Kwa nini nimuite rais wakati sikushiriki kumchagua? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa nini nimuite rais wakati sikushiriki kumchagua?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by kichenchele, Jul 8, 2010.

 1. k

  kichenchele JF-Expert Member

  #1
  Jul 8, 2010
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 490
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Wanaa JF, hebu nifahamisheni, nitamuitaje mgombea urais kama atachaguliwa wakati mimi binafsi sikushiriki kumpa kula yangu?
   
 2. doup

  doup JF-Expert Member

  #2
  Jul 8, 2010
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 1,123
  Likes Received: 296
  Trophy Points: 180
  kwa sababu tu tumejiwekea utaratibu katika chaguzi kwamba atakayeshinda ndie ataitwa hivyo "RAiS, Mbunge,M'kiti,.....nk" na wengi wape!!!

  Ingekuwaje kama ungetawaliwa na mfalme/malkia ambao ujirithisha tu!!???
   
 3. W

  WildCard JF-Expert Member

  #3
  Jul 8, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,469
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Anayelala kwa mama ndiye baba! Kama unabisha, muulize mama. Sio wewe tu ambaye unakuwa haukumchagua. JK alichaguliwa na watu kama milioni 10 hivi. Watanzania tunakaribia milioni 40 sasa.
   
 4. k

  kichenchele JF-Expert Member

  #4
  Jul 8, 2010
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 490
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Wildcard, mimi kichenchele sikubaliani na wewe hata kidogo unaposema anayelala kwa mama ndiye baba, ninapata shida kutambuwa upeo wako na ufahamu juu ya kudadafua mambo mazito, unatoa light answers to very logical questions, ina maana hata wewe enzi unalala na mama yako ukiwa mdogo ulikuwa unasitahili kuitwa baba?
   
 5. W

  WildCard JF-Expert Member

  #5
  Jul 8, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,469
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Umeshasema enzi nikiwa mdogo, nanyonya. Sasa hivi siwezi hata kufikiria kurudi kulala kule. Angalia pia na upande wa pili wa maelezo yangu bila jazba.
   
 6. Bramo

  Bramo JF Bronze Member

  #6
  Jul 8, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 9,227
  Likes Received: 2,160
  Trophy Points: 280
  Kimsingi JK sio Rais wangu mimi coz sikumchagua,hata yeye mwenyewe analijua hilo na thats why hata akipigaga kampeni huwataka wana CCM wamchague na sio Wa Tanzania...so in practise kama hukumchagua sio RAIS wako...
  Note..
  ni Kura na sio Kula
   
 7. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #7
  Jul 8, 2010
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,821
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Hamna jina lingine la kumuita hata kama hukumchagua..
  So ni ngumu lakini hatuna jinsi ndie Rais..
   
 8. W

  WildCard JF-Expert Member

  #8
  Jul 8, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,469
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Ni Rais wa JMT. Rais wetu sote. Tuliomchagua, ambao mlichagua wengine na ambao hawakupiga kura kwa sababu moja au nyingine.
   
 9. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #9
  Jul 8, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 21,271
  Likes Received: 3,946
  Trophy Points: 280
  Kwa sababu
  1)Alishinda uchaguzi kwa mujibu wa katiba:frusty:
  2)Alikula kiapo kwa mujibu wa imani yake:A S 39:
   
 10. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #10
  Jul 8, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,533
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Hujirithisha:A S tongue:
   
 11. Da Womanizer

  Da Womanizer JF-Expert Member

  #11
  Jul 8, 2010
  Joined: May 24, 2010
  Messages: 1,562
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Nadhani tatizo ni upeo wako. Yaani unataka kusema ulipokuwa mdogo ulikuwa "UNALALA" na mama yako!!!!!!!!!!??????????
   
 12. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #12
  Jul 9, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,631
  Likes Received: 1,662
  Trophy Points: 280
  'Urais' ni cheo ambacho kinapatikana kwa kutimiza masharti na taratibu kadhaa za kikatiba na kisheria. 'Kupigiwa kura ya ndio na kila mwananchi/raia' sio sharti mojawapo la kuwa rais.
   
 13. b

  blackpepper JF-Expert Member

  #13
  Jul 9, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 382
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  basi mwite rais wa waliomchagua
   
 14. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #14
  Jul 9, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,409
  Likes Received: 1,725
  Trophy Points: 280
  Ungemwita vivyo hivyo!!!
   
 15. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #15
  Jul 9, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,409
  Likes Received: 1,725
  Trophy Points: 280
  Naomba usome katiba ya nchi! Kuna kiwango au asilimia ya kufikiwa ili kuwa rais.
   
 16. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #16
  Jul 9, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,409
  Likes Received: 1,725
  Trophy Points: 280
  Si wote wenye vigezo vya kupiga kura, mfano umri chini ya miaka 18 hawapigi kura.
   
 17. mzamifu

  mzamifu JF-Expert Member

  #17
  Jul 12, 2010
  Joined: Mar 10, 2010
  Messages: 3,256
  Likes Received: 704
  Trophy Points: 280
  Utamwita rais kwa kuwa ndilo jina lake jipya na kazi yake mpya. Kwani watu unaowaita kwa majina yao ulishiriki kuwapa hayo majina? Rais ni wajibu, kazi madaraka/mamlaka juu ya watu, na vyote vinaambatana na heshima fulani
   
 18. Abunwasi

  Abunwasi JF-Expert Member

  #18
  Jul 12, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 2,680
  Likes Received: 712
  Trophy Points: 280
  A ROSE BY ANY OTHER NAME REMAINS JUST AS SWEET
  Call him anything thing you want but he will still be your president[you will pay his salary and other emoulments and take care of his well being for the duration of his tenure

  WASWAHILI WANASEMA 'WENGI WAPE' na "MKATAA WENGI MCHAWI'
   
Loading...