Kwa nini ni Mutalemwa ndiyo ajistaafishe na siyo Mwigulu ndiyo ajiuzulu?

Allen Kilewella

Verified Member
Sep 30, 2011
13,692
2,000
Nimesikia taarifa kwamba Rais John Pombe Magufuli akimshauri Mkurugenzi wa DAWASA Archad Mutalemwa kujistaafisha kwani ni "Mzee" ili awaachie "vijana". Lakini wakati Rais anamshauri Mutalemwa Askari wawili wa Usalama Barabarani waliuawa huko Mkoani Pwani ikiwa ni muendelezo wa mauaji ya watu na Askari kwenye mkoa huo.

Hivi ni mpaka nani auawe ndipo itaonekana Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Mwigulu Nchemba anatakiwa kujiuzulu. Hivi mauaji haya si kiashiria kwamba Waziri naye anatakiwa ajiuzulu ili apewe mtu mwingine mwenye maono tofauti na yeye?
 
conservative3

JF-Expert Member
Nov 12, 2013
1,035
2,000
ww unahisi kati ya waziri na mkurugenzi nani mtendaji?unahisi maono ya mtu mmoja km wazir ndo yanaweza kuokoa janga la mauaji?inawezekana unapambana na proffessional sniper .
 
Allen Kilewella

Verified Member
Sep 30, 2011
13,692
2,000
ww unahisi kati ya waziri na mkurugenzi nani mtendaji?unahisi maono ya mtu mmoja km wazir ndo yanaweza kuokoa janga la mauaji?inawezekana unapambana na proffessional sniper .
Kama mawaziri hawawezi kubadili kitu kwenye wizara wanazoziongoza sasa kwa nini wawepo?
 
conservative3

JF-Expert Member
Nov 12, 2013
1,035
2,000
Kama mawaziri hawawezi kubadili kitu kwenye wizara wanazoziongoza sasa kwa nini wawepo?
waziri ni msimamizi wa sera na sheria kwa ujumla wake ila mkurugenzi ndio mratibu wa utekelezaji.kwenye kubadili mfumo inabidi baraza lote la mawaziri likubaliane unless mfumo unaotaka kuubadili umepewa mamlaka na sheria zinazoongoza nchi na sekta husika.
tukumbuke kuwa kwenye mambo mengi sheria nyingi zinaingiliana ukiondoa zilizotungwa na bungepia kuna baadhi za sheria za bunge zimegongana,mambo mengi kwenye wizara ya mambo ya ndani ni mtambuka,huwezi jiamulia tu km alivyoamua nape
 
Allen Kilewella

Verified Member
Sep 30, 2011
13,692
2,000
waziri ni msimamizi wa sera na sheria kwa ujumla wake ila mkurugenzi ndio mratibu wa utekelezaji.kwenye kubadili mfumo inabidi baraza lote la mawaziri likubaliane unless mfumo unaotaka kuubadili umepewa mamlaka na sheria zinazoongoza nchi na sekta husika.
Wapi nimesema mambo ya kubadili mfumo? Kwani Muhongo alipoambiwa aondoke alikuwa hasimamii sera?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom