Kwa nini ngome za wapinzani ziko zaidi mijini na katika vyuo vikuu?

Mike Scofield

Senior Member
Dec 10, 2013
137
0
Tukea siasa za upinzani zianze hapa TZ tunaona wanashindwa kupanua ngome zao ndani ya nchi ili wawe na uhakika wa kuchukua dola. Sasa hivi CDM kama ilivyo kuwa NCCR Mageuzi hapo nyuma tunaona storia kama inajirudia.
Ni lipi wafanye ili kupanua wigo la mtandao wao? Naona hata chama tawala kama vile kimeshindwa kinaridhika na kuwaachia wapinzani maeneo ya mijini na kung'ang'ania vijijini kuliko na idadi kubwa zaidi ya wapiga kura.
Je, Upinzani unao uwezo au nafasi ya kujipanga na kupanua wigo wao hadi ngome kuu ya CCM - vijijini kwa muda huu uliobaki kabla ya 2015?
 
ndesamburo kwek

Senior Member
Aug 1, 2011
136
0
tukea siasa za upinzani zianze hapa tz tunaona wanashindwa kupanua ngome zao ndani ya nchi ili wawe na uhakika wa kuchukua dola. Sasa hivi cdm kama ilivyo kuwa nccr mageuzi hapo nyuma tunaona storia kama inajirudia.
Ni lipi wafanye ili kupanua wigo la mtandao wao? Naona hata chama tawala kama vile kimeshindwa kinaridhika na kuwaachia wapinzani maeneo ya mijini na kung'ang'ania vijijini kuliko na idadi kubwa zaidi ya wapiga kura.
Je, upinzani unao uwezo au nafasi ya kujipanga na kupanua wigo wao hadi ngome kuu ya ccm - vijijini kwa muda huu uliobaki kabla ya 2015?

ukweli unabaki palepale kuwa mijini uelewa wa kinachoendelea uko juu tofauti na vijijini ambako umaskini na ujinga viko juu na chama tawala kina-take advantage hiyo.
 
Adimu

JF-Expert Member
Aug 22, 2013
597
250
Mjini kuna watu wengi walioelimika na wanaojua madudu ya hao mafisadi, ila bush ni mambumbumbu na wengine wanajua mpaka leo nyerere ndo raisi
 
MWEEN

JF-Expert Member
Feb 6, 2010
482
250
Tukea siasa za upinzani zianze hapa TZ tunaona wanashindwa kupanua ngome zao ndani ya nchi ili wawe na uhakika wa kuchukua dola. Sasa hivi CDM kama ilivyo kuwa NCCR Mageuzi hapo nyuma tunaona storia kama inajirudia.
Ni lipi wafanye ili kupanua wigo la mtandao wao? Naona hata chama tawala kama vile kimeshindwa kinaridhika na kuwaachia wapinzani maeneo ya mijini na kung'ang'ania vijijini kuliko na idadi kubwa zaidi ya wapiga kura.
Je, Upinzani unao uwezo au nafasi ya kujipanga na kupanua wigo wao hadi ngome kuu ya CCM - vijijini kwa muda huu uliobaki kabla ya 2015?

Ndugu yangu, unafuatilia siasa za kimataifa?? Kama ndio, fuatilia siasa za Thailand ambako kuna kambi mbili hasimu zinazojulikana kama "Red Shirt" na "Yellow Shirt". Profiles za wafuasi wa kambi hizi ni tofauti na zinafuatana na jinsi CCM na Upinzani zimegawana Vijijini/kiwango kidogo cha elimu na Mijini/ Wasomi respectively.

Sasa hivi kuna maandamano na migomo ya Yellow shirts ambao ni wapinzani. Red shirt ambao ni watawala wanajaribu kutetea msimamo wao na inawezekana uchaguzi mpya ukaitishwa na Waziri mkuu. Hana wasiwasi kwani Yellow shirts ni wachache japo ndio wasomi na wenye pesa.

Vilevile fuatilia siasa za Venezuela utaelewa.

Upinzani una kazi sana kuwashinda CCM japo inawezekana. Hii migogoro inayojitokeza sasa kwenye kambi za upinzani haitasaidia kuchukua dola. Inazidi kudidimiza nafasi finyu waliyo nayo ya kuongeza viti bungeni.
 
Luqash

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
916
195
ukweli unabaki palepale kuwa mijini uelewa wa kinachoendelea uko juu tofauti na vijijini ambako umaskini na ujinga viko juu na chama tawala kina-take advantage hiyo.

Sasa na upinzani si unatakiwa ulione hilo? Badala ya kung'ang'ania mijini kwenye uelewa, kwa nini wasitumie resources zao kuwaondoa ujinga hao wa vijijini?
 
KING COBRA

JF-Expert Member
Nov 10, 2011
2,782
1,225
Tukea siasa za upinzani zianze hapa TZ tunaona wanashindwa kupanua ngome zao ndani ya nchi ili wawe na uhakika wa kuchukua dola. Sasa hivi CDM kama ilivyo kuwa NCCR Mageuzi hapo nyuma tunaona storia kama inajirudia.
Ni lipi wafanye ili kupanua wigo la mtandao wao? Naona hata chama tawala kama vile kimeshindwa kinaridhika na kuwaachia wapinzani maeneo ya mijini na kung'ang'ania vijijini kuliko na idadi kubwa zaidi ya wapiga kura.
Je, Upinzani unao uwezo au nafasi ya kujipanga na kupanua wigo wao hadi ngome kuu ya CCM - vijijini kwa muda huu uliobaki kabla ya 2015?
unapopindua nchi una anza na miji mikuu
 
kapuyanga mkware

JF-Expert Member
Nov 16, 2013
589
0
Sasa na upinzani si unatakiwa ulione hilo? Badala ya kung'ang'ania mijini kwenye uelewa, kwa nini wasitumie resources zao kuwaondoa ujinga hao wa vijijini?

ccm wametumia miaka hamsini na mbili na resourses za taifa kuwafundisha wananchi wa bush umbumbumbu. Itakichukua CDM kama miaka miwili kuondoa huo ujinga halafu ndio waanze kuwaelimisha
 
kambuzi

New Member
Feb 19, 2013
4
0
Vijijini asilimia kubwa hawana elimu,pili hawana muda wa kufutilia mambo muhimu,sanasana wao wanachofuatilia ni mbolea na mbegu.Ndiyo maana mara nyingi hutishiwa kuwa mkichagua chama kingine kutakuwa na vita,au hudanganywa kwa kupewa vihela kidogo tu,t-shirt,kofia,kanga,pombe,nyama n.k na wao kuridhika tu.
 
Shim

New Member
Dec 15, 2013
4
0
Tukea siasa za upinzani zianze hapa TZ tunaona wanashindwa kupanua ngome zao ndani ya nchi ili wawe na uhakika wa kuchukua dola. Sasa hivi CDM kama ilivyo kuwa NCCR Mageuzi hapo nyuma tunaona storia kama inajirudia.
Ni lipi wafanye ili kupanua wigo la mtandao wao? Naona hata chama tawala kama vile kimeshindwa kinaridhika na kuwaachia wapinzani maeneo ya mijini na kung'ang'ania vijijini kuliko na idadi kubwa zaidi ya wapiga kura.
Je, Upinzani unao uwezo au nafasi ya kujipanga na kupanua wigo wao hadi ngome kuu ya CCM - vijijini kwa muda huu uliobaki kabla ya 2015?

nguvu nyingine ya ziada inahitajika kuongezwa huko vijijini,ili wananchi waendelee kujitambua,kwani kontena lenye division zero limejaa huko...
 
Mshiiri

JF-Expert Member
Jun 16, 2008
2,014
1,500
Hili ni swali la msingi. Wako mjini kwa kuwa ni wanamageuzi "fake" na waoga wa maisha so they want to be employed in politics. Hawatatusaidia siku za usoni hawa na wala hawatofautiani na waliopo. Wote walewale. True revolution starts from the village man!!
 
Lokissa

JF-Expert Member
Nov 20, 2010
7,447
2,000
wenye kujtambua wako mijini zaidi
vijijini wakihongwa kanga na pilau unapata kura zao
wao wamerighika kuishi nyumba za tembe na kudanganywa maisha bora
 
Ben T

JF-Expert Member
Sep 18, 2013
245
500
Ni kashifa,matusi na kejeli kubwa kuwa ambia watu wa Vijijini kuwa hawajitambui, hivi mtu anaezalisha chakula cha kula ww mtu wa Mjini hajitambui huyo? Tuache kashifa tena nashangaa sana ikiwa mtu asiye na uhakika wa kupata milo mitatu kwa siku ana mcheka mtu wa Kijijini kwa mambo ya kisiasa?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom