Elections 2010 Kwa nini NEC isiwe na database ya matokeo kwa kila kituo?? (MAWAZO)

kanyagio

JF-Expert Member
Dec 10, 2009
1,021
365
:thinking:
mimi nimekaa najiuliza: hivi kwa nini tume ya uchaguzi - NEC isiwe na database (benki ya taarifa) ya uchaguzi kwa vituo vyote kwa ajili ya transparency na future reference. Mimi siyo mtaalamu wa computer, lakini naamini NEC inaweza kabisa kuwa na database matokeo ya diwani, mbunge na rais.. Uwepo wa database hii utasaidia sana kwa kila mtanzania kujua katika vituo 52,000 vya kupigia kura- kila mgombea kapata nini. tena ukiwa na interactive database inaweza kumwezesha mtu ku-generate reports mbalimbali e.g. kura za CHADEMA au CCM kwa kila kata, wilaya au hata kituo. hii itaongeza transparency.. aidha database hii inaweza kutumiwa na vyama kuona ni maeneo gani wamefanya vizuri na wapi wamefanya vibaya.. na hatimaye kutengeneza mikakati kwa chaguzi zinazokuja!!

jambo la pili, kwa nini compilation ya kura isiwe inafanyika electronically-- hii itapunguza muda wa kutangaza matokeo na pia kupunguza uchakachuaji (kama kutakuwa hakuna IT intruders). Nina mfano wa project moja ya tathmini ya magonjwa ya mifugo katika nchi ya jirani,. katika project hii walichofanya ni kuwa na database kila wilaya ambapo project hii ipo na pia wana central database.. Waganga wa mifugo waliopo vijijini wanakuwa na uwezo wa kutuma SMS kupitia simu zao za mikononi; yaani unatuma message kwa kufuata mfumo huu:- jina la kituo:number ya ng'ombe wagonjwa:namba ya ng'ombe waliokufa: idadi ya ng'ombe waliofanyia post-morterm (mfano Boko:40:5:3); kwenye database basi taarifa inapokelewa na kuhifadhiwa na kuthaminiwa,,. kama umekosea jinsi ya kuandika message, unapata message nyingine ambayo inaeleza makosa uliyofanya.

sasa kwa nini NEC isingekuja na utaratibu kama huu; yaani unakuwa na database katika kila jimbo then central database makao makuu ya NEC (unachofanya ni kuhakikisha kuna high security na mechanism nyingine ya kukabiliana na wizi kupitia IT). kwa utaratibu msimamizi wa kituo anatuma SMS kwenda database iliyopo makao makuu ya jimbo. then msimamizi wa jimbo anatangaza matokeo ya udiwani, mbunge na rais katika ngazi ya jimbo. then taarifa za zinaenda Central database iliyopo NEC kwa ajili ya (i) kwanza taarifa (kwa upande wa madiwani na mbunge) na (ii) pili kufanya compilation ya matokeo ya uraisi. Aidha wakati huo huo wasimamizi wa kila kituo na jimbo wabandike matokeo katika kituo na jimbo ili kila mwananchi ayaone na akitaka aweze kuingia kwenye database na kulinganisha. wasimamizi wanaweza kuwasilisha other documentations kwa msimamizi wa jimbo later

faida ya mfumo huu ni hizi:

  1. kwanza inawezekana kwa sababu simu za mkononi zimetapakaa nchi nzima (labda maeneo machache)
  2. itapunguza muda wa kutoa matokeo
  3. itapunguza wizi wa kura katika ngazi mbalimbali
  4. itapunguza gharama
  5. itafanya mfumo wa utangazaji kuwa decentralized
OMBI: napendekeza serikali pamoja na UNDP wahakikishe mfumo huu unatumika.. tunaweza kuanza kwa majaribio katika uchaguzi wa serikali za mitaa kwa baadhi ya sehemu kama pilot...Then in 2015 iwe full swing!!!

wananchi hapo mnasemaji
 
Waweke data base halafu wataiba vipi kura? wewe unadhani ccm hawajui kwamba hawapendwi? kwanini walifunga vyuo vikuu? Hukuusoma ule waraka wa lacairo ulioelezea kuwa vijana ni wengi na wote hawaipendi ccm?

INTELLIGENCE SECURITY wametimiza wajibu wao kwa Makamba.
 
hahahaah huwo ni ukweli,lakini hawawezi na watatoa sababu nyingi sana...utasikia ohhh hakuna rasilimali watu ,hakuna hiki,pamoja na sababu yao kuu kubwa amani itavunjika au tutaiweka amani pabaya....hii yote ni bureucracy.....time is liberty...hawataweza kutu fool all time....
 
Back
Top Bottom