Kwa nini Miss tanzania hutokea Dar es Salaam tu?

magaka Makoye

Member
Sep 11, 2011
5
2
Wana JF naomba mnifahamishe au mchangie hoja hii: Kwa nini miss Tanzania huwa akishinda ni lazima awe ametokea Dar es salaam nikimaanisha Ama Miss kinondoni, Miss temeke au Miss Ilala.
Hivi washiriki wanaotokea maeneo mengine kwa nini huwa hawawi Miss Tanzania?
 
Sio wote hutokea Dar......kuna waliowahi kutokea Mwanza na Arusha......ila hata mimi inanishangaza.....kwa nini hawatoki Tabora, Singida, Shinyanga na hata Mbeya?......
 
Dar tu ndio kuna watoto wa ukwehe!!(joke).
Sio wote wanatoka dar, fatilia waliotangulia. Pia inawezekana wa mikoa mingine hawajapata mwamko wa kushiriki na wenye mwamko hawana vigezo.
Lolote unalofikiria linaweza kuwa jibu.
 
wengine ni wahamiaji dar es salaam!.....urembo unapatikana dukani na dar es salaam ndo mambo yote
 
So unafananisha Dar es salaam na simiyu?

Mbona huulizi kwa nini kila wizara na Makampuni Head office zipo Dar ?

Hujiulizi kwa nini mtu anayeishi Tanga au Mtwara akiagiza gari analifata bandarini Dar wakati hata Mtwara na Tanga kuna Bandari?

Mbona huulizi kwa nini miradi mikubwa yote Dar kuanzia mabasi ya kwenda kasi, daraja kigamboni, Airport Terminal 3 etc zote zinajengwa Dar ? Mwanza mji mkubwa lakini airport kama nyumba ya mtumishi wa serikali?

Jiulize hayo maswali pia yatakusaidia kupata majibu ya swali lako
 
Sio wote hutokea Dar......kuna waliowahi kutokea Mwanza na Arusha......ila hata mimi inanishangaza.....kwa nini hawatoki Tabora, Singida, Shinyanga na hata Mbeya?......

labda maandalizi/faragha kati ya majaji na mamiss huanza miezi kadhaa nyuma kabla ya mashindano yenyewe. Na walio dar ndiyo rahisi kufikiwa.
 
miaka kama mitatu hivi iliyopita washindi walitoka mwanza mara mbili mfurulizo mimi ni mnazi sana wa mwanza lakini sikufurahishwa na ushindi huo kwakua ungevutia mabinti wetu weni kuwa wanashiriki katika mashindano hayo ya kikahaba
 
Back
Top Bottom