Ushindi wa CCM Igunga ni obvious kutokana na sababu moja kuu, kwamba wapiga kura ni watu wenye uelewa mdogo sana kuliko mimi na ww, na wale wenye uelewa mkubwa tuseme wasomi ndiyo hao ambao mara nyingi huwa hawapigi kura.<br>Uelewa mdogo wa mambo yanayoendelea nchini unaweza kuulinganisha na elimu duni inayotolewa na serikali ya ccm, kwa kuhakikisha shule za kata zisizo na waalimu wa kutosha, maabara, maktaba n.k.<br>Mtu wa kawaida katika vijiji na kata za Igunga hajui kama tunailipa Dowans kwa uonevu kwa hali ya juu kutoka kwenye kodi zetu. Infact hajui hata hiyo kodi anailipa hata kwenye sabuni anayoitumia kuogea. Simply ni kwamba hana elimu. Vyombo vya habari kama magazeti husomwa na watu wachache mjini Igunga, wengi vijijini hawajui kusoma na hawana hela za kununulia magazeti. Hivyo hawana habari ya maovu ya ccm. CCM bado kwao ni ya mwalimu.Uislamu nao umeshika kasi yake Igunga. Tunapoongelea hili tunaongelea ufinyu wa elimu dunia kama tunavyoiita wenyewe.<br>