Kwa nini mikorogo? Uzuri ni nini?

Kashaijabutege

JF-Expert Member
Oct 20, 2010
2,696
740
Huwa nachefuka sana nikiona mwanamke anapaka mkorogo ili awe mweupe. Inachefua unamkuta mama amekuwa mwekundu kama komamanga. Kwa nini weupe hawajibadili kuwa weusi? Ina maana weusi ni laana? Kwa ujumla tabia hii ya dada zetu na mama zetu inatudhalilisha Waafrika. Rangi yetu ni nzuri na ni adimu, kwa nini kina dada na mama hawaipendi?

Binafsi napenda mwanamke anayetunza uasilia wake. Kama mweusi, abaki mweusi. Kama mweupe abaki mweupe.

Kina baba wenzangu, mliojaribu, taste ya wanawake walio'jikoroga' ikoje?
 
Taratibu mkuu! Wakikusikia watakupiga mawe. Wengi ukiongea juu ya mikorogo ni kama unampigia mbuzi gitaa. Wengi wao hukasirika kabisa, wanaona unawaonea wivu au wewe umepitwa na wakati. Wanataka weupe kwa gharama yoyote kwani kwao weupe ndo uzuri, ndo urembo, ndo fashion, nk, nk. Tena cha ajabu wengine tayari kwa kuzaliwa ni weupe. Lakini utakuta wanajipakaa mikorogo ili wawe weupe zaidi. Hapo mtu unashindwa kuelewa kinachotafutwa ni kitu gani?!
 
Huwa nachefuka sana nikiona mwanamke anapaka mkorogo ili awe mweupe. Inachefua unamkuta mama amekuwa mwekundu kama komamanga. Kwa nini weupe hawajibadili kuwa weusi? Ina maana weusi ni laana? Kwa ujumla tabia hii ya dada zetu na mama zetu inatudhalilisha Waafrika. Rangi yetu ni nzuri na ni adimu, kwa nini kina dada na mama hawaipendi?

Binafsi napenda mwanamke anayetunza uasilia wake. Kama mweusi, abaki mweusi. Kama mweupe abaki mweupe.

Kina baba wenzangu, mliojaribu, taste ya wanawake walio'jikoroga' ikoje?

Kama ingekua sio dili wangeacha 'jikoroga' Mi sina tatizo nao ila wanaotumia 'vikorogeo' cheap bila kufuata instructions ; kukaa kwenye jua, kupika kwenye moto mkali, kuoga maji chumvi, kuchanganya visivyo changanyika but if used correctly viko poa
 
kwa kweli JF ni jungu kuu.
 
Siku hizi na wanaume wanapaka sana tu, wanamiziki wa Kongo ndio balaa, na hii in adhari kubwa sana, cancer ya ngozi inazidi sana kwa ajili ya hii mikorogo. Natamani tupate wanaharakati wa kufanya KAMPENI ZUIA MIKOROGO labda itasaidia kupunguza wapaka mikorogo.
 
Urembo una gharama zake banaa. Watu wanaweka silicone ndani ya miili yao kuongeza ukubwa wa maumbile ninyi mnashangaa mkorogo..
 
huwa nashindwa kuamini kama uzuri wa mtu unakuwa determined na weupe!ajabu ni kuwa hata vile vilivyokatazwa kutumika vikionekana kuwa na athari kny miili yetu ndivyo vinavyouzika zaidi madukani!nionavyo mimi kutumia mkorogo ni mtu kutokujikubali jinsi alivyo na kutojiamini,,haipendezi kabisa ila hata wanaume baadhi cku hizi naona nao wanajikoboa,,,lol
 
Ujinga tu!Sema wanaume nao wanachangia sana kuwadanganya wale walio tayari kudanganyika kwamba weupe ndio urembo!
 
ni kutokujiamini,na kuamini kuwa weupe ndio uzuri,wengine hujichubua mwili mzima,madhara yake watayaona baadae
 
Ukitaka kujua uafrika ni mali sasa hivi wazungu wanawake wanavaa soksi ndefu(sijui jina lake) zenye rangi ya mwafrika, ukiwa kwa mbali na kama hujamuona sura unaweze fikiri huyo dada ni mwafrika.
 
Weusi wazuri bana maana wakikufunua kunako mambo rangi ya huko ni swadakta kitu lazma kiende hewani tu
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom