Kwa nini ni lazima CHADEMA na CUF wakae pamoja wakubaliane? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa nini ni lazima CHADEMA na CUF wakae pamoja wakubaliane?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Kasheshe, Nov 13, 2010.

 1. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #1
  Nov 13, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Wanabodi,

  Katika bandiko hili naomba niongelee vyama vya kitaifa especially the big 3. Nikimaanisha CHADEMA, CCM na CUF?

  Zanzibar:

  Kama kigezo kingekuwa chama cha kitaifa lazima kiwe kile chenye wabunge wa kuchaguliwa kutoka kwenye visiwa vyote Zanzibar, yaani Unguja na Pemba basi chama halali kuongoza Zanzibar ni CUF na wala sio CCM... in other words CUF ni chama cha kitaifa zaidi Zanzibar kuliko CCM, kwa kuwa CUF kina wawakilishi kutoka Pemba na Unguja!

  Ni kutokana na mtizamo huu, CCM lazima ifanye kazi ya ziada ipate uwakilishi wa kuchaguliwa au iendelee na serikali ya Mseto kwa kuwa CCM haiwezi kuongoza kwa kuwakilishwa na kisiwa kimoja. So unless wafike kwenye hali ya kuweza kuwa na wawakilishi kutoka Pemba, itabidi waendelee na mseto huu milele.

  Tanzania (Muungano):
  Kama kigezo hapo juu cha chama cha kitaifa kingetumika then ni CUF na CCM tu ndio wanastahili kuitwa vyama vya kitafa kwa kuwa na wabunge wa kuchakuguliwa kutoka pande zote za muungano (Zanzibar na Tanzania bara)

  Kwa mtizamo wangu, CHADEMA inastahili aidha kufanya juhudi za ziada kupata uwakilishi wa kuchaguliwa kutoka Zanzibar ama kukaa sahani moja na CUF na hata ikiwezekana kuungana ili kuunda vyama viwili vya kitafa ambavyo ni strong.

  Wenzao CUF wameweza kuondoka kwenye hii changamoto maana kwenye uchaguzi huu wamepata viti bara wakati 2005 hawakuwa navyo.

  Lazima CHADEMA itumie nguvu za ziada kupata uwakilishi wa kupigiwa kura kutoka Zanzibar ama kuungana na CUF kufanya upinzani thabiti.

  ===>Kwa maana hiyo ni CUF tu ndio yenye wawakilishi a.k.a wabunge wa kuchaguliwa kutoka Zanzibar (Unguja na Pemba) na Tanzania bara. CHADEMA na CCM you have home work to do! Kwa kuwa upande wa CCM na CUF wamefanya via maridhiano. Nadhani CHADEMA na CUF kama kambi ya Upinzani need to work together.
   
 2. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #2
  Nov 13, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Una maana gani unaposema chama cha kitaifa unajua ukubwa wa Tanzania ulivyo, kama unaishi Zanzibar jaribu siku moja utembelee Tanzania bara utakuja gundua Pemba yote ni kama wilaya ya kinondoni.
   
 3. T

  Thesi JF-Expert Member

  #3
  Nov 13, 2010
  Joined: Aug 8, 2010
  Messages: 998
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Pemba iwepo isiwepo bado taifa la Tanzania lipo. Zanzibar ni sehemu ndogo sana ya Tanzani hivo hata chama kisipopata uwakilishi huko haijalishi. Huko pemba mbunge anachaguliwa kwa kura 4000 huku bara ni kura elf 40 hivo Pemba au Unguja si hoja. Hata chama kisipopata kura huko kikifanya vizuri bara bado mwerere. Upo hapo!
   
 4. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #4
  Nov 13, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  Siyo lazima kwa sababu CUF hawana mikakati inayoeleweka.
   
 5. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #5
  Nov 13, 2010
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Kinondono ni kubwa mno. Ukiingia na Doza D8 (greda) ndani ya masaa 6 kunakua hakuna kisiwa, inakua bahari tu, Kinasambaza na D8 moja tu
   
 6. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #6
  Nov 13, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  kwa vile wote ni wanyama wa kazi je punda huweza kufungwa na ng'ombe wakalime?
   
 7. f

  fundimchundo Senior Member

  #7
  Nov 14, 2010
  Joined: Jul 23, 2010
  Messages: 150
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Wataalam wa siasa mtusaidie kufafanua. CCM na CUF wana makubaliano ya kutawala kwa ushirika. Maalim Seif ni Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar. Januari Makamba alimlalamikia Jussa kuhusu Prof. Lipumba kumshambulia Jakaya Kikwete huko Mbeya wakati wa kampeni KINYUME cha muafaka wa CCM na CUF. Bungeni Dodoma CUF wamepiga kura za Spika wakiwa upande wa CCM (same block).
  SWALI LANGU NI HILI;
  CUF NI CHAMA CHA UPINZANI AU NI CHAMA TAWALA-MWENZA?
   
 8. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #8
  Nov 14, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,533
  Trophy Points: 280
  Kasheshe, ukisema ni lazima, maana yake ni must, ili kitu kiwe ni lazima, kunakuwepo shuruti la ama sheria, tatatibu na kanuni. Kama Chadema wangeshindwa kufikia idadi ya viti kwa mujibu wa kanuni, hapo ndipo hoja ya ulazima ingekuwepo.
  Kwa vile Chadema imetimiza matakwa ya kikanuni kuiruhusu kuunda kambi rasmi ya upinzani Bungeni, then hakuna ulazima wa kushirikiana na yeyote, bali kuna umuhimu kushirikiana na CUF bara na wapinzani wengine. Kwa lugha nyingine its not a must but it is important.
   
 9. mpenda

  mpenda JF-Expert Member

  #9
  Nov 14, 2010
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 250
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Analysis yako si nzuri. wapiga kura wooote wa majimbo ya pemba hawafikii idadi ya wapiga kura wa jimbo la ubungo, hivo usilete ubabaishaji. anyways who the hell cares about pemba/unguja?? nshawahi kufika mikoa zaidi ya 10 na hata nje ya nchi but sijawahi kufika huko zenj, who cares??
   
Loading...