Boramaisha
JF-Expert Member
- Apr 29, 2009
- 820
- 18
Wenye ueledi wa jambo hili tunaomba watufahamishe. Nimekuwa nikiwasikia NEC wakitaja matokeo ya urais na mwisho wanataja nafasi za wagombea watatu wa kwanza kwa misingi ya majimbo badala ya idadi ya kura na kwa hali hiyo Dk. Slaa anatangazwa kwamba ameshika nafasi ya tatu badala ya kuwa nafasi ya pili kutokana na wingi wa kura. Je jambo hilo ni sahihi ama ni mbinu tu za makusudi za kutotaka kumpa "Kaisari yaliyo ya Kaisari?'