Kwa nini ni KLM tu inaua KIA?

mstahiki

JF-Expert Member
Jul 14, 2007
308
5
Kwa nini ni KLM tu ndio inatua KIA?

Ningependa kujua ni kwanini???KLM tu kati ya ndege zote za kimataifa zinazokuja Bongo ndio inayotua KIA?NO BA,Emirates,Swiss and other more
 
Ethiopian pia inatua! Na nyingi chater za uarabuni zinatua! KLM inafanya biashara sana kutokana na kuingia na kutoka watalii wengi nchi za Netherlands n.k. Karibu abiria 300 huingia na kutoka kupitia kia kila inapotua na kupaa! Pia ina connection kubwa na nchi za ulaya na magharibi nafikiri pia ina connection na Northern Airline ambayo hufanya safari zake kati ya ulaya na amerika ya kusini
 
Hii ni destination ya wateja wake wengi ambao wanakuja nchini kutalii na wala si wale wanaotoka Dubai na kwingineko ambao wameenda kufanya biashara. Nature hii ya wateja wao ndo inayowafanya watue pale na imewaletea tija ndo maana wanaendelea nayo.

Infact uwanja wa KIA ungeboreshwa huenda ingekua ni destination ya International airlines nyingi zaidi maana tumeshuhudia watalii wengi wakishukia Jomo Kenyata na kuja Tanzania ambayo ni ongezeko la gharama na risk kwao.
 
holland ndio soko kubwa la maua duniani na kuna mashamba mengi ya maua arusha na kilimanjaro
 
Swiss air hushusha zaidi ya 70 % ya Abiria Nairobi....inapofika Dar huwa tupu, na wakati inarudi hutoka almost tupu Dar na Kujaza abiria Nairobi kwenda nao Zurich
 
hatuwezi kufananisha route ya Nairobi na Dar au Kia kumbukeni Nairobi kuna UNEP offices so so many international figures wana-fly in and out toka Geneva! Na subirini watakapoanza route za US directly watazoa wateja wote!
 
Duh, hapa naona umeingia choo cha kike...
Kiswahili kimekua TZ miaka hii.

Hio sentensi japo umeandika kiswahili lakini sina ninaloelewa.

Back to the topic:

Koninklijke Luchtvaart Maatschappij ni shirika ambalo linajua biashara sana na linatafuta masoko kila sehemu ya dunia.
Kama sio ndege zao lakini hata kuwa washirika na mashirika mengine.
 
Kinacho takiwa kufanywa na na serikali ya CCM (kama wana akili na wakiacha wizi) ni kuboresha KIA iwe na hadhi ya kimataifa kweli. Suala eti kenya wakianza route za moja kwa moja kwenda US watazoa abiria wote hilo halina msingi kwani siyo US pekee inayo leta abiria TZ.

Tatizo ni mipangilio ya CCM na serikali yake ndo wana turudisha nyuma. Fikiria wanataka wajenge international airport bagamoyo! kweli pale bagamoyo kuna nini cha maana mpaka uweke international airport? Kwa nini wasipanue KIA au hata Arusha airport au uwanja wa songwe ukawa na hadi ya kimataifa?
 
Ila kuna fununu kuwa pia mambo ya radar yanachangia, mashirika mengi yanaogopa kutua hapo kwa sababu za kiusalama
 
Kinacho takiwa kufanywa na na serikali ya CCM (kama wana akili na wakiacha wizi) ni kuboresha KIA iwe na hadhi ya kimataifa kweli. Suala eti kenya wakianza route za moja kwa moja kwenda US watazoa abiria wote hilo halina msingi kwani siyo US pekee inayo leta abiria TZ.

Tatizo ni mipangilio ya CCM na serikali yake ndo wana turudisha nyuma. Fikiria wanataka wajenge international airport bagamoyo! kweli pale bagamoyo kuna nini cha maana mpaka uweke international airport? Kwa nini wasipanue KIA au hata Arusha airport au uwanja wa songwe ukawa na hadi ya kimataifa?

Tanzania sio nchi maskini kupindukia ila tu ni ukosefu wa uongozi bora siasa zimezidi vitendo.
porojo nyingi za viongozi.
Tuna rasilimali nyingi ( madini,gesi,mito,maziwa,mbuga za wanyama,milima nk.)na nchi yetu ipo kwenye mojawapo ya maeneo maarufu yenye vivutio vikubwa na maarufu duniani kwa shuguli za utalii lakini ajabu tumeshindwa kutumia vitu vyote hivyo ili kuletea maendeleo tanzania.
Toka uhuru ni misaada tu mpaka tumelemaa kwakuwa watembeza bakuli la misaada,mwishowe wazungu wanatuita matonya .
Na hata misaada ikija inaishia mifukoni mwa kundi la watu fulani
 
Na hili linahusiana vipi na Uwanja wa KIA?
 
Na hili linahusiana vipi na Uwanja wa KIA?

usidokoe, quote the two messages ndo italeta maana, huyu mkuu alikuwa najibu mchango wa mtu mwingine sasa wewe unadakia tu kipengele kimoja.....quote michango yote miwili ndo utajua alikuwa na maana gani. Acha uvivu wa kusoma.
 
Lakini pia KLM ni shirika linaloheshimika na kuaminika, hivyo lina wateja wengi
 
usidokoe, quote the two messages ndo italeta maana, huyu mkuu alikuwa najibu mchango wa mtu mwingine sasa wewe unadakia tu kipengele kimoja.....quote michango yote miwili ndo utajua alikuwa na maana gani. Acha uvivu wa kusoma.
Najua fika kwamba alikunukuu, lakini sijaona nukuu yake kama imeweza kutoa jibu la mada yako juu ya CCM na KIA. KIA ni uwanja wa kimataifa na ulijengwa kama ni uwanja wa kimataifa.

Hoja yako ni kupanua uwanja huo, lakini utapanua vipi uwanja ambao matumizi yake ni madogo? Ukaenda mbali zaidi kwa kusema Arusha Airport ipanuliwe na iwe ya kimataifa, hii ina maana ya kuua KIA. Hapo hapo unashangaa kuwepo na ujenzi wa airport nyingine Bagamoyo!

Ukiangalia lengo la ujenzi wa KIA hapana shaka siwezi kuona umuhimu wa kunukuu mada yako!
 
nilisafiri hivi karibuni toka Amsterdam hadi dar kupitia kilimanjaro(KLM)siku ya kwanza nilikosa connection pale Amsterdam kwa sababu ndege ilijaa sana walitumia Airbus-200 abiria 327,nilipata next flight Airbus-300 abiria 427 nayo ni full na captain aliposema sasa tunatua kilimanjaro airport kulikuwa na shangwe kubwa sana ndani ya ndege..kati ya watu 427 about 380 walishuka hapo KIA ni route maarufu sana lakini kioja ni unapotua kili yenyewe mmh tunahitaji marekebisho makubwa sana ili ifanane na zile shangwe za watalii!!!!!!kibunango tukibisha tu kila kitu haipendezi something must be done kuokoa ule uwanja though we actually need 2nd strategy kwenye utalii ambayo ita-concentrate mikoa mingine ili mzunguko wa hela TZ uwe fair sio kila siku kibosho na Arusha>>>!!!
 
usidokoe, quote the two messages ndo italeta maana, huyu mkuu alikuwa najibu mchango wa mtu mwingine sasa wewe unadakia tu kipengele kimoja.....quote michango yote miwili ndo utajua alikuwa na maana gani. Acha uvivu wa kusoma.

mkuu Magezi nakushukuru kwa kunielewa,huyu jamaa anayebisha tumwache abishe abakie na giza ktk akili yake sababu mtu asiyekubali kujifunza kutoka kwa wenzake sio mwerevu wa akili
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom