STEIN
JF-Expert Member
- Aug 29, 2010
- 1,770
- 553
Ndugu zangu wanaJF,
Miongoni mwa sababu nyingi ambazo zinafanya waTZ wengi kutokupata kazi ni hizi zifuatazo:
1. Makampuni mengi hapa TZ kumilikiwa na wageni kiasi cha faida inayopatikana huchukuliwa na kupelekwa kwenye nchi waliko wamiliki, zingekuwa zinamilikiwa na waTZ ungekuta wanaanzisha makampuni/investment zingine na watu tukaendelea kupata ajira.
2. Kwa sababu makampuni haya yanmilikiwa na wageni, basi kumekuwa na wimbi kubwa la wageni kubebana wenyewe kwa wenyewe kwenye nafasi za ajira, mfano mzuri ni mahoteli mengi ya utalii utakuta hadi wafanya usafi wanatoka Kenya, uganda, etc.
3. Sheria za Kazi kutokufuatwa, kwani utakuta hata kazi ambayo haihitaji kuagiza mtalamu/specialist kutoka nje, anatafutiwa mtaalamu kutoka nje kwa kisingizio eti hakuna mTZ anayeweza kuhandle hiyo post.
4. Serikali kukimbia wajibu wake wa kuhakikisha inatengeneza nafasi za ajira kwa waTZ wengi badala yake imekuwa inasubiri kukata watu kodi kubwa.
5. Serikali kutokuwapa makampuni ya wazawa fursa nzuri ili yaweze kushindana na ya wageni katika kupata kazi mbali mbali badala yake imekuwa inayabeba makampuni ya kigeni.
Sababu ziko nyingi sana, tuziainishe na kuhakikisha tunapambana hadi mwisho ili kuhakisha serikali inapitia upya sera ya kuingiza wageni nchi na kufanya kazi kiholela.