Kwa nini mkurugenzi wa halmashauri na mkuu wa wilaya wawe paka na panya? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa nini mkurugenzi wa halmashauri na mkuu wa wilaya wawe paka na panya?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mahmetkid, May 29, 2012.

 1. Mahmetkid

  Mahmetkid JF-Expert Member

  #1
  May 29, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 557
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 45
  Habari za asubuhi wa JF especially wana JI.
  Namshukuru mwenyezi mungu kwa kuniamsha siku ya leo na kuniwezesha kufika kazini salama na kuanza majukumu yangu ya kujenga Taifa kama ipasavyo.

  Mimi ni mtumishi mpya kabisa katika kulitumikia Taifa hii, nimepangiwa kazi katika Halmashauri moja ya Wilaya za Taifa hili zilizoko mipakani na nchi jirani za upande wa Magharibi mwa Tanzania.
  Kutokana na ka-elimu kangu ka chuo, nikajikuta nakuwa mkuu wa Idara husika ambayo nimesomea toka nikiwa nipo chuoni. Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa hilo pia.
  Wanajamii Intelligence, huku Mawilayani kuna mambo ya ajabu ya kiutendaji, katika kipindi cha miezi minne niliyokuwepo huku kuna mambo mengi nimeyaona tofauti kabisa na utendaji unaotakiwa. Ila kubwa zaidi nililoliona ni uadui mkubwa uliopo kati ya watu wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya (ambao wanajiita Wilayani) na watu wa ofisi ya Mkurugenzi (ambao wanajiita Halmashauri) japokuwa ofisi hizi zimetenganishwa na ukuta mmoja. hii chuki hipo hadi kati ya Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wake.
  Kwa bahati nzuri Wilaya yetu tumepata safu mpya ya viongozi kuanzia mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi hadi baadhi ya wakuu wa Idara nikiwepo na mimi.
  Mfano nzuri nilikuwa nauzulia vikao vya kumkaribisha Mkuu Mpya wa Wilaya, Wilayani wao wameanda ya kumkaribisha mkuu wa wilaya na hawataki kusikia ya kumkaribisha mkurugenzi na Halmashauri wameandaa ya kumkaribisha mkurugenzi pia hawataki kusikia habari ya kumkaribisha mkuu wa Wilaya.
  Jana kulikuwa na kikao cha Council Mainagement Team kinachoongozwa na mkurugenzi, nikaomba hili suala la sherehe mbili kwa wakati mmoja ni upotevu wa rasirimali, tunaweza kupanga zote zikafanyika kwa pamoja. Kuanzia mkurugenzi mwenyewe na wakuu wengine wa Idara wale wazamani alimanusura wanitafune mule ukumbini.
  Nakumbuka katika vikao vya kumkaribisha mkuu wa wilaya niliwahi kuulizia kuhusu suala la kumkaribisha mkurugenzi, wakaniambia Halmashauri wemeandaa ya kwao.
  Ndugu WanaJI, japokuwa mkuu wa wilaya ni political leader na mkurugenzi yeye ni mtendaji wa maendeleo ya wilaya lakini utofauti walionao unatishia amani maendeleo ya wilaya.
  Bahati nzuri hawa wote hawatakuwepo katika hizo nafasi za kazi kwani wapya tayari wameanza kuwasili.
  WanaJI naomba tunchangie hili kwa nini mkurugenzi wa Halmashauri na Mkuu wa Wilaya wawe kama paka na panya?
   
Loading...