Elections 2010 Kwa nini NEC isiwe na database ya matokeo kwa kila kituo??

kanyagio

JF-Expert Member
Dec 10, 2009
1,021
365
mimi nimekaa najiuliza: hivi kwa nini tume ya uchaguzi - NEC isiwe na database (benki ya taarifa) ya uchaguzi kwa vituo vyote kwa ajili ya transparency na future reference. Mimi siyo mtaalamu wa computer, lakini naamini NEC inaweza kabisa kuwa na database matokeo ya diwani, mbunge na rais.. Uwepo wa database hii utasaidia sana kwa kila mtanzania kujua katika vituo 52,000 vya kupigia kura- kila mgombea kapata nini. tena ukiwa na interactive database inaweza kumwezesha mtu ku-generate reports mbalimbali e.g. kura za CHADEMA au CCM kwa kila kata, wilaya au hata kituo. hii itaongeza transparency.. aidha database hii inaweza kutumiwa na vyama kuona ni maeneo gani wamefanya vizuri na wapi wamefanya vibaya.. na hatimaye kutengeneza mikakati kwa chaguzi zinazokuja!!

jambo la pili, kwa nini compilation ya kura isiwe inafanyika electronically-- hii itapunguza muda wa kutangaza matokeo na pia kupunguza uchakachuaji (kama kutakuwa hakuna IT intruders). Nina mfano wa project moja ya tathmini ya magonjwa ya mifugo katika nchi ya jirani,. katika project hii walichofanya ni kuwa na database kila wilaya ambapo project hii ipo na pia wana central database.. Waganga wa mifugo waliopo vijijini wanakuwa na uwezo wa kutuma SMS kupitia simu zao za mikononi; yaani unatuma message kwa kufuata mfumo huu:- jina la kituo:number ya ng'ombe wagonjwa:namba ya ng'ombe waliokufa: idadi ya ng'ombe waliofanyia post-morterm (mfano Boko:40:5:3); kwenye database basi taarifa inapokelewa na kuhifadhiwa na kuthaminiwa,,. kama umekosea jinsi ya kuandika message, unapata message nyingine ambayo inaeleza makosa uliyofanya.

sasa kwa nini NEC isingekuja na utaratibu kama huu; yaani unakuwa na database katika kila jimbo then central database makao makuu ya NEC (unachofanya ni kuhakikisha kuna high security na mechanism nyingine ya kukabiliana na wizi kupitia IT). kwa utaratibu msimamizi wa kituo anatuma SMS kwenda database iliyopo makao makuu ya jimbo. then msimamizi wa jimbo anatangaza matokeo ya udiwani, mbunge na rais katika ngazi ya jimbo. then taarifa za zinaenda Central database iliyopo NEC kwa ajili ya (i) kwanza taarifa (kwa upande wa madiwani na mbunge) na (ii) pili kufanya compilation ya matokeo ya uraisi. Aidha wakati huo huo wasimamizi wa kila kituo na jimbo wabandike matokeo katika kituo na jimbo ili kila mwananchi ayaone na akitaka aweze kuingia kwenye database na kulinganisha. wasimamizi wanaweza kuwasilisha other documentations kwa msimamizi wa jimbo later

faida ya mfumo huu ni hizi:

  1. kwanza inawezekana kwa sababu simu za mkononi zimetapakaa nchi nzima (labda maeneo machache)
  2. itapunguza muda wa kutoa matokeo
  3. itapunguza wizi wa kura katika ngazi mbalimbali
  4. itapunguza gharama
  5. itafanya mfumo wa utangazaji kuwa decentralized
OMBI: napendekeza serikali pamoja na UNDP wahakikishe mfumo huu unatumika.. tunaweza kuanza kwa majaribio katika uchaguzi wa serikali za mitaa kwa baadhi ya sehemu kama pilot...Then in 2015 iwe full swing!!!

wananchi hapo mnasemaji
 
NIKITU AMBOCHO KINAWEZEKANA, TENA KWA WATAALAMU WA HAPA HAPA KWETU;

unajua nilishanga niliposikia teknologia iliyakuwa inatumiwa na kulalamikiwa na NEC kumbe ni MS Excel.!!!!!!!?????
vichekesho, maandalizi yote haya bado wanatumia excel.

Naamini Kusambaza computer ktk kila kituo na kuzi-link, hiyo ingekuwa ngumu lakini wangeweza hata kutumia simu za mkononi- kwa kutumia USSD; teknologia inayo tumiwa na makampuni ya simu Mfano: kuongeza muda wa hewani, kuona balance, M-Pesa,Tigo-Pesa, Z-pesa, N.k...

Naamini mitandao ya simu sasa ipo kila maahari, japo umakini utajika katika kuhakikisha matokeo yanayotumwa ni hakika na ni yametoka katika kituo husika.

Hapo watu mnaweza kukaa kwenye screen kubwa mkifuatilia hesabu utafikiri unasubiri Jackpot , roho mkononi kwani namuber zitakuwa zinapanda na kushuka kadri vituo vinavyotuma matokeo.

Diwani,Mbunge na Hata Rais wanaweza wakawa wanapata instant messages kadri mambo yanavyo endelea
 
Doup hapo umenena.,. natamani NEC wawatumie wataalamu wetu wa IT kutengeneza system!!

ila kuna uwezekano mkubwa wa NEC na wahusika wengine wanafurahia loopholes zilizopo!!... watendaji wa serikali (taasisis mbalimbali) walipinga computerization kwa sababu ilikuwa inazida mianya ya wizi wa fedha za umma. sasa inaweza kuwa mchezo uleule kwa NEC
 
hiyo ni idea nzuri sana.I have been thinking in the same area.

Wachina wameishatuibia vya kutosha. tuwatumie hao hao. watutengenezee touch devices 52000 (1 for each kituo cha kupigia kura) hiyo screen wewe unapuch ur voting card number then unapata picha za wagombea udiwani. unamchagua wako then inakuletea wagombea ubunge same thing until raisi.

to make it effective hizo devices ziwe zinasupport upto 4G. waongee with each mobile network ili data zitumwe to regonal centers n central command. hakuna mtu kuweka mkono wala nini. verification features zitakuwa reasonable n itacheki 4 errors on its own.

Ican guarantee u presidential results in 3 hours from closing of all polling stations nationwide.

dedicated servers can be used na mambo mengine kibao kiasi kwamba hata wazime umeme haitasaidia wala wabanie network connection itakula kwao. TATIZO NEC WATASEMA ITS TOO COMPLICATED N WE CANT AFFORD. ila wanatumia ma land cruiser.
 
ndio mujuwe kuwa hakuna demokrasi, wanajuwa dhahiri kuwa hayo mambo yanawezekana lakini kwa kuwa hakuna uaminifu ndio maana wanachakachua tu basi
 
Mbona Mkileta Hizi Systems Mtawakamata Kirahisi Sana na Leo Hii Tusingekuwa na Hii Discussions. Kukiwa na Loop Holes Kama Masanduku na Vituo Hewa na Poor Security na Kutokurusiwa kwa Waakilishi Kutoka Upinzani Wakati wa Kuhesa Kura ni Ushindi CCM Miaka Yote. Funds Wanazotumia Kuandaa Uchaguzi Hazipelekwi kwa Ajili ya Kununulia Machine au New System ila Kuwalipa Usalama wa Taifa, Wanaosimamia Vituo vya Kupigia Kura, Wanajeshi wa Ngazi za Juu na Vijana Wanajua Kuchekecha Kura Kwenye Computer. Hii Ndio Election Budget Guys Ilipokwenda na Nani Atauliza? This is the same Reason Why We don't Have National ID au Some Type of Social Security System in Tanzania. CCM na Mafisadi Wao Wanajua Very Well Loop Holes Kwenye System Work All the Time. Thats Why Africa is a Disaster to do Any Kind of Investments? Go CCM ... GO CCM GO... Tutaona Mwisho Wenu!
 
[Wachina wameishatuibia vya kutosha. tuwatumie hao hao. watutengenezee touch devices 52000 (1 for each kituo cha kupigia kura) hiyo screen wewe unapuch ur voting card number then unapata picha za wagombea udiwani. unamchagua wako then inakuletea wagombea ubunge same thing until raisi.

to make it effective hizo devices ziwe zinasupport upto 4G. waongee with each mobile network ili data zitumwe to regonal centers n central command. hakuna mtu kuweka mkono wala nini. verification features zitakuwa reasonable n itacheki 4 errors on its own.

Ican guarantee u presidential results in 3 hours from closing of all polling stations nationwide.

dedicated servers can be used na mambo mengine kibao kiasi kwamba hata wazime umeme haitasaidia wala wabanie network connection itakula kwao. TATIZO NEC WATASEMA ITS TOO COMPLICATED N WE CANT AFFORD. ila wanatumia ma land cruiser.]
Mkuu nimefurahishwa sana na mchango wako hapo juu. Kumbe ni kweli inawezekana hata kupiga kura kwa kutumia simu bila hata ya kuchafuana vidole na mpigaji akiwa popote anaweza piga kura bila ya uwezekano wa kurudia yaanikupiga zaidi ya mara moja kwani program itagundua udanganyifu na kugoma kusajili kura ya marudio. Tatizo hapa ni corrupt government system ambayo inafahamu kwa kina possibility hii na unafuu wake lakini wanaukumbatia utaratibu huu wa karne ya 20 ili kufanikisha uhaini wao. Kama program hii ingetumika, sasa hivi
 
[Wachina wameishatuibia vya kutosha. tuwatumie hao hao. watutengenezee touch devices 52000 (1 for each kituo cha kupigia kura) hiyo screen wewe unapuch ur voting card number then unapata picha za wagombea udiwani. unamchagua wako then inakuletea wagombea ubunge same thing until raisi.

to make it effective hizo devices ziwe zinasupport upto 4G. waongee with each mobile network ili data zitumwe to regonal centers n central command. hakuna mtu kuweka mkono wala nini. verification features zitakuwa reasonable n itacheki 4 errors on its own.

Ican guarantee u presidential results in 3 hours from closing of all polling stations nationwide.

dedicated servers can be used na mambo mengine kibao kiasi kwamba hata wazime umeme haitasaidia wala wabanie network connection itakula kwao. TATIZO NEC WATASEMA ITS TOO COMPLICATED N WE CANT AFFORD. ila wanatumia ma land cruiser.]
Mkuu nimefurahishwa sana na mchango wako hapo juu. Kumbe ni kweli inawezekana hata kupiga kura kwa kutumia simu bila hata ya kuchafuana vidole na mpigaji akiwa popote anaweza piga kura bila ya uwezekano wa kurudia yaanikupiga zaidi ya mara moja kwani program itagundua udanganyifu na kugoma kusajili kura ya marudio. Tatizo hapa ni corrupt government system ambayo inafahamu kwa kina possibility hii na unafuu wake lakini wanaukumbatia utaratibu huu wa karne ya 20 ili kufanikisha uhaini wao. Kama program hii ingetumika, sasa hivi CCM wangkewa chaliiiii.
 
Back
Top Bottom