Kwanini mikoa ya kusini ni masikini?

ishengom

Senior Member
Jul 23, 2012
152
67
Kilichonisukuma ni kutaka kujua umasikini wa mikoa ya kusini umetokana na nini wajkati historia inaonyesha kilwa ulikuwa mji mkubwa sana kibiashara na mambo mengi sna yalifadhika kwa mikoa ya kusini ya Tanzania

Sasa swali langu ni hivi kwanini mambo yamegeuka ka kuwa ni mikoa isiyojiweza kiuchumi ukilinganisha na mikia mingine ya Tanzania, natalajia kujifunza na kusikia mengi kutoka kwa wadau mbalimbali natangulisha shukrani!
 
Natumaini swali lako si la kisiasa !!
Ukitaka kupata majibu mazuri lazima uweke analysis yako kuhusu umasikini. Tuwekee vigezo vya umasikini unavyovitumia hadi kufikia hapo ulipo conclude kuwa ni masikini ili tuweze kujua umasikini upi unaoulenga ambao labda ni tofauti na ule wa Kondoa, Singida, Kasulu au Mpanda.

Unapouliza swali linaloelekea kuwa la la kihistoria usiishie hapo kwasababu historia ina dada zake kama jiografia, sosholojia na uchumi.

Ungeweza kujiuliza kwanini Timbuktu, moja ya falme kubwa zilizojulikana leo ni masikini sana.
 
ishengom, Nguruvi3,

..mimi nadhani ni kwasababu WANANCHI wa mikoa hiyo hawana mfumo mzuri wa mauzo/manunuzi ya MAZAO wanayozalisha.

..suala lingine ni kukosekana kwa MIUNDOMBINU ktk maeneo hayo kwa kipindi kirefu.

..mikoa ambayo ina ahueni kidogo ni ile ambayo WANANCHI wake wamebahatika kuwa na mfumo mzuri wa ununuzi wa mazao yao, na kuwepo kwa MIUNDOMBINU ya uhakika.

..najua wengine wanaweza kuleta hoja ya uvumbuzi wa GESI ktk maeneo ya kusini. jibu langu ni kwamba sekta hiyo haihusishi watu wengi kama ilivyo sekta ya KILIMO. nchi hii inaweza kuwa tajiri sana lakini wananchi wake wakabaki masikini kama hazitafanyika jitihada za kufufua KILIMO ambacho kinaajiri 70%++ ya population.
 
Last edited by a moderator:
tuzingatie kuwa historia ya uarabu imeathiri sana sehemu ambazo ziliingiliwa sana na waarabu na hasa waarabu wa eneo la Ghuba
 
pitia vitabu vya mohd said _untold story
sababu hasa ni chuki vita inayoendeshwa dhidi ya uislam na mikoa yenye waislam wengi.
 
Hilo swali ni la kumuliza BABA yako wa Taifa manake ndo chanzo cha yote unayotaka kujua.Ka chini utaelewa nilichokiandika
 
Back
Top Bottom