Kwa nini naona Watanzania Bara tumenufaika sana na Muungano zaidi sana wa Wazanzibar - wametuokoa mara mbili kutoka shimo lenye giza nene!

Mimi ni Mtanzania bara. Nimetafakari sana juu ya kile watu wa Tanzania bara wanaita kero za Muunganom au kupendelewa kwa Wazanzibar katika muungano. Utaona kwamba ni mambo madogodogo sana, vitu kama fedha za misaada sijui, Wazanzibar kuwekeza bara na kununua ardhi tofauti na watu wa bara wakienda Zanzibar, watu wa bara kupewa nafasi za uwaziri wizara zisizo za Muungano nk. Vitu vidogo vidogo sana. Jambo wanalosahau wengi ni kwamba watu wa Zanzibar ni Watanzania kwanza na Wazanzibar pili, na Uzanzibari wao haupaswi kuwaondolea Utanzania wao.

Lakini sisi watu wa bara tuna mengi sana ya kushukuru kwa kuwa Muungano umewezesha Wazanzibar watuokoe katika majanga makubwa mawili.

Janga la kwanza lilikuwa kutoka hali mbaya sana kiuchumi tuliyokuwa nayo miaka ya mwisho ya Nyerere.

Raisi Mwinyi toka Zanzibar alikuja akatubadilishia kabisa maisha kwa sera yake ya Ruksa. Nchi ilikuwa imefikia hali mbaya, na huenda hata kungetokea mapinduzi kama sio Mwinyi kubadilisha mambo. Hilo la kwanza.

La pili ni hali mbaya tena tuliyokuwa nayo kisiasa katika utawala wa Magufuli. Tuliona mambo ambayo hatukuwahi kufikiria yanaweza kutokea Tanzania.

Utawala wa ajabu wenye kuonea na kuumiza watu ukawepo. Nchi ikagawanyika kati ya walio upande wa wenye dola na walio upande mwingine.

Tabaka la kikabila au kanda moja likaanza kupata nguvu kubwa katika kila nyanja ya serikali - kuanzia jeshini hadi uraiani, likijijengea mizizi ya kuwa watawala tuliyoshuhudia ikileta umwagaji damu mkubwa nchi jirani. Akaja Samia kutoka Zanzibar kutuokoa na hadi sasa anafanya juhudi kubwa kututoa katika tope kubwa tulilokuwa tunazamishwa. Wanaofaidika zaidi na juhudi za mama huyu Mzanzibar ni watu wa bara, sio Zanzibar. Pia u-neutral wake kwa kuwa Mzanzibar ulikuwa factor kubwa sana katika kutokuwa na vurugu ya kugombania madaraka ndani ya CCM baada ya Magufuli kufa.

Sasa, mara mbili katika historia ya Tanzania tunaokolewa na mtu kutoka Zanzibar, na hilo limewezekana kwa kuwa watu wa Zanzibar wanaweza kuwa maraisi Tanzania kwa ajili ya muungano wetu! Na tukumbuke kwamba kwa mara zote mbii watu wa bara ndio tuliokuwa tunaumizwa, sio watu wa Zanzibar.

Je, bado tu hatupaswi kuona katika namna kubwa, sisi watu wa bara ndio tumenufaika na huu muungano?
 
Back
Top Bottom