Kwa nini ni lazima CCM iangushwe katika uchaguzi wa mwaka 2015 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa nini ni lazima CCM iangushwe katika uchaguzi wa mwaka 2015

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mechard Rwizile, Jan 24, 2012.

 1. m

  mechard Rwizile JF-Expert Member

  #1
  Jan 24, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 937
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 80
  Watanzania kwa muda wa miaka zaidi ya ishirini baada ya uhuru walielewa kuwa uongozi wao ulitokana na wao wenyewe. Viongozi walikuwa ni sehemu yao kwa kila jambo. Kwa mfano; watoto wote walisoma shule za aina moja na kupata huduma sawa bila ya kujali vyeo vya baba na mama zao.Walipata matibabu katika hospitali zile zile na hadi mwishoni mwa miaka ya themanini kila aliyeugua alipata dawa sitahiki kutoka katika mfumo uliokuwepo. Ninakumbuka nilikuwa na matatizo ya miguu mwaka 1977, niliandikiwa rufaa kwenda hospitali ya Bugando nikitokea Arusha. Niliandaliwa safari na Mwl. Mkuu wa shule yangu ya Ilboru kama ambavyo angekuwa anamuandalia mwanae. Hakutumia fedha zake ila za walipa kodi zilizokuwa zinaletwa na serikali mashuleni. Nilipomaliza masomo ya kidato cha nne, nilienda kukaa nyumbani nikisubiri kupangiwa kazi. Muda ulipotimia niletewa barua ya kupangiwa kazi na kupokelewa kama ilivyopangwa bila ya kukutana na kubembeleza mtu yeyote. Katika mazingira kama haya, ni kwanini mtu asiuamini uongozi uliopo madarakani?

  Watu watakimbilia kusema kuwa wasomi walikuwa wachache kulinganisha na wasomi wa leo, ni kweli. Na kweli tupu. Lakini ukweli mwingine ni kwamba, hakuna eneo tunaweza kusema ajira zilizopo zinatosheleza mahitaji. Hadi mwishoni mwaka 2011, mahitaji wa walimu ni makubwa kuliko walimu waliopo. Tuanhitaji walimu wengi zaidi ya waliopo. Tumeshindwa kuwaajiri wote kwa sababu hatuna fedha ya kuwalipa mishahara na stahili zao. Katika afya, watumishi waliopo ni chini ya asilimia 40% ya mahitaji, Ulinzi na usalama, askari wetu walio na ajira ni chini ya nusu ya mahitaji. Kwa mifano hiyo michache ni dhahiri kuwa wasomi wetu wanahitajika sana leo kama ilivyokuwa zamani.

  Tutapata wapi fedha za kulipa waajiriwa wapya kama tumeuza viwanda vya nguo kwa waliobadili matumizi na kuuza mitambo ya kutengeneza nguo kama vyuma chakavu na kufanya majengo yawe maghala ya bidhaa zilizoagizwa kutoka nje ya nchi? Tutapata wapi fedha za kuwalipa waajiriwa wapya, kama faida inayopatikana kutokana na dhahabu inayochimbwa hapa nchini ni mishahara tu wanyolipwa wazawa wache walioajiriwa na migodi ya dhahabu, kana kwamba dhahabu ghafi sio bidhaa ya kuuza?Yaani haina thamani yeyote! Tutapata wapi fedha kama kila kiongozi anona fahari ya kumiliki mali zisizokuwa na maelezo? Tutapata wapi fedha kama wafanyabiashara wanatanguliza bendera za CCM na sare za kijani kama mbadala wa kulipa kodi? Tutapata wapi fedha za kuwalipa waajiriwa wapya kama viogozi wetu wanajiongezea posho kwa madai ya kuwagawia wapiga kura wao? Orodha ni ndefu.

  CCM haina masikio ya kusikia shida za watu, haoni matatizo ya watu, haina mpango wakutaka kujua matatizo ya msingi ya watu ndio maana wanawagawia wapiga kura kofia za njano, T shirt za kijani na kanga za mchanganyiko wa kijani na manjano. CCM inachosikitisha zaidi ni yale majimbo ya "sera zetu zinakubalika kwa wananchi" wakati wakijua wameiba kura au wamehujumu upigaji wa kura. Maadui wa CCM ni wale wasema ukweli, wapenda haki na usawa, hasa wale ambao uadilifu wao ni wa kuigwa! Hiki ni chama gani sasa?

  2015 ndio mwaka wa ukombozi, kujiandikisha, kupiga kura, kuwashawishi ndugu na jamaa kujiandikisha na kupiga kura na kulinda kura hadi mshindi atakapotanganzwa. CCM wanaweza kuiba na kuhujumu kura zisizozidi milioni tano. Kama mwaka 2015, wapiga kura milioni 25 watajitokeza kupiga kura na kura zikalindwa, hawatakuwa na lao. Hapo ndipo tutakaa chini na kuandika katiba bora ya kututoa hapa tulipo.

  Shime watanzania tutoe mchango wetu katika hili kwa maarifa ya hali ya juu na tuanze sasa. Au mnadhani nisemacho si sahihi?
   
 2. k

  kastarehe JF-Expert Member

  #2
  Jan 24, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 231
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Umenena vyema mkuu!!!!
   
 3. monongo

  monongo JF-Expert Member

  #3
  Jan 24, 2012
  Joined: Oct 25, 2011
  Messages: 370
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  kwa kweli umetoa mawazo mapana sana mkuu,laiti kama wna jaf wangekuwa na mawazo km hayo,wote tungeungana kuwahamasisha wananchi vijijini,na tukafanya maamuzi yalio sahihi tungeweza kufikia lengo hilo.
   
 4. k

  kipinduka Senior Member

  #4
  Jan 24, 2012
  Joined: Nov 11, 2011
  Messages: 130
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  chama gan kinaweza kuwa hata nafuu,kwa cdm mndengeleko kama mi cna nafac hata kama nina cfa,au nihamie kaskazin mwa nchi?
   
 5. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #5
  Jan 24, 2012
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Masaburi yameongea! Endelea kutumiwa kama condom japo indirectly angalau umekiri ccm ime outlive its usefulness!
   
 6. A

  Ame JF-Expert Member

  #6
  Jan 24, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 3,352
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280
  Well said ndugu yangu. Mimi tangu 2009 nilikwisha tamka a decree kuwa Tanzania njema lazima izaliwe na naona mawingu yamefika kiasi cha mkono wa mtu so dont worry hata kama wasipotaka watanzania Tanzania njema lazima izaliwe.
   
 7. m

  mwikumwiku Senior Member

  #7
  Jan 24, 2012
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 153
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Amenena nini Mkuu?
   
 8. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #8
  Jan 24, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Mkuu umenena vema. kazi iliyobakia ni sisi Watanganyika kuhakikisha CCM wanang'oka 2015 lasivyo nchi itakuwa kama Nigeria kwa rushwa
   
 9. Kikarara78

  Kikarara78 JF-Expert Member

  #9
  Jan 24, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,164
  Likes Received: 514
  Trophy Points: 280
  Mechard Rwizile na Wana JF,
  Maelezo ni mazuri, na ni matumaini yangu mwenye macho na masikio ya kusikia na kuona na kusoma ujumbe umefika hata kama hawatasema moja kwa moja. Hakuna lenye mwanzo lisilo na mwisho.
  Mungu ibariki Tanzania
  Nawakilisha   
 10. M

  Maengo JF-Expert Member

  #10
  Jan 25, 2012
  Joined: Jul 7, 2011
  Messages: 280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nina wadogo zangu wawili. Mmoja hakupiga kura kwa sababu alikuwa shule na hakuwa amejiandikisha japo ndo alikuwa ametimiza miaka 18, mwingine hakuwa amefikisha umri! Sasa 2015 naamin wote watapiga kura. Kwa hyo kwenye familia yetu tumeshaongeza vichwa viwili..
   
 11. M

  Maengo JF-Expert Member

  #11
  Jan 25, 2012
  Joined: Jul 7, 2011
  Messages: 280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ccm inapendwa na wazee na wakina mama wakihongwa khanga na mitandio, halafu inachukiwa na vijana! Kufikia 2015 wazee wengi watakuwa wamekufa na vijana wengi watakuwa wametimiza umri wa kupiga kura!
   
 12. W

  We know next JF-Expert Member

  #12
  Jan 25, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 664
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hembu fanyeni mpango basi hii habari iandikwe magazetini kama makala maalum, au front page kama uchambuzi makini. Kwa kweli watanzania wote bila kujali itikadi, inabidi kuisoma hii.
   
 13. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #13
  Jan 25, 2012
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 9,147
  Likes Received: 3,335
  Trophy Points: 280
  Kwa sababu ni chama cha Mafisadi.
   
 14. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #14
  Jan 25, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Ref. To the heading above, Arusha wana usemi kwamba "hiyo sio kitu ya kuuliza!"

  Binafsi naamini hakuna sababu ya ccm kuendelea kututawala! Tunahitaji viongozi na ccm hakuna hata mmoja!
   
 15. I

  Independent Voter JF-Expert Member

  #15
  Jan 25, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 279
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  siasa sampuli hii ndio zinaikosesha chadema kura hasa za watu kama mimi ambao tuko wengi na huwa tunafanya maamuzi kwa kusikiliza sera za chama husika kuelekea uchaguzi,kwa style hii ya siasa mtakua mnapata kura za wanachama wenu tu ambazo hazitoshi!
   
Loading...