Kwa nini misiba ya siku hizi hasa ya wakristo ni kama sherehe tu !?

Wasalaam waungwana

Miaka ya nyuma suala la msiba lilikua ni la kuhuzunisha sana yani nyumba ya wafiwa inagubikwa na vilio,simanzi na masikitiko

Majirani na watu wengine wanawafariji wafiwa,huku mchango ukipita ili kuandaa chochote kitu kwa ajili ya waliohudhuria mazishini

Kaburi linachimbwa jeneza linaletwa linafukiwa udongoni na kuhitimisha Yale maandiko ya kuwa tumetoka udongoni na udongoni tutarejea

Baada ya maziko watu wanarudi nyumbani maisha yanaendelea

Ila siku hizi msiba umekua sherehe unakodiwa muziki mnene zitapigwa nyimbo za kila aina ,bia zitanyweka na mavyakula ya kila aina yataliwa

Wafiwa nao wanalia kidogo tu baada ya hapo wanapata nguvu ya kupiga selfie na kutupiwa mtandao huku wakijifanya kuwa na huzuni kuu

Kaburi litachimbwa udongo utatupwa huko ,sasa malumalu inashika hatamu ,kaburi linapambwa jeneza linaingizwa juu linafuata zege la bei mbaya habari imekwisha

Sasa cha ajabu wakati marehemu anaumwa aliteseka sana kwa kukosa hela ya matibabu Leo amekufa hana thamani tena basi anagharamiwa na kufanyiwa sherehe baada ya yeye kufa

Je hali hii inasababishwa na utandawazi,kuiga tamaduni za nje au roho mbaya tu waliyo nayo watu hadi suala la huzuni kwao halipo!???
Kikawaida mwanadamu ana sherehe kuu tatu
kuzaliwa
kuoa au kuolewa
kifo
Hivyo sioni shida pale ndg wanapoamua kuyasheherekea maisha ya mpendwa wao katika safari yake ya mwisho hapa duniani
 
Sherehe zipo tatu kuzaliwa,ndoa na kifo.. zote ni sherehe... Wenye nazo wanasherehekea zote.. ila kwa wengine tunachagua moja ama mbili...

Sherehe ya kifo means umeyashinda ya dunia sasa unapumzika..
 
nikiitwa hukumuni rohoni nina amani
nikivikwa haki yake sina hofu mbele zake

kwanini tusikitike?
kufa ni faida
kuzaliwa kungekuwa hakuna maana
kama kufa kusingelikuwepo
 
Ukifa upelekwe fasta ukazikwe kwa mujibu wa Imani yako tukitoka huko tuna sherekea maisha yako kwa kula bata tuwezavyo kwa sababu harudi tena
 
Back
Top Bottom