kwa nini ndugu wanapenda kugombania mali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

kwa nini ndugu wanapenda kugombania mali

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Joyceline, Apr 9, 2009.

 1. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #1
  Apr 9, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mimi nashangaa mwanaume anapofariki kama alikuwa na mke au mchumba wanaanza kumsakam huyo mwanamke na kudai anajua mali za mtota wao zilipo.
  Kuna rafiki yangu mchumba wake amefariki juzi amezikwa jana aliuwawa na majambazi huko kampala na ilikuwa afunge ndoa na mchumba wake wiki mbili zijazo,maandalizi yalishaanza.
  Ndugu wa mvulana kusikia tu amekufa wakaanza mtafuteni R mchumba wa huyo marehemu atuonyeshe hela za fulani zilipo ni kweli huyo mvulana kila kitu chake anakijua huyo dada mpaka pesa, haziko benki ila huyo binti anajua zilipo na wamemzuia kwenda kwenye mazishi kwa madai kamuua mpenzi wake arithi mali na si kweli baba wa kijana hana shida anamwambia chukua chochote ulichonacho alikuwa mchumba wako kasheshe ni mama na mashangazi na wakati wanaanza uhusiano jamaa alikuwa form five kwa hiyo mali kazipata wakiwa nae..
  sasa mimi kaniuliza awaonyeshe pesa zilipo au anyamaze nazo. halafu kama miezi miwili iliyopita jamaa alimuandikisha kila kitu huyo mchumba wake na akaweka kwa mwanasheria maana ndugu zake wakorofi avirudishe au achukue, nisaidieni nipate cha kumjibu
   
 2. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #2
  Apr 9, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Kuna zana kwamba mme ndo kichwa cha familia na mwenye haki miliki ya maali zote katika familia....kwa hiyo mme pindi anapoondoka wanafamilia wanajua ni haki yao kudai chao kwa mjane wanasahau watoto wataishi na nani?Vilevile wanasahau kuwa mama naye amechangia kwa kiasi kikubwa kupatikana kwa mali hizo hata kama alikuwa mama wa nyumbani lakini alikuwa anampepea mzee anamliwaza na kumpa ushauri mzuri mpaka hapo walipo fikia.
   
 3. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #3
  Apr 9, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Joyceline,
  Huyo mdada yeye rohoni mwake anajisikiaje?
  Ingekuwa mimi, ningeangalia tu kile ambacho kihalali ninaona nina haki nacho.Kung'anga'nia kila kitu na huku alikuwa bado hajaolewa kutapelekea asumbuliwe bure.Ndiyo maana ni vema kurasmisha mahusiano ili kuzuia mambo kama haya.Angekuwa mke aliyefunga ndoa, basi angekuwa na uhalali kugombea haki yake na sheria pia ingeweza kutumika kumlinda.Kama Fidel alivyosema hapo juu, angekuwa na haki na kila kitu kama mjane wa marehemu alimradi marehemu hakuwacha wosia wenye maelekezo mengine kuhusu urithi.
   
 4. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #4
  Apr 9, 2009
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,927
  Likes Received: 2,080
  Trophy Points: 280
  Katika taratibu za mirathi za kidini ama kiserikali sidhani kama mchumba ana haki ya kurithi. Labda kama kulikuwapo na 'dhana ya ndoa' na huyo dada alikuwa defacto ni mke wa marehemu.

  Huyo marehemnu ni dini gani?
   
 5. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #5
  Apr 9, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mwambie avirudishe na arudishe hela au aonyeshe hela hizo zilipo haraka sana. Akibana mzimu wa marehemu utamwandama maana sio haki yake kumiliki pesa na vitu vya marehemu atakuwa amewadhurumu ndugu zake marehemu.
   
 6. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #6
  Apr 9, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Huu ni mgogoro wa kisheria, ambapo kimsingi maoni hayana nafasi bali sheria inabidi ichukue mkondo wake.

  Wataalamu wa sheria tupeni mwongozo.
   
 7. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #7
  Apr 9, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Kwa kumwandikisha una maana gani? Aliandika wosia na kumuachia kila kitu au aliweka hati za mali zake kwa jina la huyo dada? Hii ni muhimu kujua maana itakuwa ndo msingi wa madai yake.
   
 8. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #8
  Apr 9, 2009
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mkuu Fidel umeshaambiwa huyo alikuwa ni mchumba, si mke. Mchumba hata kama alikuwa na watoto hatambuliki popote yeye na watoto wake. Ndiyo mjue umuhimu wa kufunga ndoa.
   
 9. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #9
  Apr 9, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mkuu ndo maana hapo juu nikasema huyo binti hana haki ya kumiliki vitu na mali pamoja na pesa za mchumba wake maana hajaidhinishwa kisheria kama mke wa marehemu. Kwa hiyo pale hana chake.
   
 10. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #10
  Apr 9, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Nadhani kuna sheria inayosema mwanaume na mwanamke wakiishi kwa kipindi fulani, kisheria wanakuwa na haki fulanifulani hivi za kindoa. Wenye uelewa watalinyoosha hili.
   
 11. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #11
  Apr 9, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0  kama nimemsoma vzr joyceline anasema mchumba alihamwandikishia kila kitu huyo mchumbake, so mchumba wa kiume kwa maana nyingine alishamkabidhi huyo dada sehemu ya vitu vyake, sasa hata hivyo alivyoandikishiwa na marehemu mwenyewe avirudishe?.....fidel mzima baba?
   
 12. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #12
  Apr 9, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  ni hivi huyu binti ni yatima alikuwa msichana wa kazi kwa kina huyo kijana wakapendana wakamfundisha ufundi tangu akiwa na miaka 14. muda ulivyoenda kijana akamuhamisha kutoka arusha akamleta dar akamtafutia shule zile za QT ili asome maana akiwa kule kazi za nyumbani nyingi atashidwa kusoma akawa anamtembelea mara kwa mara ndo amemaliza form six mwaka huu, ndo jamaa alikuwa anataka wafunge ndoa kabla hajaenda chuo. sasa vitu vingi vya huyu kijana dada anavijua na ndo alikuwa tegemeo lake kula, kulala, na ada sasa anauliza akiwapa hela zote atashidwa kusoma na ndo anamtegemea na kuna vitu vingine vya kijana yeye ndo anajua vilipo awaonyeshe vyote anachohofia anaweza akawapa kila kitu akakosa msaada. Embu vaeni viatu vyake ndo ingekuwa nyie na ndugu wameishaanza maneno kweli watampa kitu atakuwa mgeni wa nani, kumbukeni yule ndo ndugu yake hana m2, yuko peke yake hana wa kumlilia.
   
 13. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #13
  Apr 9, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Fidel hujanielewa ni hivi wakati wa uhai wake marehemu alimwambia, ngoja nikuandikishe vitu vyangu kabisa maaana nikifa hapa ndugu zangu nawajua hutapata kitu na unanitegemea mimi, hati za nyumba na mambo mengine vimeandikwa jina lake sasa anachouliza avitoe awape na hizo pesa za marehemu au anyamaze wabakie na hivyo vilivyoko arusha, maana vya dar vyote hawavijui
   
 14. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #14
  Apr 9, 2009
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  Acheni kumtisha dada wa watu,marehemu alimwandikisha na kumwonyesha mali zake akiwa na akili timamu.Dada wala usirudishe kitu,mtaani wanasema zali la mentali limekudondokea!
   
 15. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #15
  Apr 9, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Amwandikishe kwani alikuwa mke wa marehemu? mbaka awepo kwenye urithi?
   
 16. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #16
  Apr 9, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mkuu mtakuja kula vitu vya wamwinyi mkavimbishwa nanihii shauri zenu watu wanatengeneza kitu.
   
 17. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #17
  Apr 9, 2009
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Jamaa alijuaje kama yeye ndo atatangulia kufa kabla ya mchumba wake (msichana) ? Kama msichana angetangulia kufa, nani angerithi mali za huyo marehemu (msichana)? Kuna utata hapa, maybe jamaa ameuawa kiaina.
   
 18. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #18
  Apr 9, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Je walikuwa wanaishi wote sehemu/chumba kimoja?

  Hawa ndugu wana haki kuuliza mali kwa vile huyu jammaa hakuwahi kuwa na mke!

  Concept ya kuishi pamoja pia inajegemea kama kuna watoto!

  Kama hamna hata mtoto..basi ni ngumu hapo kisheria hakimu atagawa mali zaidi wazazi watapewa % kubwa na huyu dada atapata tu kifuta machozi!

  Ila kama mali alimwandikishia huyu dada..na walikuwa wachumba..je alijuaje atakufa??? hapo kuna utata!!

  Hata mie ningekuwa ndugu yake marehemu lazima tu ningeuliza kulikoni uandikishiwe mali wakati wewe ni mchumba?
   
 19. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #19
  Apr 14, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  nimewasoma vizuri ni hivi, huyu dada alikuwa housegirl wao wakamsomesha ufndi wa cherehani , huyu kijana akampenda wakanza uhusiano uhusiano ulipokomaa akawaambia wazazi nataka kumsomesha maana ndo atakuja kuwa mke wangu wazazi wakapinga pinga ila jamaa akakomaa, akamleta dar kwa mama yake mdogo kaaka kwa muda akatafuta nyumba akanunua hapa dar akaandikisha jina la msichana tabgu 2005 akamwambia kaa hapa utulie usome, jamaa alikuw ICTR arusha akwa anakuja kumwanga lia mara kwa mara akamfungulia account sasa sababu alikuwa ni mke mtarajiwa mambo mengi alikuwa anajua, huyo kaka anazo mali hata arusha ana vitu vingi nadhani 75% vya dar ni 25%. na kuhusu kusema kwamba alijia atakufa siku hizi ni mambo ya kawaida kuandika uridhi kila mahali mbona kwenye maofisi tunaambiwa tuandike warithi. Sasa kuna hela nyingi zilikuwa ndani huyu dada anasema awape wazazi wake au, maana huyu kaka alimwambia ndugu zangu wakorofi linaweza kutokea lolote wakakusumbua. Ni kweli huyu kaka ameuwawa na wakati anauwawa msichana alikuwa na mimba alivyopewa habari za msiba mshtuko mimba ikatoka.msichana walikuja watu wakamuhoji ijumaa basi wakamwambia wakimuhitaji watamfuata ila kuna baba mdogo wa kijana anashikiliwa na polisi hadi leo kwa mahojiano nitakuwa nawaletea kila kinachoendelea.Ofisi za Un zina camera wamechukua kwa uchunguzi
   
 20. P

  Preacher JF-Expert Member

  #20
  Apr 14, 2009
  Joined: Aug 25, 2008
  Messages: 328
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Issue ni kuwa hivi mtu unapokuwa hai, ukachuma mali - na mali ni za KWAKO MWENYEWE - nadhani una uhuru wa kumrithisha umtakaye mali zako - kama utakufa - of course in the case of WANANDOA - MALI YA URITHI NI YA MWANANDOA MWENZAKO UTAKAYEMWACHA HAI - kwa case ya huyo kijana ni sawa kaona amwachie mchumba kwani ni mtu aliyemwingia moyoni mwake. NDUGU WENGINE HUWA HUWAFANYI BIDII YOYOTE KATIKA MAISHA WAKO BUSY KUSUBIRIA NDUGU AKIFA WACHUKUE -
   
Loading...