Kwanini ngozi yako haina mvuto?Mambo 5 ya kufanya uwe na ngozi nyororo nila kutumia vipodozi

Dr. Zaganza

JF-Expert Member
Jul 15, 2014
1,195
1,661
Cha kwanza niwafahamisheni kuwa , kuanzie leo ondoa mawazo yako kuwa ili uwe na ngozi yenye afya ni lazima uwe na vipodozi vingi.Bali baadhi ya vipdozi havipendani na vingine, ukazidi haribu ngozi yako.

WhatsApp Image 2021-01-17 at 19.31.05.jpeg


Leo nakupa mambo 5 ya kuzingatia, hata ukitumia mafuta aina moja tu, utakuwa na ngozi yenye afya

1: Mazoezi
Ngozi inapumua kupitia vinyweleo, inahitaji jasho lipite. Kama shughuli zako Ni za kukaa muda mrefu, au Una usafiri,tembelea hata ndugu na jamaa wikiend kwa mguu
moja ya faida ya mazoezi inafanya ngozi kukaza na mikunjo kuondoka, kwa hiyo weka ratiba fupi japo ndani kwako ya mazoezi,

WhatsApp Image 2021-01-17 at 19.32.02.jpeg
WhatsApp Image 2021-01-17 at 19.32.02 (1).jpeg




2. Ulaji wa matunda na mboga mboga kwa wingi

Vitamin zote zinazohitajika kwa afya ya ngozi zipo kwenye matunda ikiwemo vitamin E. Kwa hiyo hata mafuta ya ngozi au lotion yanaongezewa vitamin E kwa kuwa Kuna uhaba wa vitamin E kwenye Ngozi yako. Pia tahadhari ya vitamin E Kuna wanaokunywa vidonge ili kupata matokeo ya haraka ya ngozi na nywele ndefu ,bila kujua athari za baadaye za kunywa vitamin E.Ni rahisi mtu anayeishi shamba kuwa na ngozi nyororo kushinda wa mjini,kwa sababu wa mjini,muda mwingi,hula vitu vya sukari kama lamba lamba n.k
Kwa hiyo 2021 weka ratiba ya tunda kwa siku

WhatsApp Image 2021-01-17 at 19.34.23.jpeg


3. Kunywa maji ya kutosha

Kama hunywi maji ya kutosha, Ngozi hufanya makunyanzi na michirizi.Kunywa maji ya kutosha hufanya ngozi ing'are kwa rangi yake ya asili
Wataalam wametuwekea muongozo wa kiasi cha maji mwili unahitaji kwa masaa 24. Note: Usinywe kwa mara moja, kunywa glass moja, baadaye glass tena,baadaye glass n.k.Maji hurahisisha kutoa sumu nje ya mwili kupitia kibofu (mkojo)
Ukishindwa ratiba ya maji: weka glass 8 za maji kwenye chupa moja , na kila asubuh uwe unajaza tena ukiwa umwemaliza ya jana

WhatsApp Image 2021-01-17 at 19.35.13.jpeg


4. Kupumzika ikiwemo kupata usingizi wa kutosha

Kukosa usingizi Mara kwa Mara hushusha Kinga ya mwili, hivyo Ngozi huzeeka mapema.
Mchana tukifanya kazi, damu ambayo inabeba lishe zote kama vitain E, protin n.k inakuwa iko busy kuhudumia maeneo muhimu ya mwili kama ubongo,ini,mapafu,moyo wenyewe,macho,misuli ya miguu,mikono n.k
Unapoala, damu inakuwa haina kazi nyingi, inaenda maeneo yalosahaulika mchana ikiwemo ngozi. Kadri unavyopuzika vya kutosha,unaipa nafasi ngozi yako kusambaziwa lishe na damu,hivyo inng;ara(glow).
Mnawajua wale mabint wanaowekwa ndani kabla hawajaolewa,tunawaita wali? wakitoka ngozi zao inakuwaje?
kama una ugonjwa wa kukosa usingizi, jitibu kwanza. Laa sivyo,utapoteza pesa nyingi kwa kununua cosmetics bila kupata matokeo chanya.

WhatsApp Image 2021-01-17 at 19.35.52.jpeg


5. Kutumia mafuta na vipodozi asilia

Hivi ni vipodozi unaweza andaa hata ukiwa nyumbani mfano kwa kukamua Nazi n.k
Kwa kuwa tayari ngozi nyingi zishatoka kwenye unyoro,tunahitaji kuzirudisha kwwa njia asilia ili kuipa ngozi kinga,kisha yenyewe itairudisha ngozi unyororo

Kwa upande wetu, Natural Skin Solution, Tumeandaa online clinic kwa ajili ya kuwasaidia watanzania kuwa na ngozi na nywele zenye afya. Wasiliana nasi kwa kupiga au whatsapp namba 0713-039 875 kupata ushauri bure na tiba asilia kwa changamoto yoyote ya ngozi na nywele.
 
Ushauri mzuri sana,utashangaa bonge la mtu,kitambi kule,maji hunywi ya kutosha,hana zoezi hata moja halafu analalamika chunusi zinanisumbua kweli 😂 😂 😂...
 
Ushauri mzuri sana,utashangaa bonge la mtu,kitambi kule,maji hunywi ya kutosha,hana zoezi hata moja halafu analalamika chunusi zinanisumbua kweli 😂 😂 😂...
Ungejua chanzo cha baadhi ya chunusi usingesema!

Hormonal acne kwa mfano unadhani kunywa maji ni tiba?.
 
Back
Top Bottom