Kwa nini Miswada ya sheria zetu iko kwa Kiingereza?

Game Theory

Platinum Member
Sep 5, 2006
8,545
835
Nimepita pale kwenye dula linalouza miswada mbali mbali iliyopitishwa na serikali na nimekuta karibu yote imeandikwa kwa kiingereza

nilikuwa nina taka sana ile ya serikali za mitaa tena ambayo inamhusu mtu wa kawaida kabisa...lakini nayo imeandikwa kwa kiingereza tena kile kigumu

sasa cha kujiuliza waziri wa Utamaduni anafanya nini?

ofisi ya waziri mkuu kwa nini hawasemi jambo kuhusu hili?

na muhimu zaidi je nia ya kuchapisha hii miswada kwa kiingereza ni nini hasa?

je ni haku kusema kuwa kuna nia za siri ambazo watawala wetu hawataki tujue?
 
Nadhani wengi wetu hususani wananchi wa kawaida wasielewe, wasije wasumbua!
 
Sheria ni taaluma iliyogubikiwa na ukoloni mamboleo. Ili uwe mwanasheria unayeogopewa ni lazima ukimudu kiingereza kigumu kilichochangnyikana na kilatini. Kama unabisha nenda kamuulize AG Werema!
 
Ile ya serikali za mitaa ni kubwa kweli lakini pia yote ni kiingereza kitupu

surely mtoto wa Mkulima anaweza kufanya jambo kuhusu hili la miswada kuchapishwa katika lugha ya Kiswahili ambayo asilimia 100 ya watanzania wanaifamu vizuri
 
Back
Top Bottom