Kwa nini mikutano ya mashirika ya hifadhi ya jamii yote hufanyikia Arusha?

masare

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
1,719
1,782
Wadau,
Nimekua nikijiuliza kwa muda mrefu hivi ni sababu gani kuu inayopelekea mikutano ya wadau kwenye haya mashirika ya hifadhi ya jamii kama NSSF,PSPF,PPF,LAPF na GEPF yote kufanyikia Arusha kila mwaka.
Je kuna sababu yoyote ya msingi ya kufanyikia Arusha na sio miji mingine.
Kwanini isifanyikie kwenye miji mingine ambayo inazo kumbi na hoteli za kuweza kuaccomodate wadau wengi kwa pamoja mfano Bagamoyo,Morogoro,Dodoma,DarEsSalaam n.k

Juzi mkutano mkuu wa 9 wa wadau wa mfuko wa hifadhi ya watumishi wa serikali za mitaa-LAPF umemalizika jijini Arusha.
Je kwanini usingefanyikia Dodoma ambapo ndipo makao makuu ya LAPF vilevile Dodoma ndipo katikati ya nchi hivyo kijiografia ni rahisi zaidi kuwakutanisha wadau wote kutoka kila pembe ya Tanzania kuliko Arusha.
Ieleweke pia Dodoma zipo kumbi za mikutano na mahoteli mengi kwamfano St Gaspar Conference Center,Morena Hotel,CCT Conference n.k ambayo yanaweza kuchukua idadi yoyote ya wahudhuriaji.

Hivi what is so special about Arusha hadi mashirika yote hayo yawe yanafanyia mikutano yao Arusha tu na sio miji mingine tena karibia kila mwaka.
 
Sasa huko kwenu Kigoma, watafanyia wapi?
Arusha wanachofuata ni facilities zilizopo Ukumbi mkubwa na Hotels pia
 
Ingefanyikia Morogoro ungehoji kwa nini Morogoro, ingefanyikia Mwanza ungehoji kwa nini mwanza, ingefanyikia Chato ungehoji kwa nini Chato,
Mbona Arusha au mikoa mingine hawaulizi kwa nini kila
Kitu kiko Dar es Salaam and whats so special about Dar na sio kwingine?
 
Bila shaka utakuwa mkazi wa Arachuga bi dada...ha ha ha ha!
 
Umesahau na uchaguz wa TLS nao pia utafanyka chuga...
Hii ndio geniva ya africa
 
jibuni hoja za mtoa mada sio ushabiki wa miji mliyozaliwa.
Swali kuu ni Je kwanini mikutano yote hiyo ifanyike Arusha ..!?What is so special about Arusha .Kama ni Conference plus Hotel facilities Je hizo hazipatikani miji mingine.Hivi kuna mji Tanzania wenye hotels na kumbi nyingi za kimataifa za mikutano kama Dar EsSalaam .Sasa huo ni mfano tu
Miji mingine tumeona pia imekua ikifanya vizuri kwenye masuala ya kuhost mikutano iwe ya mashirika ya ndani hata mikutano ya kimataifa kwamfano miji kama Bagamoyo,Tanga,Morogoro,Dodoma.

CCM wanafanyia mikutano yao Dodoma maelfu ya wanachama wanakua accommodated at per kwanini LAPF wasifanyie mikutano yao Dodoma sehemu ambayo ni makao makuu yao na vilevile makao makuu ya nchi hadi wang'ang'anie Arusha kila mwaka.Mwenye hoja zilizoenda shule na sio ushabiki ndio anijibu
 
Wadau,
Nimekua nikijiuliza kwa muda mrefu hivi ni sababu gani kuu inayopelekea mikutano ya wadau kwenye haya mashirika ya hifadhi ya jamii kama NSSF,PSPF,PPF,LAPF na GEPF yote kufanyikia Arusha kila mwaka.
Je kuna sababu yoyote ya msingi ya kufanyikia Arusha na sio miji mingine.
Kwanini isifanyikie kwenye miji mingine ambayo inazo kumbi na hoteli za kuweza kuaccomodate wadau wengi kwa pamoja mfano Bagamoyo,Morogoro,Dodoma,DarEsSalaam n.k

Juzi mkutano mkuu wa 9 wa wadau wa mfuko wa hifadhi ya watumishi wa serikali za mitaa-LAPF umemalizika jijini Arusha.
Je kwanini usingefanyikia Dodoma ambapo ndipo makao makuu ya LAPF vilevile Dodoma ndipo katikati ya nchi hivyo kijiografia ni rahisi zaidi kuwakutanisha wadau wote kutoka kila pembe ya Tanzania kuliko Arusha.
Ieleweke pia Dodoma zipo kumbi za mikutano na mahoteli mengi kwamfano St Gaspar Conference Center,Morena Hotel,CCT Conference n.k ambayo yanaweza kuchukua idadi yoyote ya wahudhuriaji.

Hivi what is so special about Arusha hadi mashirika yote hayo yawe yanafanyia mikutano yao Arusha tu na sio miji mingine tena karibia kila mwaka.
Kwa sababu ni Geneva ya Tanzania hutaki unaacha
 
Back
Top Bottom