mkononi nao wametahadharishwa kwamba waanze kufungasha vilago. Ndani ya siku chache tu za kuingia ofisini, Mhe. Magufuri ameshafanya kazi ambazo waziri aliyepita zilimshinda.

Ninachojiuliza ni je, kwa nini perfomanle ya wizara itegemea kwa kiwango kikubwa usharp wa waziri mwenyewe badala ya kutegemea uwezo wa watendaji waliopo wizarani?
 
bump!
 
Mind you Magufuli kwa utendaji wake wa kazi sioni kama ana act kama Waziri but as Katibu Mkuu sababu naona kwenye Wizara zetu katibu mkuu wa Wizara ndio mara nyingi anafanya mambo mengi kwenye Wizara
 
Hapa mkuu umenena. Ndio maana madudu ni mengi.

Ila cha msaingi ni kwamba mawaziri wertu hawajui mipaka ya kazi zao. Kimsingi hawa wanapaswa kuwa watungaji na wasimamiaji wa utekelezaji wa Sera na wala sio wenyewe kuwa watekelezaji wake.

Sasa katika mgongano wa kimaslahi ndipo unapomkuta waziri anaingilia mpaka majukumu ya makatibu wakuu na hivyo kuwafanya wao kuwa kama midoli maofisini. Kwa hiyo unapompata wazziri makini wa kusimamia sera na kuachia watendaje wafanye sawasawa na mikataba yao ya kazi hapo ndipo pananoga.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom