Kwa nini ndoa kuvunjika haraka inawakumba sana vijana?

Zinavunjika kwa sababu wote walioana wakijua ndoa si kifungo; they can walk in and out as they wish! Kwa hiyo wanaokotana tu wakijua fika kuwa if he/she is not the one nachapa lapa.

Wale wanaochukulia ndoa kuwa ni life time commitment wanafanya upembuzi yakinifu kabla ya kuingia kwenye commitment.

Ndoa inakuwa jinsi ilivyo kwa kuwa watu wanataka iwe hivyo. Na ndoa ya kuvunjika nyingi zinajulikana hata kwa ndugu na jamaa za karibu from the wedding day. Utasikia "hapa kazi ipo" hapo ujue wote mapepe. Mmoja akiwa mapepe mwenzie katulia chance ya ndoa kudumu ni higher kuliko wote wakiwa mule mule.

Ndoa zinazodumu ni za couples ambazo ni mature. Na maturity si age!
 
Wanaingia kila mmoja akijifanya mjuaji sana.Sasa nani atamsikiliza nani?
Wanakubaliana kutokukubaliana kama wanasiasa.Hawajui hiyo ni ndoa siyo siasa.
 
....Tatizo siku hizi kila mmoja anajifanya yeye mjanja, hakuna anayejishusha. Vile vile wanawake wengi siku hizi hawataki kupelekeshwa kama wamama waliolewa zamani.....na wanaume wengi wa siku hizi maneno mengi mdomoni, nakupenda nyingi, vitendo hakuna.

Uvumilivu kwenye ndoa za sasa ni zero, wanasema maisha mafupi na raha jipe mwenyeweeee!! Hivyo watu wanataka mteremko tu kwenye ndoa , wamesahau kama kuna milima na mabonde.
 
Ndoa ni fenomeno ambayo haina fomula, sijawahi ona
ndoa =pai R skwea.

Fanyeni muwezavyo ili mzeeke pamoja ili tuwafanyie sherehe ya miaka hamsini au ishirini na tano
 
Habarini wana MMU
nimefanya analysis nimegundua vijana wa zama hizi ndoa zao ni nguvu ya soda wanaachana fasta kwanin?
Mfano. Bro wangu mmoja ni tutorial assistant pale SUA alimuoa class mate wake bonge la harusi kule kwetu mwanza waliachana baada ya miezi miwili kwa Ugomvi mkubwa sana na bro mwingine alioa mwaka jana mwezi wa 7 binti mmoja wa kidigo yani by december ndoa ikavunjika kbsaaa
sasa wenzetu mliodumu ndoani what are the mistakes tunazokosea jamani???
Tujulisheni tujifunze maana haileti picha nzuri kabisa.

1. kuwa "tutorial assistant SUA "hakuvunji ndoa wala kuongeza kudumu kwa ndoa
2. ukioa "mdigo "siyo ndo ndoa yako itadumu, aidha siyo kweli kuwa ndoa yako haitadumu
3.si kweli ukiwa "tutorial assistant SUA" au ukioa msichana "mdigo" ndiyo wewe ni "kijana wa zama hizi"

aidha kutokana na ukweli kuwa hawa wote uliowataja kuwa ndoa zao hazijadumu ni "Bro" zako. inaweza ikawa ina nguvu ya kiuchunguzi ikiwa utahusisha kuvunjika kwa hizo ndoa na familia, au ukoo wenu. kuhusisha na vijana wa zama hizi haitoshi kwani hilo eneo ulilochukua sampuli zako ni jembamba mno kuwakilisha jamii ya vijana wa zama hizi
 
Soap Operas zinawadanganya sana vijana.
Ukisasa ndio unawapoteza maana wameyapokea tofauti sana.
Eti unakuta Dada Anamwambia mchumba/mumewe kuwa hawezi kuachana na facebook ila yuko tayari waachane.
Na wengine hukimbilia kuolewa ili wasiwachwe nyuma na wenzao, na sio sababu wana mapenzi ya kweli.

USHAURI.
Ukimaliza shule/chuo au ukianza kujitegemea usikimbilie ndoa au kuishi na mpenzi. Kama binadam unahitaji uhuru, tumia muda kidogo kufurahia maisha ukiridhika na kuona sasa ni kweli unahitaji mwenza fanya hivyo na hautopata shida.

Mtu katoka chini ya sheria na ulinzi wa wazazi anakimbilia ulinzi mwingine wa mke/mume. Lazima mchokane mapema muachane
 
Ndoa ni kwa ajili ya wanaume na wanawake na siyo kwa wavulana na wasichana. Kama hujaelewa wewe bado ni mvulana.

Hili jibu linaweza kuonekana simple ila limebeba msingi mkubwa sana wa majibu kwa mtoa mada. Utoto tunaosema hapa siyo kutobalehe bali unaweza kuwa umebalehe lakini uwezo wenu wa ku stahimili mikiki mikiki ya ndoa ikawashinda kwa sababu ninyi mnaoana mkifikiri ndoa ni paradiso. Pia ndoa huwezi kuiga eti na mimi nataka niwe na ndoa kama watu wengine; ukienda hivi hata mwezi ukimaliza ktk ndoa utakuwa umejitahidi sana.
 
Soap Operas zinawadanganya sana vijana.
Ukisasa ndio unawapoteza maana wameyapokea tofauti sana.
Eti unakuta Dada Anamwambia mchumba/mumewe kuwa hawezi kuachana na facebook ila yuko tayari waachane.
Na wengine hukimbilia kuolewa ili wasiwachwe nyuma na wenzao, na sio sababu wana mapenzi ya kweli.

USHAURI.
Ukimaliza shule/chuo au ukianza kujitegemea usikimbilie ndoa au kuishi na mpenzi. Kama binadam unahitaji uhuru, tumia muda kidogo kufurahia maisha ukiridhika na kuona sasa ni kweli unahitaji mwenza fanya hivyo na hautopata shida.

Mtu katoka chini ya sheria na ulinzi wa wazazi anakimbilia ulinzi mwingine wa mke/mume. Lazima mchokane mapema muachane

Kwenye red kidogo natofautiana na wewe kwani mimi sikupitia hiyo stage na nina 12 years kwenye marriage na ups and downs tunazimudu kiutu uzima tangu tuoane. Ndoa imeanzishwa na Mungu mwenyewe pale bustani ya Edeni na ili mdumu ktk ndoa principle ya kwanza ni kumwomba Mungu hata kabla ya kufikia kuchumbia ili akupatie mwenzi mtakayeweza kuishi pamoja kwa amani, upendo na kuvumiliana ktk kipindi chote cha uhai wa ndoa yenu. Then mchumba unayempata unamweleza vitu realistically na mnajadili kiuwazi na ukweli aina ya ndoa mnayotaka kuwa nayo. Ndoa nyingi zinaanzishwa ktk udhanifu zaidi kuliko kiuhalisia kwani vijana wanadanganyana sana. ndoa inapojengwa ktk msingi dhaifu kama udanganyifu, utapeli na madoido ya kupelekana vilabu ujue haitadumu kamwe kwani kama mlipendana kwa sababu ni waenda club ujue hapo imekula kwenu na ndoa itakatika soond mtakapotaka kuishi maisha ya kiukweli ya ndoa.
 
....Tatizo siku hizi kila mmoja anajifanya yeye mjanja, hakuna anayejishusha. Vile vile wanawake wengi siku hizi hawataki kupelekeshwa kama wamama waliolewa zamani.....na wanaume wengi wa siku hizi maneno mengi mdomoni, nakupenda nyingi, vitendo hakuna.

Kwa hiyo ww

Uvumilivu kwenye ndoa za sasa ni zero, wanasema maisha mafupi na raha jipe mwenyeweeee!! Hivyo watu wanataka mteremko tu kwenye ndoa , wamesahau kama kuna milima na mabonde.

Kwa hiyo wewe unatoa ushauri gani au na wewe umekata tamaa ya kuishi hadi uzeeni na mume wako? Maadili mema huanzia nyumbani ila siku hizi wasichana hukataa kata kuwasikiliza mama zao ambao isipokuwa ni tabia zao njema hawa wasichana wasingezaliwa ktk ile familia. Kutaka uhuru na haki kwingi kumewafanya akina dada kuvimba vichwa badala ya kuwanyenyekea waume zao na waume zao wawapende. Mwanmke asiyemnyenyekevu ni vigumu sana mumewe kumpenda na huishia kugombana na hatimaye ndoakukatika
 
1. kuwa "tutorial assistant SUA "hakuvunji ndoa wala kuongeza kudumu kwa ndoa
2. ukioa "mdigo "siyo ndo ndoa yako itadumu, aidha siyo kweli kuwa ndoa yako haitadumu
3.si kweli ukiwa "tutorial assistant SUA" au ukioa msichana "mdigo" ndiyo wewe ni "kijana wa zama hizi"

aidha kutokana na ukweli kuwa hawa wote uliowataja kuwa ndoa zao hazijadumu ni "Bro" zako. inaweza ikawa ina nguvu ya kiuchunguzi ikiwa utahusisha kuvunjika kwa hizo ndoa na familia, au ukoo wenu. kuhusisha na vijana wa zama hizi haitoshi kwani hilo eneo ulilochukua sampuli zako ni jembamba mno kuwakilisha jamii ya vijana wa zama hizi

Bwana mdogo karudi darasani ujifunze upya ku present point zako. halafu Huku kujidai kujua kila kitu na kubisha bisha ndiko kunakowaponza vijana kama wewe. Unataka afanye utafiti gani zaidi ya huo .Ebu acha kuleta theories za darasani ambazo humu haziwezi kamwe kufanya kazi hapa tunaongea kwa uzoefu.
 
Habarini wana MMU
nimefanya analysis nimegundua vijana wa zama hizi ndoa zao ni nguvu ya soda wanaachana fasta kwanin?
Mfano. Bro wangu mmoja ni tutorial assistant pale SUA alimuoa class mate wake bonge la harusi kule kwetu mwanza waliachana baada ya miezi miwili kwa Ugomvi mkubwa sana na bro mwingine alioa mwaka jana mwezi wa 7 binti mmoja wa kidigo yani by december ndoa ikavunjika kbsaaa
sasa wenzetu mliodumu ndoani what are the mistakes tunazokosea jamani???
Tujulisheni tujifunze maana haileti picha nzuri kabisa.

Kashengo
Ndoa za sasa hazidumu like before because people (and by that I mean women) now days have choices! Fortunately tumefunguka macho and we are no longer afraid to put ourselves and our hapiness first. Sio kama zamani mtu unakuta anavumilia crap after crap iili asiachik na kuishia kuaibika na kutokuitwa someone's missus !
 
Pia dhana ya kuendeleza u-boyfriend and u-girlfriend kwenye ndoa ni kikwazo. Kwenye ndoa kuna vikwazo ambavyo unakuta wengi hajavifikira kwa umakini wake.... nafasi ya ndugu, marafiki kwenye ndoa yenu; matatizo yenu mnayatatua ndani ya kuta nne au ndio mnampelekea mtu; matumizi ya pesa; mipango ya baadaye; watoto (huyu anataka sasa mwingine anataka baada ya miaka miwili, n.k); mnaongea lugha moja au kila mtu ndio msemaji wa familia; ushirikiano, maelewano, heshima n.k. Ndoa ni kazi inayohitaji akili, ufanisi, sema mshahara wake si pesa
 
Kashengo
Ndoa za sasa hazidumu like before because people (and by that I mean women) now days have choices! Fortunately tumefunguka macho and we are no longer afraid to put ourselves and our hapiness first. Sio kama zamani mtu unakuta anavumilia crap after crap iili asiachik na kuishia kuaibika na kutokuitwa someone's missus !

Hapo kwa bolded and red: hebu fafanua, una maana unapoona mambo ni kinyume na ulivyodhani ndo unaamua kwenda kwingine au?
 
Bwana mdogo karudi darasani ujifunze upya ku present point zako. halafu Huku kujidai kujua kila kitu na kubisha bisha ndiko kunakowaponza vijana kama wewe. Unataka afanye utafiti gani zaidi ya huo .Ebu acha kuleta theories za darasani ambazo humu haziwezi kamwe kufanya kazi hapa tunaongea kwa uzoefu.

Umepiga ikulu hapo mkuu, ndo maana unaona hasira zote hizo.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom