Kwa nini ni wachaga...? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa nini ni wachaga...?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bowbow, Nov 7, 2008.

 1. Bowbow

  Bowbow JF-Expert Member

  #1
  Nov 7, 2008
  Joined: Oct 20, 2007
  Messages: 545
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  WanaJF

  Hapo siku za nyuma kulikua na topic ndefu sana kuhusu ukabila na makabila mengi yalichambuliwa kwa kila namna lakini bado hakuweza kupatikana muafaka kwamba nani ni mkabila.

  Lengo la mada hii sio kurudia maelezo yaliyotolewa kwenye ile mada iliyopita, la hasha ni kutaka kuchambua dhana nzima KWA NINI TUNAFIKIRI WACHAGA NI WAKABILA????. Sio kabila lingine Please

  Maswali ninayo jiuliza na nadhani ndio iwe guidance ya mada yetu ni haya:

  1. Ukabila ni nini na lini na wapi ukabila Umeanzia???
  2. Ni lini tulianza kufikiria Wachaga ni wakabila??????

  3. Ni nini kiashirio kwamba kabila fulani ni wakabila????

  4. Je ukabila ni tabia ya mtu ama kikundi cha watu?????

  5. Ni vipimo gani tunavyotumia kuelezea, kupima na hata kuendeleza ukabila ?????

  6. Je ukabila ni kitu ambacho ni endelevu(sustainable)????

  7. Je kuna faida na hasara gani ((kwa wachaga na kwa wasio wachaga ) kuwa mkabila???

  [B]NOTE[/B] Sio lazima uchangie hii mada kama hutaweza kujibu kwa hoja bila jazba. Ni bora hata wachangie watu 10 kitu chenye maana kuliko 100 wenye jazba.

  Nimeshawishika kutoa hoja hii baada ya kuona kuna harufu sio nzuri kwenye mmojawapo ya mjadala unaoendelea hivi sasa.

  Karibuni kwa maoni,

  Mimi ni chotara wa kichaga nahitaji kuelimishwa kwenye hili na sina jazba,
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Nov 7, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  so basically unataka tuwajadili wachagga.. na siyo kabila jingine.. why don't we just jadili "Ukabila" na badala yake wachagga? Miye nimetoa posa Uchaggani so najitoa kwenye mjadala na mtu yeyote aliyoa, kuchumbia, au mwenye damu ya kichagga should the same.. na mtu yeyote aliye na rafiki mchagga pia.. well anybody who knows a mchagga should recuse him/herself..
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Nov 7, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,818
  Likes Received: 83,217
  Trophy Points: 280
  Wachaga kwa maoni yangu hawana ukabila bali ni watu ambao wanajua kuhangaika ama kuhakikisha wanapata elimu nzuri au kibiashara. Wachaga hawajalemaa kwa kubakia mkoani kwao tu wamesambaa Tanzania nzima na huko wengi wao wanafanya biashara ambazo nyingi zimeshamiri mno. Wachaga pia wamefumbuka macho mapema kuhusu CCM kuliko kabila jingine lolote ndiyo maana Kilimanjaro chama cha mafisadi hakioni ndani Kilimanjaro.

  Sababu kubwa ya CCM kutaka CHADEMA ionekane kama ni chama cha Wachaga ni kwamba CHADEMA ndiyo tishio kubwa la CCM hivyo wakishawapakazia kwamba ni chama cha wachaga basi hawatapata kura za wananchi wengine na hivyo kuihakikishia CCM kuendelea kupeta, lakini hili la CHADEMA kuwa ni chama cha wachaga bado haliingii akilini miongoni mwa Watanzania walio wengi ndiyo maana CHADEMA ikaweza kuwabwaga tena CCM huko TARIME.

  Mbeya nako wanaanza kufunguka macho kuhusu CCM hali ikiendelea hivi na CCM kuanza kupoteza chaguzi mkoani humo Wanyakyusa nao wataambiwa wana ukabila, divide and conquer.
   
 4. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #4
  Nov 7, 2008
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Heshima yako MKJJ,
  najua utakuja tena ukiwa na lundo la utetezi, tunakujua jinsi ulivyo na utetezi biased kwa hawa ndugu zetu.na hata kama umetoa posa haina mantiki yoyote kusema kuwa umejitoa na kuwataka na wengine wenye maslahi fulani fulani na chagaz kujitoa kuboresha thread hii.jitoe kwenye mjadala wewe kama wewe.unajua kuna watu wengi mnaoamini kuwa kuwa wale wanaosema chagaz wana ukabila labda ni chuki, wivu au husda.lakini ukweli ni kuwa kuna baadhi ya vitu viko wazi sana wala huitaji kuwa na elimu kiasi gani kuvitambua kwamba vinafanywa kwa misingi ya ubaguzi wa kikabila.Binafsi sina chuki wala wivu na chagaz lakini kuna baadhi ya mambo ambayo huwa sikubaliani nayo kutokana na kuendekeza huo uchagaz.
   
 5. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #5
  Nov 7, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Hapa tena tunarudia kosa la kuangalia kabila kama vile ni kitu kimoja. Hauwezi kusema wachaga wako hivi au vile kwa sababu ndani ya hilo kabila kuna watu walio tofauti kabisa. Wako wanaoendekeza ukabila na wako wanaopinga ukabila. Ninawajua wahaya ambao hawakubali mhaya kuoa au kuolewa na asiye mhaya. Ninawajua wahaya ambao wako tayari kuolewa na au kuoa mtu yeyote yule isipokuwa mhaya mwenzao. Ninawajua wahaya ambao wao ndio hawajali kabisa kabila au rangi ya mtu. Wote hawa ni wachaga. Naamini ni hivyo hivyo kwa wachaga. Ni sisi tunaotaka kuhukumu jamii nzima kutokana na vitendo vya watu wachache katika kabila hilo ndio wakabila!
   
 6. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #6
  Nov 7, 2008
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Si vibaya kujadili Wachagga peke yao ila kama ulivyoonesha hapo juu itakuwa vigumu kidogo.

  Kwanza nadhani tuangalie haya mambo kwa mapana yake.
  1. Kuna ukabila unaokuja kwa sababu jamii fulani inataka kujilinda dhidi ya mambo hatari inayofanyiwa na jamii nyingine ambazo zinawazunguka. Mfano mzuri ni Wahindi. Je hawa nao ni wakabila? Kama kabila linajiona linaweza kumezwa, suala la kuwa na mikakati ya wazi (formal) au isiyo wazi haliepukiki.
  2. Ukabila mwingine unasababishwa na nguvu toka nje. Mfano mzuri ni kuwa baada ya uhuru Serikali ya Mwalimu iliamua kuyawekea vikwazo baadhi ya makabila kwa sababu Nyerere mwenyewe aliyaona kama hatari kwa utawala wake kwa sababu makabila hayo yalikuwa yamepiga hatua sana. Ninayo mifano mingi sana ila mmojawapo ni kuweka idadi ya wanafunzi waliochaguliwa kuingia sekondari toka baadhi ya maeneo. Kuna sehemu mwanafunzi mwenye alama 60/150 alipata nafasi wakati sehemu nyingine mwenye 80/150 alikosa. Ingawa ilikuwa hatua muhimu kuendeleza maeneo yaliyokuwa nyuma, ila sidhani kama unatakiwa kukwamisha watu wengine ili wenzao wanyanyuliwe!
  3. Sababu za kihistoria na mazingira yetu pia zinachangia. Kwa watu ambao wameshapata nafasi ya kwenda nje ya nchi, watakubaliana nami kuwa mtu unajisikia furaha sana kukutana na MTz na hata Mkenya au Mganda. Hii pia ni sawa kama mnakutana Dar na mtu unayetoka naye kijiji kimoja. Hapa tunahitaji sheria nzuri tu kuhakikisha tunapunguza upendeleo kwenye kugawana keki ya nchi na kuwajibishana tunapokosea badala ya kuendelea kufanya makosa ya kuwapiga watu mihuri kuwa ni wakabila.
  4. Kwa kuwa sasa tuna mwingiliano mkubwa kuliko ilivyowahi kutokea huko nyuma, sina shaka kwamba tuna vizazi vichache sana ambavyo vitakuwa vinaongelea ukabila. Jukumu letu ni kuwapa mazingira ya kukabiliana na upendeleo wa aina yoyote badala ya kuendekeza upuuzi unaofanywa na watawala wetu wa kuingiza mambo ya ukanda/mikoa na kabila katika utawala wa nchi yetu.
   
 7. K

  Kithuku JF-Expert Member

  #7
  Nov 7, 2008
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Ukiuliza ama ukitafiti kuhusu ukabila ama dhana yoyote ile hakikisha hao unaowauliza wanamaanisha kilekile wanaposema "ukabila". Nitakupa mifano. Kuna watu wakikuta idara fulani ya serikali au kampuni kuna wachaga wengi wanalalamika ukabila, lakini wakikuta "shoe-shiners" wengi pia ni wachaga, hapo ati si ukabila! Wakikuta viwanja vya kujengea nyumba vimegawiwa sehemu fulani na wengi waliovipata ni wachaga watu wanalalamika ukabila, lakini wakikuta wauzaji wengi wa "kitimoto" ni wachaga pia, ati hapo si ukabila! Wakikuta wanafunzi wengi walioingia university mwaka huu ni wachaga watalalamika ukabila, lakini wakikuta miongoni mwa watu wanaohangaika kuhakikisha wamesomesha watoto wao shule za sekondari hasa za binafsi wengi wao ni wachaga pia, hapo ati si ubinafsi! Wakikuta waliokopa pesa nyingi katika benki na SACCOS na kupewa ni wachaga watasema ukabila, lakini wakisikia pia katika watu wanaofia kwenye ajali za machimbo ya Tanzanite huko Mererani wengi wao ni wachaga pia ati hapo si ukabila!

  Sasa kumbe ukabila ni kitu gani, na hao wachaga wana nini hadi mtu akataka wafuatiliwe kuhusu ukabila?

  Walinzi wengi binafsi huko mijini Dar na kwingineko ni wamasai (zamani ilikuwa wamakonde), nayo ni ukabila pia? Wauza mayai wengi, wale kutoka Ukonga, Kiwalani, Kitunda,wanaopita na misafara ya baiskeli yenye matrei ya mayai yaliyopangwa urefu hadi kumzidi mwendeshaji, wengi wao ni wakurya, ni ukabila pia? Vipi kuhusu wasichana kutoka Iringa wanaofanya kazi ya uyaya Dar, kwa wingi kuliko makabila mengine, ni ukabila?
   
 8. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #8
  Nov 7, 2008
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Mkuu nakubaliana na wewe,,,, hahaaa haaaa
  Na wanasema Wachaga wezi nao ukabila?
   
 9. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #9
  Nov 7, 2008
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Hii kali!
  Mheshimiwa Kithuku umegonga penyewe.
  Sioni discussion hii italeta nini cha ajabu au tofauti na a similar discussion iliyowahi kuanzishwa na MKJJ siku za nyuma.
  Bow wow..labda uonyeshe what is the added value kurudiarudia kitu ambacho kilishawahi kuongelewa kwa marefu na mapana yapata miezi si zaidi ya minne iliyopita.Ingependeza kama ungefanya rejea ya ule mjadala halafu utuambie unataka ku achieve nini.SAMAHANI LAKINI.
   
 10. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #10
  Nov 7, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Kwangu mimi moja ya kigezo kikubwa cha ubaguzi wa kikabila ni ndoa. Hadi leo sijasikia mtu aliyekatazwa kuoa au kuolewa na mchaga kwa vile yeye si mchaga! Kama hawa watu hawaoni taabu kuolewa au kuoa na kuzaa na wasio kabila lao, tutasemaje kuwa wana ukabila?
   
 11. Bowbow

  Bowbow JF-Expert Member

  #11
  Nov 7, 2008
  Joined: Oct 20, 2007
  Messages: 545
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Thanks BAK,

  So wachaga sio wakabila bali ni siasa chafu tu ya kuwapakazia
   
 12. Bowbow

  Bowbow JF-Expert Member

  #12
  Nov 7, 2008
  Joined: Oct 20, 2007
  Messages: 545
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mwanakikjiji

  Sababu ya kuleta hii mada ni kuona ukweli uko wapi kwa hawa ndugu zetu

  Je ni kweli niwakabila ama ni propaganda tu ndio maana sijataka kuzungumzia
  wahaya, wanyakyusa ama wasukuma. Tukishajiridhisha ndio tuongelee hayo mengine
   
 13. Bowbow

  Bowbow JF-Expert Member

  #13
  Nov 7, 2008
  Joined: Oct 20, 2007
  Messages: 545
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Fundi uko right,

  ndio maana kuna haya maswali soma moja baada ya jingine so ni kama unajaribu kujibu swali number 4.

  Maswali ninayo jiuliza na nadhani ndio iwe guidance ya mada yetu ni haya:

  1. Ukabila ni nini na lini na wapi ukabila Umeanzia???
  2. Ni lini tulianza kufikiria Wachaga ni wakabila??????

  3. Ni nini kiashirio kwamba kabila fulani ni wakabila????

  4. Je ukabila ni tabia ya mtu ama kikundi cha watu?????

  5. Ni vipimo gani tunavyotumia kuelezea, kupima na hata kuendeleza ukabila ?????

  6. Je ukabila ni kitu ambacho ni endelevu(sustainable)????

  7. Je kuna faida na hasara gani ((kwa wachaga na kwa wasio wachaga ) kuwa mkabila???
   
 14. M

  MpiganajiNambaMoja Member

  #14
  Nov 7, 2008
  Joined: Sep 20, 2007
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ukabila ni pale ambapo mtu anakosa kupewa kitu fulani kwa sababu si kabila fulani. Kwa mfano unaomba kazi unaambiwa kuwa vigezo vya elimu na ujuzi unavyo lakini kwa sababu si kabila fulani huwezi kupata kazi.

  Nijuavyo mimi Tanzania hakuna ukabila kabisa kabisa. Ila hili swala la ukabila linakuzwa tu na baadhi ya viongozi wenye malengo yao kisiasa au kibiashara. Wote tunasoma shule aina moja, tunafanya kazi na watu wa makabila tofauti, tuna fursa sawa katika kila kitu bila kujali kabila. Kwanza hata huwa hatuulizani makabila. Utakubaliana na mimi unaweza kusoma au kufanya kazi na watu fulani hata hujui makabila yao kwa miaka mingi tu.

  Swala la networking katika maswala ya kazi na shughuli nyingine za kijamii liko kila mahali. Hata huku ughaibuni swala la networking pia lipo. Networking hizo zinaweza kuwa za kirafiki, kikabila au kidini kutegemeana na makundi yanayowakutanisha pamoja. Ndo maana unaweza ukawa unatafuta kazi au msaada kutoka shirika au kampuni flani, then ndugu au rafiki yako (bia kujali kabila) anakwambia ahh pale nina rafiki yangu anafanya kazi pale, ananyanyua simu, anampigia anakupa kimemo ukienda mambo yakuwa mswano. Huu sio ukabila ila ni networking, iko kila mahali na huwezi kuizuia. Ndo maana hata vyuoni au makazini kunakuwaga na networking events. Social activities kama michezo, kunywa bia bar n.k zote ni some kind of networking ambayo inafanya ujuane na watu. Its open for anybody bila kujali kabila.

  Zamani kidogo wakati nafanya kazi Tanzania ilitokea kwenye kitengo changu ambacho mimi nilikuwa mkubwa, chenye watu wa 5 watu 3 tulikuwa tunatoka mkoa mmoja. Na sikujua hilo hadi jamaa wa kwanza alipoleta maombi ya likizo akionyesha anaenda mkoa ninaotoka, ndo nikamuuliza kumbe tulikuwa kabila moja. hii ilikuwa baada ya mwaka. lakini nafasi zote 3 zilitangazwa kwenye gazeti na wao ndo wakapatikana. So sometimes mambo kama hayo yanatokea bila kupangwa.

  Ni vyema tu watanzania tukaishi kwa amani na kusaidiana bila kujali ukabila na udini.
   
 15. Bowbow

  Bowbow JF-Expert Member

  #15
  Nov 7, 2008
  Joined: Oct 20, 2007
  Messages: 545
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mkuu heshima mbele

  naona now tunaelekea maana tunaanza kuujadili huoja UKABILA NI NINI na ni KIPIMO gani tutumie tuseme huo ni ukabila.

  Mimi ni mchaga sitopenda kutake side nitamoderate tu hii topic
   
 16. Bowbow

  Bowbow JF-Expert Member

  #16
  Nov 7, 2008
  Joined: Oct 20, 2007
  Messages: 545
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  WOS,

  Nakushukuru kwa comment.

  Kwenye ile thread ilikua inazumza ukabila kwa maana ya sehemu za kazi TRA, IKULU, UDSM ni kwengineko zikatolewa hoja mbali mbali. Of all hoja imezidi kuibuka kwenye siasa na hata miongoni mwetu kwamba WACHAGA specifically ni wakabila. So nimeamua kunarrow down the topic na kuchukua specific case kuona hicho kinachoitwa ukabila nini?, ni tabia ya kikundi ama ni tabia ya mtu binafsi_? Inapimwa vipi, inarisishwa vipi kutoka one generation to another??? n.k
  Hope nimeiweka clear hii hoja zaidi
   
 17. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #17
  Nov 7, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mimi nadhani Wachagga wamedraw attention sana sababu zao za kuhangaika kutafuta pesa na kuheshimu chochote wanachopata!
  Sababu nyingine ambao wachagga wanapata attention sana ni pale mwenzi wa kumi na mbili wanaposafiri kuelekea Kilimanjaro kwa madai ya kuhesabiwa!
  Ukweli utabaki pale pale kwamba kati ya watu wanaojituma sana hapa nchini ni Wachagga na tabia zao za kupendeleana hasa watu wa huko.
  Kwa mfano ukienda mahali ukisema unaitwa Shayo,Mchagga mwenzako atakuuliza swali la kwanzi Shayo wa Rombo?
  Ukikuta sasa ni wa huko basi ni kilugha one way na ajira juu kama ulikuwa unatafuta!
   
 18. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #18
  Nov 7, 2008
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Soetimes unaweza kuta issue sio ukabila bali ni wingi wao na Elimu.
  Mfano huwezi sema wakwele wana ukabila wakati hawfiki ata one mil.
  Wanyakyusa,wahaya na wahaya wamekula shule na wako wako wengi ndo maana wamezagaa kinoma.
  Ila chembe chembe za ukabila zinakuwemo si unajua mwamba ngoma huvutia kwake
   
 19. Bowbow

  Bowbow JF-Expert Member

  #19
  Nov 7, 2008
  Joined: Oct 20, 2007
  Messages: 545
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Nakubalina na wewe.

  wakati nasoma mlimani course niliyosoma tulikuwa wanafunzi 30, kati yao 8 ni wachaga, sina uhakika kama ni ukabila huo. Tulipo maliza zikatangazwa kazi serikalini by then wizara ya Mipango walioajiriwa 5, watatu ni wachaga. Kukaanza fununu ndani ya hiyo ofisi mpaka katibu mkuu akaamua kuunda tume ndogo kuchunguza, conclussion hakuna mchaga hata mmoja aliyeshiriki, wala kuifluence maamuzi ya ajira na walioajiriwa hawakuwa wanamfahamu mtu hata mmoja kwenye ile ofisi.

  Je kwa nini walifiri huo ni ukabila?????

  Note this is a true story
   
 20. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #20
  Nov 7, 2008
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Kithuku;Sina chakuongeza wala kupunguza.
  Mkuu Kithuku mchango mzuri sana kwa maoni yangu umejibu maswali yote yaliyokuwa yakinisumbua kwa muda mrefu.Asente sanaaaaaaaaaaaaa.
   
Loading...