Kwa nini mwanamke akifumania hujilinganisha na hawara…….?

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,807
2,000

Kimaumbile inaelezwa kwamba, mwanaume hahusishi tendo la kujamiiana na kumpenda mwanamke. Kwa mwanaume, kupenda ni jambo moja na tendo la kujamiiana ni jambo lingine. Hii ni tofauti na wanawake ambao wanaonekana kuunganisha tendo la kujamiiana na kupenda.Ndiyo maana katika hali kama hiyo, unaweza kukuta mwanaume anatoka nje, anafumaniwa na mkewe, badala ya kuwa mjeuri huomba radhi sana nap engine hutoa zawadi kubwakbwa ili kumbembeleza mkewe asimwache. Anaweza kufumaniwa hata mara tano, lakini bado akaendelea kuomba radhi na kunyenyekea sana kwa mkewe. Mtu anaweza kujiuliza, kama anamtaka au bado anampenda huyo mke wake, ni kwa nini ameamua kutoka nje , tena siyo mara moja?Ni kwamba mwanaume hatembei na mwanamke kwa sababu anampenda, bali anaweza kuoa mwanamke kwa sababu anampenda. Kutembea na mwanamke, kwa mwanaume ni suala la haja ya mwili kujiridhisha na labda udadisi kutaka kujua umbo la mwanamke la aina hii lina ladha gani kimapenzi lakini siyo kupenda.Unaweza kukuta wanaume wengine wanatembea na wanawake lukuki, lakini wakifika nyumbani wanakuwa na adabu zao. Kwa wanawake hali siyo hiyo, na ndio maana mwanaume akimfumania mkewe, inabidi ajue kwamba, kupendwa kumeisha au kumefifia sana. Hii ni kwa sababu kwa mwanamke kupenda na tendo la ndoa ni kama kitu kimoja. Kwa mwanamke kama hampendi mwanaume, kufanya naye mapenzi ni vigumu, labda tu kama amempendea fedha na anazihitaji sana ili kumaliza matatizo yake ya kifedha au anafanya biashara.Ndiyo maana wanaume wanapowafunia wanawake huumia zaidi na huweza kuchukua hata hatua mbaya, ukilinganisha na hatua wanazochukua wanawake. Hata kama mwanamke aliyetoka nje ataomba radhi na kudai kwamba, alitoka kwa bahati mbaya na mazingira yanaonyesha hivyo, bado mwanaume atasukumwa na kitu asichokijua kuamini kwamba, sababu pekee ya mpenzi wake kutoka nje ni kujirahisisha. Kwa kudhani kutoka nje ni kujirahisha na kukosa thamani, mwanaume humchukulia mke au mpenzi wake kwa thamani ya chini sana. Ndiyo maana huanza kumwita Malaya, kahaba na majina mengine yanayofanana na hayo.Kwa mwanamke hali ni tofauti, yeye akifumania anataka kujua huyo mwanamke aliyemchukua mumewe au mpenzi wake anamzidi kitu gani. Hii ni kwa sababu, akilini kwa mwanamke huamini kwamba kuna kitu kilichomvutia mumewe au mpenzi wake kwa huyo mwanamke aliyemfumania ambacho yeye hana. Mwanamke atajitahidi kujilinganisha ili kutafuta kile kilichomvutia mumewe kwa mwanamke huyo, na ndipo hapo maswali kama haya hujitokeza. “Hivi ulimpendea nini yule mwanamke..? au “ Ni kitu gani ulichokikosa kwangu mpaka ukakifuata kwa yule mwanamke…..?”
 
Kongosho

JF-Expert Member
Mar 21, 2011
36,024
1,500
Ili ajue kama kweli moja yashinda sifuri, kuna saa sifuri yashinda moja (usibishe, kihesabu inawezekana kabisa ukiweka negation, kadhalika kimahusiano)
 
utafiti

JF-Expert Member
Jul 18, 2013
12,794
0
Mwanamke ni mdhaifu sana na hudanganyika kwa kitu kidogo na kuacha kitu muhimu. Mwanaume anaweza kua na nyumba ndogo (kimada) ila bado akatunza familia yake na kumpenda mke wake kama kawaida, ila mwanamke akionyeshwa pesa tu hapo mume wake/mpenzi ndo anakua takataka, wengi ndo huondoka na mabegi yao kuhamia kwa "mpenzi" mpya...do not trust a woman...
 
Kongosho

JF-Expert Member
Mar 21, 2011
36,024
1,500
Wee nae, mwanamme kuwa na mke afu ana kimada sio udhaifu?

Kongosho, ni kweli mwanaume kuwa na kimada ni udhaifu lakini anajali familia yake na anakuwa na adabu zote akiwa nyumbani kwake. kwa mujibu wa madai ya MTAFITI anasema kwamba mwanamke akimpendea mwanaume pesa anafungasha mabegi na kuhamia kwa mume mwenye pesa na kumtelekeza mumewe... Hebu tujadili kwa kuanza na tuhuma hizi za MTAFITI
 
Last edited by a moderator:

Kongosho

JF-Expert Member
Mar 21, 2011
36,024
1,500
Mwanamke sio pesa tu, hata akimpenda shamba boi wa nyumbani kwake, basi mapenzi yake yoote huhamishia huko.
Wanamme wana uzoefu wa mitala, kwa hiyo kugawanya mapenzi kwao si shida. Wanawake wanajifunza japo wapo walohitimu pia na kufaulu.

Bottom line ni kuwa, ukishatoka nje ya mahusiano yako halali wewe ni dhaifu, no shugakoting'i.

Kongosho, ni kweli mwanaume kuwa na kimada ni udhaifu lakini anajali familia yake na anakuwa na adabu zote akiwa nyumbani kwake. kwa mujibu wa madai ya MTAFITI anasema kwamba mwanamke akimpendea mwanaume pesa anafungasha mabegi na kuhamia kwa mume mwenye pesa na kumtelekeza mumewe... Hebu tujadili kwa kuanza na tuhuma hizi za MTAFITI
 
Heaven on Earth

JF-Expert Member
Mar 21, 2013
37,140
2,000
Mwanamke ni mdhaifu sana na hudanganyika kwa kitu kidogo na kuacha kitu muhimu. Mwanaume anaweza kua na nyumba ndogo (kimada) ila bado akatunza familia yake na kumpenda mke wake kama kawaida, ila mwanamke akionyeshwa pesa tu hapo mume wake/mpenzi ndo anakua takataka, wengi ndo huondoka na mabegi yao kuhamia kwa "mpenzi" mpya...do not trust a woman...

Mhhhhhhhhhhhhhh hii ni iksipiriensi ama
 
Mashaxizo

JF-Expert Member
Jun 13, 2013
6,712
1,225
Khaa! Jamaani!
Natamani huu uzi auone Cka wangu!
Haniskilizi hata kidogo baada ya kugundua na.na.naa....
Ukweli nampenda yeye na tatizo lake MAFUTA HAYAPIMIKI!
Ningefanyaje sasa?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom